[emoji16][emoji16][emoji16] sio kwamba point yako nawewe inatakiwa uiweke hivi, Nyoka wengi wanaoishi katika mazingira ya majumbani au wanaoishi karibu na binadamu hawana sumu ya kuweza kudhuru wanyama wakubwa kama binadamu nk
Nyoka wenye sumu waga wana tabia ya kuhama kadri watu wanavyosogea, nyoka wenye sumu waga hawataki kabisa mazoea na binadamu maana huofia sana usalama wao
ila nyoka wasio na sumu nawao huogopa sana kuambatana na nyoka wenye sumu maana hugeuzwa kuwa vitoweo, hivo huona ni bora wabakie katika mazingira ya watu ili waambulie Panya na wadudu wengine wengine ndomana sehemu zenye Panya wengi kukuta nyoka ndani ya nyumba kawaida sana
nyoka wenye sumu Kali na wabishi kuhama ni kama vile koboko, huyu hataki kuhama katika mazingira ya watu Kwa sababu hupenda sana Bangi na tumbaku kwahiyo akienda huko ndichi ni ngumu kupata vitu vyake vya kupatia stimu
Na nyoka mwingine ambae ni ngumu kuhama mazingira yenye watu ni Kifutu, huyu kwakuwa ni mvivu na mpole waga anahisi kama vile yeye sio hatari kwa binadamu ndomana hubaki na kuishi kwa kuamini kutokana na tabia zake basi atakuwa msela Kwa binadamu
ila ukweli ni kwamba huyu ndio nyoka ambae ni muhanga wa kwanza kwa binadamu maana ni rahisi sana kumuuwa pamoja na sumu yake kuwa hatari, unaweza kumkanyaga alafu yeye akawa anahangaika kujitoa badala ya kushambulia ila akiuma ndo utajua hujui