Jinsi nilivyonusurika kung'atwa na nyoka wakati nataka kumuokoa

Jinsi nilivyonusurika kung'atwa na nyoka wakati nataka kumuokoa

Huruma na wanyama
c3812c31ecf4499f98cd6bebfeae2c80.jpg
 
Juice ya unga wa mkaa ukinywa usaidia kufyonza sumu je KWA sumu ya nyoka inaweza fyonza pia? Wakati ukijiandaa kwenda kituo cha afya
Juice ya mkaa ni kwa ajili ya sumu iliyoingia orally au tumeseme mdomoni. Kwa nyoka haisaidia maana inaingia mwilini mwako kwa IV yaani Intravenous au tuseme moja kwa moja kwenye mishipa ya damu
First aid kubwa ya kwanza ni kufunga kamba sehemu ya juu damu isiende kwenye moyo.Halafu kwa haraka sana ni kuchanja sehemu ya jeraha kwa chale bila kuwa mwoga na kutoa kama kuna meno yamebakia hii inatka roho ngumu maana ni maumivu makali.Kisha kama huna jiwe la nyoka unachukua mkaa huo unaubandika juu ya jereha kisha unakwenda hospitali.Angalizo chonde chonde ukisema utembee na hospital ni mbali damu itakuwa imefika mbali kama kuna usafiri wa haraka sana wa gari upelekwe hospitali.Ila pia inategemea na aina ya nyoka aliyekuuma kama ni black mamba RIP inakuwa karibu sana maana unakuwana dakika tu za kuishi
 
Kwasababu zangu binafsi ambazo sitapenda niziseme (but very reasonable) hua siui kiumbe yoyote aliye hai tofauti na mbu. Kiukweli siwapendi na nawaogopa sana nyoka ila hata wao imekua ikiniwea vigumu kuwaua hivyo pindi napokutana nao hua naishia kuwafukuza au kuwapotezea kama wameenda eneo ambalo mimi sifiki au watu wengine. Sehemu Fulani nilipokua nakaa kulikua na kisima kisicho na maji humo ndani kuna nyoka alikua akishi humo hadi akawa na watoto kwakweli iliniwea vigumu kumuua japo wananchi weye hasira kali walikuja wakateketeza ile familia, Fast-forwarding

Siku moja natembea barabarani usiku nikakutana na nyoka mdogo yupo katikati ya barabara kashindwa kuvuka ajili ya mwanga wa maloli yaliyokua yanapita, mimi nikaenda kwa nia njema kabisa nimsaidie avuke upande wa pili cha ajabu nilipomfikia akainua kichwa juu anaigonge/ng’ate, nikawa namkwepa. Kila nikimfukuza aende upande wa pili anakua ananijia aning’ate kwakweli nikashindwa kumsaidia ikabidi nimuache roli likamgonga. Iliniuma kiasi maana nilikua nina nafasi ya kumsaidia ila nilishindwa.

Unadhani kwanini japo nia yangu ilikua ni njema kumsaidia maisha yake lakini aliniona adui na kutaka kunigonga?
Kwa mujibu wa biblia baada ya wanadamu wa kwanza kufanya maasi Mungu alitoa laana kati ya nyoka na mwanadamu kwa kusema “name nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino” kwa mantiki hiyo watu wengi huchukulia kwamba hiyo laana aliyotoa Mungu kati ya binaadamu na nyoka ndio inafanya mwanadamu na nyoka waviziane kumuua mwingine lakini mimi nasema hiyo sio kweli laana hiyo aliotoa Mungu sio sababu bali ilitumika kama fumbo. Maana kubwa aliyomaanisha mungu ni kwamba ujuzi wa mema na mabaya walioupata wanadamu kwa kula tunda/kuasi ndio unaofanya mwanadamu na nyoka wawindane….nitajaribu kulielezea hili kisayansi zaid ili nieleweke vizuri.

