Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Sasa kuliko ku take risk ya kumsindikiza mshikaji airport usiku why huyo jamaa yenu asingeenda mapema huko Airport, say Saa kumi na moja akatafuta Lodge jirani na airport? Mimi Kuna kipindi pale JKNIA nilikuwa na safari ndege inaondoka saa 10 alfajiri, kuliko kusumbua watu saa moja usiku nikaenda zangu kupata Lodge jirani na airport kabisa..
 
Ushasema USA. Kule ni mbali ndio maana wengi hatufikirii kwenda kuishi kule.
Hapa Kaburu ni karibu mno na nyumban, na kila mara nikitaka kuja bongo kufanya mambo yangu, naruka mara 1 baada ya wiki 1 au 2 narudia Kaburu kuendelea na maisha.
Sasa si ni bora uwe mbali ambako ni safe kuliko hapo kwa majambazi?
 
Pale nyumbani Tanzania Kuna amani na upendo mwingi sanaa
Pale nyumbani!!!

Mbona inaonekana hata na wewe haupo huko mkuu.

Hata hivyo ushaur wako ni mzuri, japo kwa mtu ambae ashajipanga na kuwa na familia hapa, ni vigumu sana kuchukua uamuzi huu kwa haraka haraka.
 
Mkuu sometimes kama una usafiri na haujawahi kukumbana na jambo la aina hii basi ni vigumu sana mtu kufanya kama ulivyoandika.
 
Sasa si ni bora uwe mbali ambako ni safe kuliko hapo kwa majambazi?
Hata huko mbona watu wanauwana tena kwa bunduki mkuu, au wewe huwa haufatilii taarifa za mauaji ya USA.

Sehemu salama kuishi ni Nordic countries kama Norway, Sweden na Denmark japo kifo kikikuhitaji kutakufuata mpaka huko kukumaliza.
 
Kifupi kwa hapa ni mara 10 uishi Pretoria, kwani ndio mji mkuu, lkn matukio ya kijinga jinga hivi ni vigumu kutokea.

Japo kuna uhalifu mdogo wa hapa na pale ila sio kama miji mikubwa ya joz, cape na durban. Alaf poda inauzwa sana huko.
Vipi kama mtu anataka akatembee tu, labda kwa wiki moja au mbili hivi?

Nimeyakenga hayo majiji mawili: Durban na Johannesburg.
 
Kumbe kutokujulikana sana ni ulinzi pia!
 
Miliki mguu wa kuku ndugu , ulimwengu umebadilika sana , miliki bastola ii uwe na Chance ya kukabiliana na mabedui kama hao wakijipendekeza
 
Vipi kama mtu anataka akatembee tu, labda kwa wiki moja au mbili hivi?

Nimeyakenga hayo majiji mawili: Durban na Johannesburg.
Kutembea na hata kuishi pia haina shida. Miji yote hiyo ni mikubwa. Na kwa hapa mji wa kwanza kwa mzunguko wa fedha ni jozi, wa pili ni cape town, alafu durban inashika bafas ya 3.

Kikubwa ujue tu kwamba katika dunia au nchi kama hii kuna matukio yanatokea kwa kupangwa, na mengine kama ajali (bahati mbaya).

Haya yakupangwa mtu unaweza kuyaepuka ikiwa utawahi kuyabaini na kuchukua hatua ya kuyaepuka kama ninavyoamua kufanya mimi.

Lakini haya yanayotokea kama ajali yanaweza kukuta popote hata hapo bongo. Mfano unaweza kwenda posta kutembea, likatokea tukio la ujambazi ghafla.. katika urushianaji wa risasi kati ya askari au walinzi wa bank na majambazi ukashangaa risasi imekupitua ghafla na kukujeruhi, au kupoteza kbs uhai wako.
 
Kumbe kutokujulikana sana ni ulinzi pia!
Yah.. watu wakikujua ni rahisi sana kukuchorea ramani. Mfano mtu anajua huyu jamaa anafanya biashara ambayo kwa siku anaingiza kiasi kikubwa cha fedha. Hivyo kama anahitaji hizo fedha na anakufahamu vizuri, basi itakuwa rahisi yeye kukuchorea ramani ya kukuibia.

1. Kwanza huenda anakuwa ashajua wewe haumiliki silaha au unayo lkn huwa unakuwa nayo muda gani.

2. Anakuwa ashajua kwamba wewe ukitoka katika biashara zako, au nyumbani kwako hupitia njia gani na wapi akienda kutinga au akituma watu wakutinge utapatikana kiurahisi.

3. Pia anajua au wanajua kwamba wewe ukitoka huwa peke yako, au unaongozana na nani kwenda kazini au kurudi nyumbani.

Kifupi ukijulikana sana nchi kama hizi huwa ni shida, kwa sababu ni rahisi sana watu kuchora mfumo mzima wa maisha yako, na hivyo kuyaweka hatarini maisha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…