Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Mpaka sasa sijajua kama walikuwa na lengo la kuiba gari, kuniua mimi au kumuua rafiki yangu.

Hata hivyo tumeshafikisha taarifa kwenye vyombo husika. Hivyo tunafuatilia na kumuomba Mungu atuepushe na umauti wa aina hii.

Shukran sana kwa mchango wako mkuu.
Sasa kuliko ku take risk ya kumsindikiza mshikaji airport usiku why huyo jamaa yenu asingeenda mapema huko Airport, say Saa kumi na moja akatafuta Lodge jirani na airport? Mimi Kuna kipindi pale JKNIA nilikuwa na safari ndege inaondoka saa 10 alfajiri, kuliko kusumbua watu saa moja usiku nikaenda zangu kupata Lodge jirani na airport kabisa..
 
Ushasema USA. Kule ni mbali ndio maana wengi hatufikirii kwenda kuishi kule.
Hapa Kaburu ni karibu mno na nyumban, na kila mara nikitaka kuja bongo kufanya mambo yangu, naruka mara 1 baada ya wiki 1 au 2 narudia Kaburu kuendelea na maisha.
Sasa si ni bora uwe mbali ambako ni safe kuliko hapo kwa majambazi?
 
Pale nyumbani Tanzania Kuna amani na upendo mwingi sanaa
Pale nyumbani!!!

Mbona inaonekana hata na wewe haupo huko mkuu.

Hata hivyo ushaur wako ni mzuri, japo kwa mtu ambae ashajipanga na kuwa na familia hapa, ni vigumu sana kuchukua uamuzi huu kwa haraka haraka.
 
Sasa kuliko ku take risk ya kumsindikiza mshikaji airport usiku why huyo jamaa yenu asingeenda mapema huko Airport, say Saa kumi na moja akatafuta Lodge jirani na airport? Mimi Kuna kipindi pale JKNIA nilikuwa na safari ndege inaondoka saa 10 alfajiri, kuliko kusumbua watu saa moja usiku nikaenda zangu kupata Lodge jirani na airport kabisa..
Mkuu sometimes kama una usafiri na haujawahi kukumbana na jambo la aina hii basi ni vigumu sana mtu kufanya kama ulivyoandika.
 
Sasa si ni bora uwe mbali ambako ni safe kuliko hapo kwa majambazi?
Hata huko mbona watu wanauwana tena kwa bunduki mkuu, au wewe huwa haufatilii taarifa za mauaji ya USA.

Sehemu salama kuishi ni Nordic countries kama Norway, Sweden na Denmark japo kifo kikikuhitaji kutakufuata mpaka huko kukumaliza.
 
Kifupi kwa hapa ni mara 10 uishi Pretoria, kwani ndio mji mkuu, lkn matukio ya kijinga jinga hivi ni vigumu kutokea.

Japo kuna uhalifu mdogo wa hapa na pale ila sio kama miji mikubwa ya joz, cape na durban. Alaf poda inauzwa sana huko.
Vipi kama mtu anataka akatembee tu, labda kwa wiki moja au mbili hivi?

Nimeyakenga hayo majiji mawili: Durban na Johannesburg.
 
Kuhusu rangi nyingine mfano wazungu ni vigumu sana wao kuuwawa kwa sababu wengi wao wanatembea na silaha za kujilinda, lkn pia hawana ushirikiano sana na watu weusi hivyo inakuwa ngumu mtu kuwaingia kichwa kichwa cause hawezi kujua yeye au mwenzake wa pemben amebeba nini ndani ya gari au suruali yake.
Kumbe kutokujulikana sana ni ulinzi pia!
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Kwanza napenda kumshukuru mw/Mungu kwa kuendelea kunipa nafasi nyingine ya kuishi hapa duniani. Naelewa kila mtu atakufa kwa kifo cha namna yake hapa duniani, lkn katika maisha yangu nimekuwa nikimuomba Mungu siku akinihitaji kurudi kwake, basi kifo changu kiwe cha amani mfano kiwe cha usingizini, cha nyumbani nikiwa nimekaa nk.

Vifo vya kufa kwa kuuwawa mara nyingi huwa sio vizuri. Ni vya mateso na maumivu makali, japo dini hutuambia kwamba wale wanaouwa wenzao kwa namna yoyote, na wao adhabu yao huwa kubwa kwa Mungu, na pia hapa duniani kwa sheria za nchi husika. Hivyo inapotokea mtu umenusurika kifo cha kuuwawa na mtu/ watu, basi ni bora kutumia muda mwingi kumshukuru Mungu na yule/ wale waliokuwa sababu ya kukuokoa.