Catecholamine The Adrenaline

Endocrine Glands
ni mfumo wa tezi ambao wenyewe hutoa hutoa homoni moja kwa moja kwenda kwenye mfumo/mzunguko wa damu wa damu. Adrenal Gland ni tezi iliyopo katika mfumo watezi ambayo inapatikana juu ya mafigo kazi kuu ya tezi hii ni kuweka sawa kiwango cha chumvi na kurekebisha kiwango cha musukumo wa damu. tezi hii hutengeneza homoni mbali mbalimbali kama vile cortisol,epinephrine,catecholamine nk pia hutengeneza homoni ya adrenaline, adrenaline hutengenezwa pia katika medulla oblongata kwa kiwango kidogo

Pindi unapokua na hasira au unapoona kitu cha hatari kama vile nyoka tezi hii ya Adrenal hutoa homoni ya epinephrine, husababisha kutengenezwa kwa homoni ya cortisol, ambayo huongeza shinikizo la damu, sukari ya damu, na kukandamiza mfumo wa kinga.Mwitikio wa awali na miitikio inayofuata huchochewa katika jitihada za kuunda nyongeza ya nishati. Ongezeko hili la nishati huamlishwa na epinephrine kujifunga kwa seli za ini na uzalishaji unaofuata wa glucose.

NB: Adrenaline hufahamika pia kama Epinephrine

mzunguko wa cortisol hufanya kazi kugeuza asidi ya mafuta kuwa nishati inayopatikana, ambayo hutayarisha misuli ya mwili mzima kwa majibu/reaction. Homoni za catecholamine, kama vile adrenaline (epinephrine) au noradrenalini (norepinephrine), husaidia reaction ya haraka ya mwili ambayo huhusiana na maandalizi ya misuli kuchukua hatua kali…..Misuli inapofikia hatua hiyo unapofikia katika hatua hiyo moyo na mapafu huongezeka kasi yaani mapigo ya moyo yataenda haraka na mtu mtu atakua anapumua haraka, huziwia tezi ya Lacrimal ambayo hufanya kazi ya kuzalisha machozi na mate ndio maana ukiwa umeona kitu cha hatari mate na koo hukauka…pia kutetemeka mwili. Baada ya haya yote kutokea mwili ndio mwanadamu ataamua akimbie hatari(flight) au apambane na hatari(fight.
View attachment 2446763

Vomeronasal organ (VNO) ni sehemu/mlango/sense organi ya ziada iliyopo juu ndani yam domo kwa juu ambayo hutumika katika kunusa mara nyingi organ hii hupatikana zaidi katika nyoka na mijusi. VNO wa jina lingine inaitwa Jacobson Gland. Katika nyoka Tezi hii ya VNO ina uwezo mkubwa sana wa kunusa Scent za vitu….Kama nilivyoelezea huko juu kwamba mwanada mu ukiona kitu cha kutisha Adreanal Gland ina activate reaction ya Fight or Flight kumbuka kwamba mwili ukishakua kwenye reaction hiyo hormone mbalimbali zinazoachiliwa (Adrenaline) zinasambaa katika damu yako hivyo basi nyoka kwa kutumia tezi ya VNO/Jacobson gland huweza kuunusa mwili wako na kugundua kwamba mtu huyu ni adaui kwangu nae atajihmi maana atakusikia harafu yako ni tofauti ajili ya hormones hizo.
View attachment 2446749
Mwanzo kwenye mada nimeeleza nilivyotaka kung’atwa na nyoka nikiwa nataka kumsaidia sababu ni kwamba alisikia scent ya mwili wangu iliyotokana na homoni mbalimbali zilizoachiliwa katika kutekeleza reaction ya fight or flight….Kawaida ya nyoka kama yupo ndani usipomuona wala kumkanyaga hawezi kukudhuru kabisa lakini pindi utakapomuona tu basi naye atajitahidi ajihami kwani kama hujamuona mwali wako unakua upo sawa kabisa lakini pindi utakapomuona tu mwili wako utabadirika kwani utakua unajua ile ni hatari.

Kwa mantiki hiyo uadui uliopo kati ya nyoka na mwanadamu unatokana na ujuzi wetu wa kujua baya na jema kwani kujua nyoka huyu ni adui sio mwema ndio huactivate Adrenal gland kama tungekua hatujui jema na baya basi kamwe tusingekua na uadui na nyoka ndio maana mtoto mdogo chini ya miaka miwili anaweza kucheza na nyoka mkali na asing’atwe kamwe lakini kama mama yake atatokea na kumuona mtoto akicheza na nyoka basi anaweza sababisha kweli nyoka akamng’ata mtoto maana mama anajua jema na baya so akimuona nyoka na mtoto ni lazima apige kelelemna wakati huo adrenaline itakua tayari ishasambaa mwilini nyoka ataisikia scent na kujua huyu ni adui kelele za mama zitamtia uoga mtoto kisha aanze kulia maana mtoto atahisi labda kuna hatari ndio maana mama yake anapiga kelele. Ile kuhisi hatari kwa mtoto nako ni adrenal nayo inakua inaanza kufanya kazi so hapo inakua ni utashi wa nyoka mwenyewe atakachoamua.
View attachment 2446767
Hivyo Yule nyoka japo mimi nilikua nina nia njema ya kumsaidia lakini nilimfuata mwili wangu ukiwa katika hali ya fight or flight kwani najua Yule ni mbaya kwangu hivyo nyoka hakuangalia dhamira yangu bali alifuata sense yake ya Jacobson gland.
….
Hii ni theory yang tu kutokana na uelewa wangu wasayansi inawezekana sipo sahihi hivyo basi ruhusa kwenu kunikosoa na kusahihisha pale nilipokosea

