Jinsi nilivyonusurika kung'atwa na nyoka wakati nataka kumuokoa

Jinsi nilivyonusurika kung'atwa na nyoka wakati nataka kumuokoa

enzi nakua bana kijijini tumekaa tumetulia tunapia stori pembeni ya nyumba mara ghafra paka anakimbiza kitu kinamelemeta kinaelekea ndani ya nyumba,piga tochi kitu cheusi ndio kinamalizikia kuingia ndani kwenye kaupenyo ka mlango[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].

tukakaa tumepanick tusielewe tunaanzia wapi operation fukuza nyoka,masaa yanakwenda nikajitolea kushika tochi kuingia ndani na mpini wa jembe,murika mlango wote na mazingira andamizi sioni kitu,ndani ya nyumba ni carpet la mpira haya ya aftatu mita[emoji1787]kulikuwa na watoto wa paka umri ule wa kuchezacheza na kila kitu,mama yao ndio yule aliyetuletea janga,baada ya kutukabidhi msala katokomea.
sasa nikawa naskia kama kitu kinachezewa kwa zamu huko chini kinapigwa kinateleza shaaa,kupiga tochi hivi nakuta nyoka wa kijani[emoji23][emoji23][emoji23]kumbukeni aliyeingia ni mweusi,na huyu ameshakufa kitambo,nyieeeeeeeee mnaweza otea hali ilikuwaje[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
ikabidi nitoe taarifa jamani chini ya kochi kuna nyoka paka wanamchezea lakini sio mweusi,na ameshakufa[emoji53][emoji53][emoji53]sister angu akaongea kwa wenge "nipeni mito ya makochi na funguo za darasa nilale darasani mimi ndani leo humu silali hata kwa dawa",tukamtoa kwa uangalifu,tukaanza kumtafuta huyo mweusi sasa,tafuta sana,mulika kwenye bati juu,lahaula[emoji2][emoji2]juu ya kuta pembeni mwamba huyu hapa,gues what wa kijani tena,tukaanza kutoleana macho mbona kama kuna mkono wa mtu hapa,sister hata morali wa kwenda kulala huko darasani umekata ameanza kukemea mapepo[emoji16][emoji16].naye akauwawa.
ikabidi lije wazo yamwangwe mafuta ya taa ndani ila tusilale tubebe mito na mikeka tukaangushe madarasani.mafuta ya taa yakapigwa sehemu ambazo anazaniwa anawezakuwa kajificha,wakati nahangaika kutoka mikeka na mito ya makochi,ghafla naskia paka anapurukusha,kumbe alikuwa anajaribu kutoka mafichoni akakutana na wale paka wadogo ndio wamemuweka kati,tukamalizia tukamtupa nje,ila kulala ilikuwa ni lazima tukalale darasani hakukuwa na namna.kumbe mchana kutwa kulikuwa na moto mapori ya jirani.

by the way nyoka wauaji wote ni ngumu sana kukutana na binaadam,na wao wanajificha sehemu pweke sana hawapendi muingiliano,hawa wengine wanasababisha wenge tu akikuuma.
 
Mi mwenyewe hua siwezi kuwaua. Hua nawaacha wanaenda zao kikubwa nahakikisha wanaenda maaeneo ambayo hawawezi kukutana na watu. Kuna mmoja alidumbukia kwenye shimo flani jamaa alikuwa anachimba septic tank nikamuona anahangaika kutoka nilichofanya nilitafuta miti nikatengeneza kama ngazi nikaweka mule akapanda akatoka sema akanichenjia nikakimbia
Huyo ilitakiwa umwagie mafuta ya taa na si kumjengea ngazi. Tambua nyoka ni adui yako milele na milele
 
mtu anayependa nyoka na kuwaonea huruma huwa ninaona ana traces za ushirikina
You miss the point sir..sio kwamba nawaonea huruma nyoka tu bali ni viumbe wote hua siwaui kabisa. Except mbu
 
Ndiyo maana siafu hawana sumu mkuu..
Na hata nyoka hawa wa kitaa huwa hawana noma, sema wenge letu tu binadamu kutokana fikra zetu juu ya nyoka. Siafu wana madhara makubwa wakiingia usiku ukiwa usingizini kuliko nyoka alafu wamkute mtoto au mgonjwa hajiwezi anakwenda na maji lakini nyoka anapiga kimya hata mwezi na kama kuna panya na usafi na mpangilio wa vitu ni sifuri mtaishi nae vizuri anaweza akapita hata kwenye miguu kama ni giza na hakugongi
 
Kama unawarumia, mfano ukimuacha na akamuuma mtu, huoni ni kosa lako la kutokumuuwa? Nyoka ni nyoka tu ukipata chance muangamize.
 