Let's go to the mada husika hapo chini [emoji116]

Wakuu mimi ni mbongo nilieamua kuhamishia maisha yangu Kaburu longtime ago, japo mara nyingi huwa nakuja bongo kwa mambo yangu binafsi na kuondoka.

Usiku wa kuamkia leo, kuna ndugu yangu alikuwa anasafiri na ndege ya usiku, kutoka hapa Afrika kusini kuelekea Tz (nyumbani). Huyu ndugu yangu ni mwenyeji wa Cape Town, hivyo alivyofika hapa mimi ndio nilikuwa mwenyeji wake.

Alikuwa anaondoka na ndege ya saa tisa alfajiri, hivyo ikabidi mimi na rafiki yangu tumpeleke uwanja wa ndege wa Oliver Tambo saa sita usiku, ili awahi kufanya process zake zingine za usafiri nk, na pia na sisi angalau tuwahi kurudi kupumzika kwa ajili ya kesho (leo asubuhi) kazini. Basi baada ya kufika kule na kupiga story mbili tatu za kuagana, na baadae kufanya process zake za usafiri, sisi mida ya saa saba na nusu tukaanza safari ya kurudi nyumbani.

Wakati nakanyaga mafuta katika highway ya kutoka Kempton park kuelekea Johannesburg town, nikaona kama kuna gari fulan ndogo inatufuata kwa nyuma. Mwanzo tulijua ni gari tu ya kawaida au maybe askari wanataka watusimamishe wakague gari yetu (huo ni utaratibu wao), lkn kila nilipokuwa naongeza mwendo na wao pia waliongeza kimya kimya.

Nilivyofika sehemu fulani kuna mjengo mkubwa umeandikwa "Builders Warehouse" Edenvale, nikaingia kushoto kuelekea Edenvale road ila mimi nikakunja kushoto kuelekea upande wa Germiston road, kuangalia nyuma naona na wao wanaelekea upande ule ule ninaoelekea mimi. Sasa nikawa nishajua kwamba jamaa wanatufuata ni sisi na tukifanya masihara tutagawa maisha yetu kwa shetani (nasema ivi kwa sababu mtu anaetaka kukufanyia uovu anakuwa connected moja kwa moja na shetani) hivyo nikabidi nizidishe speed bila kujali mshale unasoma ngapi kibaoni.

Nilivyokunja pale Edenvale road kuelekea Germiston road nikavuka robot ya kwanza (mataa), nikavuka ya pili kuna daraja la highway ya gari zinazotoka Pretoria, alaf mbele nikakunja kulia jamaa wako na sisi tu japo tayari tulikuwa tushawaacha distance kadhaa. Nikakamua kweli kweli mpaka tukakutana na highway wa Albertina Sisulu, jamaa hawakati tamaa wako na sisi tu.

Tukatambaa na highway mpaka mitaa ya karibu na Eastgate Mall. Pale tukakuta kuna gari ya askari imepaki pembeni wanafanya ukaguzi wa kawaida, tukasema hapa hapa ndo tutapopatia usalama wetu. Japo hawakutaka kutusimisha, lkn ikabidi sisi wenyewe tusimame, ili tuwape maelezo ya ile gari inayotufatilia.

Wakati nimepaki pemben nashuka kwenda kuwapa maelezo wale askari tukaona ile gari nayo inakuja wangu wangu.., ila walipoona kuna askari, na sisi tumepaki tukiongea na askari, jamaa wakapandisha kwa njia ya juu kushoto inayoelekea Eastgate kwenyewe na kutokomea kusikojulikana.

Sasa kwa vile ni usiku na tulikuwa kwenye kukimbizwa na watu hatari, hatukuweza kui mark gari yenyewe wala namba za gari, hivyo ikawa ngumu kwa sisi na askari kuwakamata, kwani tulijaribu kuwafuatilia kwa nyuma na gari yetu tukiongozana na ile ya askari, lkn hola hatukuwapata, na ukizingatia J'burg ni mji mkubwa na una barabara nyingi mno. Basi tukarudi home na kulala hadi asubuhi.