-Criston Cole
Criston Cole ahsante sana umenifungua ubongo wangu kisayansi.Mimi nimesoma biology kama wewe ila kwenye endocrinology sio mjuzi sana

Sasa nimepata picha kuwa ni kwanini ukikutana na simba uso kwa uso ukamuangalia sana wala hutetereki anaona aibu kukudhuru hata anaweza kukutisha lakini ukiwa attentive unamuangalia tu na usimpe kisogo unarudi kinyume nyume nayeye machale yanamcheza anajua hapa maji marefu hakufanyi kitu na anaweza kutimka zake.

Pia nimepata picha ni kwanini nyoka haumi mtoto mdogo.Watu wanapelekea kukimbilia ni malaika kumbe ndani yake ni sayansi tupu hapo.Mfano mwingine kwenye ajali mtoto mdogo anaweza pona watu wote wakafa watu wanasema ni malaika kumbe hawajui uzito wa mtoto ulivyo mdogo ukizidisha na mwendo wa gari momentum yake inakuwa ni ndogo hivyo impact inakuwa ndogo kwake wengine mnakufa afterall watu wenye mauzito makubwa ndio wa kwanza kutangulia mbele ya haki kwenye ajali hapa nimeenda pembeni kidogo ya mada yako lakini najaribu kuelezea sayansi inavyoelezea wakati kwenye dini ni shortcut tu malaika

Pia nimepata picha ni kwanini ukienda nyumba ya mtu kama kuna mbwa akibweka wewe huna habari anaweza akakuacha lakini ukimpa kisogo tu anajua umeogopa anakukimbiza kumbe anakuwa amenusa ile hormone anajua huyu ni kibaka tu

Umeandika sana kujaribu kuunganisha dini na sayansi lakini nimeshagundua hilo la kusema nitaweka uadui kati yenu kumbe liko kisayansi kuliko tunavyofikiria sisi

Umenipanua akili mno hata hivyo natafuta namna naku inbox tuzidi kuwasiliana
Usikate tamaa humu wako watao kukejeli ulicho andika ila tuliosoma sayansi tumekupata
 
Huyu

Huyu wa mchongo😁
Mkuu sio wa mchongo hata kidogo, kuna nyoka aliuawa wiki 2 zilizopita dodoma nikishuhudia kwa macho yangu nami ilibidi nishirikiane kumuua alikua ni mrefu kama futi 5.6 hala mnene kama mkono wangu alikua Cobra. Aisee alivyokua akipanua shingo na kurusha mate utadhani kabisa wale wa kwenye tv. Ila aliuawa.
pote mjini vijiji ndio usiseme wanazidi hadi ya watu na baiskeli ukiwachanganya, tabora ni kwaida kuamka asubuhi ukakutana na nyoka mlangoni anakusabahi 😁😁😁
Maneo ya kanda ya kati hasa Tabora na singida kuna nyoka wengi sana sana. Singida wamejaa Cobra watupu kama wale wa kihindi na Tabora ni Koboko tu. Nyoka wa tabora wanakula hadi vitumbua, wanakula tui la nazi, wanakula ubwabwa nk nk😅
 
Hapa ndipo huwa siwaelewi freemasons, sometime huwa nafikiria hata ustaarabu si hulka ya mwanadamu aliyekamilika huenda ni namna tu freemasons wanataka wawe na namna ya kututhibiti kupitia ustaarabu tuliopandikizwa kama namna sahihi ya kutreat mambo
Kwa mujibu wa kitabu cha Enoch karibia kila kitu duniani kimeanzishwa na Viumbe walioasi Mungu. Yaani pesa,madini,uongozi,uganga,elimu nk sasa hua najiuliza kwani Mpango wa Mungu alitaka tuishi kama wanyama au ni gani
 
Back
Top Bottom