harakati za siri I took the liberty of narrating it for you....No scary snake pics

Kwasababu zangu binafsi ambazo sitapenda niziseme (but very reasonable) hua siui kiumbe yoyote aliye hai tofauti na mbu. Kiukweli siwapendi na nawaogopa sana nyoka ila hata wao imekua ikiniwea vigumu kuwaua hivyo pindi napokutana nao hua naishia kuwafukuza au kuwapotezea kama wameenda eneo ambalo mimi sifiki au watu wengine. Sehemu Fulani nilipokua nakaa kulikua na kisima kisicho na maji humo ndani kuna nyoka alikua akishi humo hadi akawa na watoto kwakweli iliniwea vigumu kumuua japo wananchi weye hasira kali walikuja wakateketeza ile familia, Fast-forwarding

Siku moja natembea barabarani usiku nikakutana na nyoka mdogo yupo katikati ya barabara kashindwa kuvuka ajili ya mwanga wa maloli yaliyokua yanapita, mimi nikaenda kwa nia njema kabisa nimsaidie avuke upande wa pili cha ajabu nilipomfikia akainua kichwa juu anaigonge/ng’ate, nikawa namkwepa. Kila nikimfukuza aende upande wa pili anakua ananijia aning’ate kwakweli nikashindwa kumsaidia ikabidi nimuache roli likamgonga. Iliniuma kiasi maana nilikua nina nafasi ya kumsaidia ila nilishindwa.
Unadhani kwanini japo nia yangu ilikua ni njema kumsaidia maisha yake lakini aliniona adui na kutaka kunigonga?

Kwa mujibu wa biblia baada ya wanadamu wa kwanza kufanya maasi Mungu alitoa laana kati ya nyoka na mwanadamu kwa kusema “name nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino” kwa mantiki hiyo watu wengi huchukulia kwamba hiyo laana aliyotoa Mungu kati ya binaadamu na nyoka ndio inafanya mwanadamu na nyoka waviziane kumuua mwingine lakini mimi nasema hiyo sio kweli laana hiyo aliotoa Mungu sio sababu bali ilitumika kama fumbo. Maana kubwa aliyomaanisha mungu ni kwamba ujuzi wa mema na mabaya walioupata wanadamu kwa kula tunda/kuasi ndio unaofanya mwanadamu na nyoka wawindane….nitajaribu kulielezea hili kisayansi zaid ili nieleweke vizuri.

Catecholamine The Adrenaline

Endocrine Glands ni mfumo wa tezi ambao wenyewe hutoa hutoa homoni moja kwa moja kwenda kwenye mfumo/mzunguko wa damu wa damu.

Adrenal Gland ni tezi iliyopo katika mfumo watezi ambayo inapatikana juu ya mafigo kazi kuu ya tezi hii ni kuweka sawa kiwango cha chumvi na kurekebisha kiwango cha musukumo wa damu. tezi hii hutengeneza homoni mbali mbalimbali kama viel cortisol,epinephrine,catecholamine nk pia hutengeneza homoni ya adrenaline, adrenaline hutengenezwa pia katika medulla oblongata kwa kiwango kidogo….Pindi unapokua na hasira au unapoona kitu cha hatari kama vile nyoka tezi hii ya Adrenal hutoa homoni ya epinephrine, husababisha kutengenezwa kwa homoni ya cortisol, ambayo huongeza shinikizo la damu, sukari ya damu, na kukandamiza mfumo wa kinga.Mwitikio wa awali na miitikio inayofuata huchochewa katika jitihada za kuunda nyongeza ya nishati. Ongezeko hili la nishati huamlishwa na epinephrine kujifunga kwa seli za ini na uzalishaji unaofuata wa glucose.

mzunguko wa cortisol hufanya kazi kugeuza asidi ya mafuta kuwa nishati inayopatikana, ambayo hutayarisha misuli ya mwili mzima kwa majibu/reaction. Homoni za catecholamine, kama vile adrenaline (epinephrine) au noradrenalini (norepinephrine), husaidia reaction ya haraka ya mwili ambayo huhusiana na maandalizi ya misuli kuchukua hatua kali…..Misuli inapofikia hatua hiyo unapofikia katika hatua hiyo moyo na mapafu huongezeka kasi yaani mapigo ya moyo yataenda haraka na mtu mtu atakua anapumua haraka, huziwia tezi ya Lacrimal ambayo hufanya kazi ya kuzalisha machozi na mate ndio maana ukiwa umeona kitu cha hatari mate na koo hukauka…pia kutetemeka mwili. Baada ya haya yote kutokea mwili ndio mwanadamu ataamua akimbie hatari(flight) au apambane na hatari(fight.