Hii imenikumbusha, week 2 zilizopita, kuna mkongo mmoja alifuatiliwa hivyo hivyo kutoka Yeoville hadi kwake Bez alley. Inasemekana kuwa mkongo baada ya kufika kwake alifungua mlango fasta, na kuingia kwake. Ila bahati mbaya (au naweza kusema siku zake zilikuwa zimefika) hakuwa amebana vizuri gate la kuingilia kwake, na jamaa wakawa wameshafika na kuona nyumba aliyoingia. Jamaa wakapush mlango, wakaingia ndani na kukuta watu wakiwa hawana hili wala lile, jamaa wakiwa na "double 9" mkononi wakauliza yule mtu aliekimbilia humu yuko wapi? Mpopo (nigeria guy) mmoja akajibu hatujamuona, kabla hajamaliza kauli akapigwa ya Paja, na kuelekezewa nyingine kichwani, akaambiwa tunauliza kwa mara ya mwisho, bila jibu sahihi tunafumua ubongo na kukamata mungine mpaka tutawamaliza. Walivyouliza kwa mara ya pili, wote wakajibu pamoja kwamba amejificha chooni.

Ndo wakamwambia mpopo akawaoneshe chooni, kweli Ile kuingia wakakuta jamaa kajificha anatetemeka. Wakamtoa nje mbele ya familia yake, wakamuomba funguo za gari na simu, akawa funguo akasema hana simu. Basi jamaa wakafumua kichwa kwa risasi 4 mbele ya ndugu zake, alafu funguo ya gari wakaachana nayo wakatoka nje na kutokomea kusikojulikana.

So na sisi tulivyokuwa tunafuatwa, basi nilihisi na mimi yanakwenda kunikuta yale ya mkongo. Kwamba huenda jamaa wamepewa dili tu kama ilivyotokea kwa yule mkongo au labda walikuwa ni majambazo wa magari nk.

Huu ndio unakuaga mwezi mgumu, na hatari kuliko miezi yote hapa Kaburu. Wengi huwa tunaweka mbele maombi na dua mbali mbali ili kuuvuka salama mwezi huu.
Miliki mguu wa kuku ndugu , ulimwengu umebadilika sana , miliki bastola ii uwe na Chance ya kukabiliana na mabedui kama hao wakijipendekeza
 
Vipi kama mtu anataka akatembee tu, labda kwa wiki moja au mbili hivi?

Nimeyakenga hayo majiji mawili: Durban na Johannesburg.
Kutembea na hata kuishi pia haina shida. Miji yote hiyo ni mikubwa. Na kwa hapa mji wa kwanza kwa mzunguko wa fedha ni jozi, wa pili ni cape town, alafu durban inashika bafas ya 3.

Kikubwa ujue tu kwamba katika dunia au nchi kama hii kuna matukio yanatokea kwa kupangwa, na mengine kama ajali (bahati mbaya).

Haya yakupangwa mtu unaweza kuyaepuka ikiwa utawahi kuyabaini na kuchukua hatua ya kuyaepuka kama ninavyoamua kufanya mimi.

Lakini haya yanayotokea kama ajali yanaweza kukuta popote hata hapo bongo. Mfano unaweza kwenda posta kutembea, likatokea tukio la ujambazi ghafla.. katika urushianaji wa risasi kati ya askari au walinzi wa bank na majambazi ukashangaa risasi imekupitua ghafla na kukujeruhi, au kupoteza kbs uhai wako.
 
Kumbe kutokujulikana sana ni ulinzi pia!
Yah.. watu wakikujua ni rahisi sana kukuchorea ramani. Mfano mtu anajua huyu jamaa anafanya biashara ambayo kwa siku anaingiza kiasi kikubwa cha fedha. Hivyo kama anahitaji hizo fedha na anakufahamu vizuri, basi itakuwa rahisi yeye kukuchorea ramani ya kukuibia.

1. Kwanza huenda anakuwa ashajua wewe haumiliki silaha au unayo lkn huwa unakuwa nayo muda gani.

2. Anakuwa ashajua kwamba wewe ukitoka katika biashara zako, au nyumbani kwako hupitia njia gani na wapi akienda kutinga au akituma watu wakutinge utapatikana kiurahisi.

3. Pia anajua au wanajua kwamba wewe ukitoka huwa peke yako, au unaongozana na nani kwenda kazini au kurudi nyumbani.

Kifupi ukijulikana sana nchi kama hizi huwa ni shida, kwa sababu ni rahisi sana watu kuchora mfumo mzima wa maisha yako, na hivyo kuyaweka hatarini maisha yako.
 
Back
Top Bottom