Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Mkeo msouth?nimewahi sikia wanawake wa South Africa...mwanamume mgeni akipata hela wanachonga mchongo anauwawa ili wabebe mali
Hapana mkuu, japo niliwahi kuzaa na msauzi, lkn mke wangu ninaeishi nae huku ni mbongo. Ila tayari tumeshazaa nae watoto wawili, mmoja anaingia darasa la tatu mwakani, na mdogo ataingia la kwanza.

Elimu ya hapa inafaida kubwa kwa nchi yoyote ya Afrika. Hivyo naona bora niendelee kupambana ili kuwapatia watoto wangu elimu bora kwa maisha yao ya baadae.

Pia huyo mtoto niliezaa na mzawa kwa sasa yupo kwenye mikono yangu namsomesha na ashafika la 5. Huyu pamoja na kwamba simtegemei sana kama nitaweza kurudi nae nyumban pale itapobidi kurudi, lkn naona ni damu yangu, siwezi kuacha kumpa haki yake ya msingi kwa ajili ya maisha yake ya baadae hata ntakapokuwa sipo hapa.

Sababu yeye hakupenda au kupanga kujileta mwenyewe dunia, bali ni starehe za sisi wawili (mimi na mama yake) ndio zilizosababisha ujio wake. Hivyo ni lazima nimpambanie kwa ajili ya dreams zake.

Nikiona presha inazidi nitahamia mji mungine, maana nchi hii ni kubwa na kila mji au kila sehemu kuna fursa zake.
 
Nakumbuka mwishoni mwa mwezi Septemba, 2017 tuliwasili hapo OR Tambo International Airport Saa 6 usiku, nilishangaa kuona Wanajeshi wengi pamoja na Askari Polisi wengi pia wakiwahutubia Abiria na Wageni wanaowasili kwamba wasitoke nje ya uwanja huo kwani kuna tukio kubwa la ujambazi limetokea usiku huo eneo la Four Ways Jhb ambako Watalii kutoka Ujerumani waliporwa kila kitu na Majambazi. Watalii hao walikodisha basi kubwa ili liwafikishe hotelini, majambazi waliovalia Yunifomu za Polisi walisimamisha basi hilo na Kisha kuwaweka watalii wote at gun-point na kuwapora kila kitu, mabegi na simu zao zote zilichukuliwa. Ni hatari sana kuwasili OR Tambo usiku na Kisha kuchukua usafiri wa gari bila escort ya ulinzi mkali wa silaha.
 
Wahalifu wanakufata kwa sababu fulani , miongoni mwa sababu hizo ni inawezekana una kitu cha thamani, au una ugomvi nao, au kuna deal haramu unafanya nao na mmepishana sehemu

Hao ambao wanakufata kwasababu una kitu cha thamani huwa hawawezi kukurudia kama hawana connection na mtu wako wa karibu, ila hao waliobaki kama una watu unafanya nao deals haramu na umepishana nao, au una kisasi na mtu hao hawawezi kukuacha watakutafuta sana

Kwahiyo ni muda wa kutulia na kujitafakari na kuwa standby muda wote
 
Aisee kipindi hiki huku huwa ni hatari sana.
 
Ulichoandika kina ukweli mkuu, ila binafsi nafanya shughuli zangu halali.

Japokuwa duniani kuwa watu hawapendi kuona wengine wakipiga hatua kuwazidi. Watu hao huwa tayari kufanya lolote aidha kukuroga, kukusingizia kesi mbaya ili upotezwe au kukuuwa kabisa.
 
Yani nlipata mchongo wa biashara na kampuni glani south Africa lakni Kila nikiifkria Ile nchi nashindwa kabisa ,
Nimeamua ntafute kampuni zengne Austria na ulaya huko Mana hii nchi so mchezo naiogopa balaaa.
Hta stamani kwenda hata buree
 
Yani nlipata mchongo wa biashara na kampuni flani south Africa lakni Kila nikiifkria Ile nchi nashindwa kabisa ,
Nimeamua ntafute kampuni zengne Austria na ulaya huko Mana hii nchi so mchezo naiogopa balaaa.
Hta stamani kwenda hta bure
 
Labda una gari kali sana🙂
Yani hapo ndo nashindwa kuelewa kama lengo lilikuwa ni gari au kitu gani.

Lakini kama ni gari kali mbona kuna wanaoendesha kali zaidi ya hili langu mkuu!

Anyway sio mimi au wewe anaeweza kujua lengo la wale jamaa isipokuwa mwenye kufahamu malengo yao ni Mungu pekee.
 
Kwa nchi ya Afrika ya Kusini hususani kwenye miji mikubwa zaidi kama vile Jhb, Cape Town au Durban, kufuatiliwa na Wahalifu au Majambazi ni kitu cha kawaida kabisa, wala siyo ajabu. Kitu cha msingi ni kuwa mwangalifu sana muda wote unapokuwa safarini barabarani.
 
Mkuu una uhakika hawajakariri plate no pamoja na rangi ya gari wakakuwinda mitwa hiyo uliyokuwa unakatiza wwkati wanakufatilia?

Pole sana chief, umakini uongezeke zaidi.
 
Mnadhulumiana kwenye biashara...
Mnachukuliana mademu..
Hampendani wahamiaji.

Huyo jamaa mliyemsindikiza huenda aliwaset. Trust nobody.
Japo hayo hutokea kwa baadhi ya watu, lkn mimi sio mmoja wao mkuu.

Na jamaa niliemshindikiza hawezi kufanya huo mchongo kwani yeye hapa ni mgeni kutoka cape town, na mimi ndio nilikuwa mwenyej wake, alaf ni ndugu wa damu kabisa.
 
Hakika wewe unaifahamu vizuri nchi hii, na ushauri wako uliotoa ni wa kuzingatiwa.

Tatizo wengi ambao hawajawahi kuishi nchi hii hawajui kama hayo mambo yapo kila siku, na hutokea kwa mtu yoyote haijalishi unafanya dili za hatari, unatembea na wake za watu au unaishi peace na watu.

Wakikuotea ndo hivyo tena inabidi utafute namna ya kuwaepuka au kukabiliana nao tu kama ilivyokuwa kwangu na kwa watu wengine walionusurika.
 
Daaa
 
Mkuu una uhakika hawajakariri plate no pamoja na rangi ya gari wakakuwinda mitwa hiyo uliyokuwa unakatiza wwkati wanakufatilia?

Pole sana chief, umakini uongezeke zaidi.
Hili ndio nina wasi wasi nalo. Kama sio majambazi basi ni watu waliotumwa au wanaonifahamu kati ya mimi au jamaa niliekua nae.

Na kama ni hivyo basi tayari watakuwa washaifahamu au wanaifahamu gari yangu. Hivyo nimeamua niipaki uani huku nikiangalia utaratibu wa kumtafuta mtu tusiefahamiana nae nimuuzie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…