Ant vemonFirst aid ya nini Sir?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ant vemonFirst aid ya nini Sir?
Ngoja nitafuatilia nijue what's special about Queen bees. Sasa kwanini hua hawaondoki wote Kama hua wanasense Hatariinasemekana malkia huondoka mapema sana! na hao nyuki hufuata nyayo zake, ktk safari yao wakichoka hupumzika kwa kurundikana sehemu kisha safari inaendelea
Halafu kipindi hiki cha mvua hua wanapenda kupanda kitandani unajifunika nae shuka. Utasikia tu ubaridi na kuteleza ukimulika unamuona mzee baba kajikunja kama kata. Angalia chini ya mto🏃Haaa hamna kiumbe namuogopa kama nyoka, hapa nimeanza kukagua uvunguni uwii😒
Kuna ile jiwe jeusi ambalo tunalitumia kutoa sumu ya nyoka akikung'ata scientifically is correct. Lile jiwe linaweza ondoa sumu lakini kwa kiwangu kiasi tu. Usidanganywe kua kila nyoka hilo jiwe linaweza kutoa sumu sema kinachotusaidia ni kwamba Africa nyoka wengi hawana sumu kali (Ukimtoa Black mamba) wengine hawana sumu kabisa.Criston Cole ahsante sana umenifungua ubongo wangu kisayansi.Mimi nimesoma biology kama wewe ila kwenye endocrinology sio mjuzi sana
Sasa nimepata picha kuwa ni kwanini ukikutana na simba uso kwa uso ukamuangalia sana wala hutetereki anaona aibu kukudhuru hata anaweza kukutisha lakini ukiwa attentive unamuangalia tu na usimpe kisogo unarudi kinyume nyume nayeye machale yanamcheza anajua hapa maji marefu hakufanyi kitu na anaweza kutimka zake.
Pia nimepata picha ni kwanini nyoka haumi mtoto mdogo.Watu wanapelekea kukimbilia ni malaika kumbe ndani yake ni sayansi tupu hapo.Mfano mwingine kwenye ajali mtoto mdogo anaweza pona watu wote wakafa watu wanasema ni malaika kumbe hawajui uzito wa mtoto ulivyo mdogo ukizidisha na mwendo wa gari momentum yake inakuwa ni ndogo hivyo impact inakuwa ndogo kwake wengine mnakufa afterall watu wenye mauzito makubwa ndio wa kwanza kutangulia mbele ya haki kwenye ajali hapa nimeenda pembeni kidogo ya mada yako lakini najaribu kuelezea sayansi inavyoelezea wakati kwenye dini ni shortcut tu malaika
Pia nimepata picha ni kwanini ukienda nyumba ya mtu kama kuna mbwa akibweka wewe huna habari anaweza akakuacha lakini ukimpa kisogo tu anajua umeogopa anakukimbiza kumbe anakuwa amenusa ile hormone anajua huyu ni kibaka tu
Umeandika sana kujaribu kuunganisha dini na sayansi lakini nimeshagundua hilo la kusema nitaweka uadui kati yenu kumbe liko kisayansi kuliko tunavyofikiria sisi
Umenipanua akili mno hata hivyo natafuta namna naku inbox tuzidi kuwasiliana
Usikate tamaa humu wako watao kukejeli ulicho andika ila tuliosoma sayansi tumekupata
Aaah usinifanyie hivo mkuu, mwili unasisimka kabisa😪 kuna siku home natoka nje hamadi mzee baba huyu hapa nilikimbia kurudi ndani nikapanda kwenye kiti, mama ndiyo akatoka kumpiga aah alinicheka sanaHalafu kipindi hiki cha mvua hua wanapenda kupanda kitandani unajifunika nae shuka. Utasikia tu ubaridi na kuteleza ukimulika unamuona mzee baba kajikunja kama kata. Angalia chini ya mto🏃
Sir.. Thanks so much for clarification.Mkuu nashkuru Kwa Andiko zuri na lenye madini mazuri sana
ila nadhani kuna sehemu hatujaenda Sawa, unaposema uwezo wa kujua Mema na mabaya katika mada yako haina uhusiano na mtu kung'atwa na nyoka au kinyume chake
Ukisema Jema na Baya utapata tafsiri tofauti kutoka Kwa kila jumuiya, kwenu kitu kibaya kinaweza kikawa kizuri Kwa wengine, au katazo la kabira fulani linaweza kuwa sio katazo katika kabira lingine, kwahiyo hakuna definition sahihi ya Jema na Baya
Nadhani ulipaswa kuongelea HATARI/USALAMA, hiki ndio kinafanya either nyona akuduru au asikudhuru maana Kuna tofauti Kati ya JEMA/BAYA na HATARI/SALAMA, kujua kwako jema au baya hakukufanyi ung'atwe au using'atwe na Nyoka