Vomeronasal organ (VNO) ni sehemu/mlango/sense organi ya ziada iliyopo juu ndani yam domo kwa juu ambayo hutumika katika kunusa mara nyingi organ hii hupatikana zaidi katika nyoka na mijusi. VNO wa jina lingine inaitwa Jacobson Gland. Katika nyoka Tezi hii ya VNO ina uwezo mkubwa sana wa kunusa Scent za vitu….Kama nilivyoelezea huko juu kwamba mwanada mu ukiona kitu cha kutisha Adreanal Gland ina activate reaction ya Fight or Flight kumbuka kwamba mwili ukishakua kwenye reaction hiyo hormone mbalimbali zinazoachiliwa (Adrenaline) zinasambaa katika damu yako hivyo basi nyoka kwa kutumia tezi ya VNO/Jacobson gland huweza kuunusa mwili wako na kugundua kwamba mtu huyu ni adaui kwangu nae atajihmi maana atakusikia harafu yako ni tofauti ajili ya hormones hizo.

Mwanzo kwenye mada nimeeleza nilivyotaka kung’atwa na nyoka nikiwa nataka kumsaidia sababu ni kwamba alisikia scent ya mwili wangu iliyotokana na homoni mbalimbali zilizoachiliwa katika kutekeleza reaction ya fight or flight….Kawaida ya nyoka kama yupo ndani usipomuona wala kumkanyaga hawezi kukudhuru kabisa lakini pindi utakapomuona tu basi naye atajitahidi ajihami kwani kama hujamuona mwali wako unakua upo sawa kabisa lakini pindi utakapomuona tu mwili wako utabadirika kwani utakua unajua ile ni hatari.

Kwa mantiki hiyo uadui uliopo kati ya nyoka na mwanadamu unatokana na ujuzi wetu wa kujua baya na jema kwani kujua nyoka huyu ni adui sio mwema ndio huactivate Adrenal gland kama tungekua hatujui jema na baya basi kamwe tusingekua na uadui na nyoka ndio maana mtoto mdogo chini ya miaka miwili anaweza kucheza na nyoka mkali na asing’atwe kamwe lakini kama mama yake atatokea na kumuona mtoto akicheza na nyoka basi anaweza sababisha kweli nyoka akamng’ata mtoto maana mama anajua jema na baya so akimuona nyoka na mtoto ni lazima apige kelelemna wakati huo adrenaline itakua tayari ishasambaa mwilini nyoka ataisikia scent na kujua huyu ni adui kelele za mama zitamtia uoga mtoto kisha aanze kulia maana mtoto atahisi labda kuna hatari ndio maana mama yake anapiga kelele. Ile kuhisi hatari kwa mtoto nako ni adrenal nayo inakua inaanza kufanya kazi so hapo inakua ni utashi wa nyoka mwenyewe atakachoamua.

Hivyo Yule nyoka japo mimi nilikua nina nia njema ya kumsaidia lakini nilimfuata mwili wangu ukiwa katika hali ya fight or flight kwani najua Yule ni mbaya kwangu hivyo nyoka hakuangalia dhamira yangu bali alifuata sense yake ya Jacobson gland.
….
Hii ni theory yang tu kutokana na uelewa wangu wasayansi inawezekana sipo sahihi hivyo basi ruhusa kwenu kunikosoa na kusahihisha pale nilipokosea.
-Criston Cole
Mkuu nashkuru Kwa Andiko zuri na lenye madini mazuri sana

ila nadhani kuna sehemu hatujaenda Sawa, unaposema uwezo wa kujua Mema na mabaya katika mada yako haina uhusiano na mtu kung'atwa na nyoka au kinyume chake

Ukisema Jema na Baya utapata tafsiri tofauti kutoka Kwa kila jumuiya, kwenu kitu kibaya kinaweza kikawa kizuri Kwa wengine, au katazo la kabira fulani linaweza kuwa sio katazo katika kabira lingine, kwahiyo hakuna definition sahihi ya Jema na Baya

Nadhani ulipaswa kuongelea HATARI/USALAMA, hiki ndio kinafanya either nyona akuduru au asikudhuru maana Kuna tofauti Kati ya JEMA/BAYA na HATARI/SALAMA, kujua kwako jema au baya hakukufanyi ung'atwe au using'atwe na Nyoka

Kinachokufanya using'atwe ni kujua either ni hatari au salama, mtoto mdogo haumwi na nyoka sio Kwa sababu hajui Jambo jema na Baya lahasha haumwi Kwa sababu hajui kutofautisha hatari na salama