Kinachokufanya using'atwe ni kujua either ni hatari au salama, mtoto mdogo haumwi na nyoka sio Kwa sababu hajui Jambo jema na Baya lahasha haumwi Kwa sababu hajui kutofautisha hatari na salama
Na wasioumwa na nyoka sio watoto tu bali ata wakubwa pia wapo ambao hawana hofu ya nyoka japokuwa wanajua Jambo jema na Baya, ukizoea kuwa karibu na nyoka hiyo hali itakufanya uwe una feel normal towards them
Na kama utakuwa kawaida kabisa mbele yao basi kupelekea mfumo wako wa hormone usi react kuzalisha hormone ya uoga hivo nyoka hatokuona kama wewe ni hatari kwake na kufanya asi react tofauti
Kuna muda sie tuliekuwa tunaenda kuchezea nyoka sehemu Fulani, wale wenyeji wetu wanatuelekeza ni namna gani ufanye ili nyoka awe kawaida kwako, na moja ya njia hiyo ni kupumua vizuri na kumfanya nyoka ajifeel yuko sehemu salama
Kama utaweza kubalance uhemaji wako na mapigo ya moyo ni hapo hormone ya uoga huondoka mwilini na utaweza kushika nyoka, ila endapo Kwa makusudi au bahati mbaya ikatokea mtu akakutisha ghafra ukiwa umeshika nyoka basi yule nyoka atakung'ata
Jambo zuri ni kwamba hiyo michezo tulikuwa tunaifanya kwa wale nyoka wasiokuwa kuwa na sumu kama pythons au wale ambao wameondolewa Meno, kwahiyo ata aki react kukung'ata anakuwa hajakudhuru
Kwahiyo nachelea kusema kwamba sio KWELI kwamba nyoka anang'ata/kugonga mtu Kwa sababu anajua Jema na Baya, bali atang'ata/kugonga mtu Kwa sababu anajua tofauti ya hatari na salama
Masai wanauwa Simba na kuogopwa na Simba sio Kwa sababu Masai hajui Jema na Baya ispokuwa kwakuwa Masai anabadirisha hali ya Hatari na kuitafsiri kinyume kuwa ni salama hivo endocrine system itakuwa normal muda wote na kupelekea Simba kuwa na hofu mbele ya Masai na yeye ndio kupoteza kujiamini
Mind you, kuna nyoka ambao wao by nature tu ni wakorofi kwahiyo hawaathiriwi na mfumo wa hormone zako, either adrenaline izalishwe au isizalishwe wewe unakuwa katika hatari ya kuzulika
na baadhi ya hao nyoka ni Black Mamba huyu hanaga usela na binadamu ata siku moja, yeye muda wowote yule anakuchenjia ata kama wewe ndio unamfuga na always unatakiwa kuwa makini sana unapokuwa karibu nao
Mwisho kabisa, katika ukoo wetu sie hatuuwi nyoka na hiyo kupelekea kuwa tunafeel normal pindi tunapowaona, japokuwa Kwa mara ya Kwanza naskia haya nilipoenda Kwa Bibi yangu nilikuwa muoga sana ila badae nikazoea
Pole sana sasa kwenye kiti si angeinua kichwa tu akakudokoa. Nyoka akiingia ndani ya sofa lako akiwa mdogo anatoka akiwa anaconda kabisa na watoto kadhaa..Aaah usinifanyie hivo mkuu, mwili unasisimka kabisa😪 kuna siku home natoka nje hamadi mzee baba huyu hapa nilikimbia kurudi ndani nikapanda kwenye kiti, mama ndiyo akatoka kumpiga aah alinicheka sana
Hv nn maana halisi ya juice!?maana kila mkorogo ck hz unaitwa juice!!Juice ya unga wa mkaa ukinywa usaidia kufyonza sumu je KWA sumu ya nyoka inaweza fyonza pia? Wakati ukijiandaa kwenda kituo cha afya
Ooh wanazaliana ndani ya sofa? Tobaa, kwenye kiti niliassume hawezi kuniona hivo angepita zake chini😂Pole sana sasa kwenye kiti si angeinua kichwa tu akakudokoa. Nyoka akiingia ndani ya sofa lako akiwa mdogo anatoka akiwa anaconda kabisa na watoto kadhaa..
PS. Usiogope niko hapa nitakulinda🤗
Hivi niliskia eti nyoka ukimmwagia mafuta ya taa anakatika vipande vipande kweli?Anakua anakula panya tu humo anajinenepea zake hana stress. 😅
Hizo ni myths tuu.Hivi niliskia eti nyoka ukimmwagia mafuta ya taa anakatika vipande vipande kweli?
No. Ndo kwanza nimejiunga jf sina muda sana..ni miezi hii tu nimeanza kuitumia zaid jf