Na wasioumwa na nyoka sio watoto tu bali ata wakubwa pia wapo ambao hawana hofu ya nyoka japokuwa wanajua Jambo jema na Baya, ukizoea kuwa karibu na nyoka hiyo hali itakufanya uwe una feel normal towards them

Na kama utakuwa kawaida kabisa mbele yao basi kupelekea mfumo wako wa hormone usi react kuzalisha hormone ya uoga hivo nyoka hatokuona kama wewe ni hatari kwake na kufanya asi react tofauti

Kuna muda sie tuliekuwa tunaenda kuchezea nyoka sehemu Fulani, wale wenyeji wetu wanatuelekeza ni namna gani ufanye ili nyoka awe kawaida kwako, na moja ya njia hiyo ni kupumua vizuri na kumfanya nyoka ajifeel yuko sehemu salama

Kama utaweza kubalance uhemaji wako na mapigo ya moyo ni hapo hormone ya uoga huondoka mwilini na utaweza kushika nyoka, ila endapo Kwa makusudi au bahati mbaya ikatokea mtu akakutisha ghafra ukiwa umeshika nyoka basi yule nyoka atakung'ata

Jambo zuri ni kwamba hiyo michezo tulikuwa tunaifanya kwa wale nyoka wasiokuwa kuwa na sumu kama pythons au wale ambao wameondolewa Meno, kwahiyo ata aki react kukung'ata anakuwa hajakudhuru

Kwahiyo nachelea kusema kwamba sio KWELI kwamba nyoka anang'ata/kugonga mtu Kwa sababu anajua Jema na Baya, bali atang'ata/kugonga mtu Kwa sababu anajua tofauti ya hatari na salama

Masai wanauwa Simba na kuogopwa na Simba sio Kwa sababu Masai hajui Jema na Baya ispokuwa kwakuwa Masai anabadirisha hali ya Hatari na kuitafsiri kinyume kuwa ni salama hivo endocrine system itakuwa normal muda wote na kupelekea Simba kuwa na hofu mbele ya Masai na yeye ndio kupoteza kujiamini

Mind you, kuna nyoka ambao wao by nature tu ni wakorofi kwahiyo hawaathiriwi na mfumo wa hormone zako, either adrenaline izalishwe au isizalishwe wewe unakuwa katika hatari ya kuzulika

na baadhi ya hao nyoka ni Black Mamba huyu hanaga usela na binadamu ata siku moja, yeye muda wowote yule anakuchenjia ata kama wewe ndio unamfuga na always unatakiwa kuwa makini sana unapokuwa karibu nao

Mwisho kabisa, katika ukoo wetu sie hatuuwi nyoka na hiyo kupelekea kuwa tunafeel normal pindi tunapowaona, japokuwa Kwa mara ya Kwanza naskia haya nilipoenda Kwa Bibi yangu nilikuwa muoga sana ila badae nikazoea
 
Unaweza ishi na Koboko(hata nyoka wengine pia) zaidi ya Miaka 100 asikudhuru ila sharti ni moja tu" nyoka ndiye ajue uwepo wa binadamu eneo ilo ila si binadamu ndiye ajue kuna nyoka eneo ilo".. Hii ni kwa uzoefu binafsi na kusoma maandishi kama haya.
Duu! Fafanua kdg
 
Mkuu sio wa mchongo hata kidogo, kuna nyoka aliuawa wiki 2 zilizopita dodoma nikishuhudia kwa macho yangu nami ilibidi nishirikiane kumuua alikua ni mrefu kama futi 5.6 hala mnene kama mkono wangu alikua Cobra. Aisee alivyokua akipanua shingo na kurusha mate utadhani kabisa wale wa kwenye tv. Ila aliuawa.

Maneo ya kanda ya kati hasa Tabora na singida kuna nyoka wengi sana sana. Singida wamejaa Cobra watupu kama wale wa kihindi na Tabora ni Koboko tu. Nyoka wa tabora wanakula hadi vitumbua, wanakula tui la nazi, wanakula ubwabwa nk nk😅
😁😁😁 Tabora kuna mahala tulikuwa tumeenda kufunga pump ( igombe ) kwa ajiri ya kusukuma maji enzi hizo, unaambiwa pale ambapo tunakaa au kulala juu yake kuna koboko wanaishi.. yani kule Tabora koboko kama gugwaa ( panzi ).


Singida nahisi itakuwa kuna maeneo na maeno yenye nyoka nimekaa ukiwa unatoka puma unaenda kushoto ndio ndio nilikutana na manyoka kula kama vitoweo, sikurudi tena
 
Back
Top Bottom