Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Yaani umemzalisha mwanamke mzawa na kumtelekeza? wewe hawakuachi.
 
Sawa brother ila hakuna ruhusa ya Polisi wa SA kukimbiza gari na raia wanachokifanya ni kutoa taarifa kwenye radio call na wanawatafuta kwa mawasialiano kama wana hatari sana wanaweza kutafutwa kwa Chopa upo sawa na pia sijui ulipita wapi ila kutoka Airport Robot ya kwanza ni hiyo hapo East Gate Mall kama ulitoka na R 24 na ukaunga baadae na Albertina Sesulu Road na hapo chini kushoto mara nyingi wazee ndio huwa wanapenda kukaa hapo East Gate na wengine walikua wale Polisi wezi wanawazuia watu hapo wanaotoka Airport kwa kujifanya Polisi na kuwaibia Mali zao...ili uwe salama mara nyingi unatakiwa uingie kama unaingia kwenye hiyo Mall then unakata kulia unaendelea na safari ili kuwakwepa hao wezi wa kwenye mataa wa usiku..
 
Pole sana! Na hongera kuwa makini. Mara nyingi watu wanaotoka Airport au Shopping malls wanakuwa wanawindwa sana na vibaka.Mungu akulinde Ndugu. Kitambo sana hapo Hillbrow Flamingo Hotel, wape high majita wote hapo the pertz na mitaa mingine
Asante sana mkuu kwa maombi na dua yako kwangu. Kuhusu salam kwa masela nitawafikishia tu mkuu wangu.

Mungu akubariki ndugu yangu
 
Pole mzee, SAUZI ni nchi ya hatari sana kuishi.
Ongeza umakini kuanzia unapoamka mpaka unaingia kulala.
Ikiwezekana fuatilia tu upate kibali uwe na cha moto.
Nimeona umesema kupata kibali ni changamoto, pambana upate mzee.
 
Wanasema south africa uzunguni pamekuwa pagumu mno kuingilika na vibaka kwai io siku iz vibaka shughuli za ukabaji wamezihamishia kwa weusi wenzao
 
Tatizo watu wa nje( hasa wanigeria na watanzania) wanafanya biashara haramu ya unga, wizi, utapeli, ndio kinachowakera wazawa wa huko
South Africa kuna mchanganyiko mkubwa sana wa wahamiaji kutoka karibu nchi zote za hapa.duniani. Ndio nchi pekee ktk bara la Afrika yenye wahamiaji wengi zaidi, na hii imekuwa sababu mojawapo ya kuongezeka kwa matukio ya uhalifu kwenye nchi hiyo due to the "scramble of scarce resources."
 
Yah ni kweli ulichoongea kuhusu robot ya kwanza hapo Eastgate, lkn hao polisi hawakuwa maeneo ya robotini bali walikuwa wametinga nyuma kabisa karibu na ile barabara inayopandisha kushoto kuelekea Eastgate Mall kama unatokea Albertina Susulu.

Kuhusu askari kukimbiza gari na raia hilo pia linafanyika. Kuna siku moja week end asubuhi nilienda kunyoa sehemu (salon). Sasa wakati nikiendelea kunyolewa, mimi pamoja na wateja wengine tukaanza kusikia risasi zinalia nje, ikabidi wote tutoke nje kuangalia nini kinaendelea. Wakati tunatoka kuangalia, tukaona jamaa mmoja anatoka ndani ya gari yake (ilikuwa hiace quantum) akiwa na bomba mkononi akijaribu kurusha na yeye risasi kuelekea upande wa mbali kidogo ambapo kulikuwa na gari nyingine tena aina ya X5 ikiwa na jamaa wawili waliokuwa wakimshambulia jamaa kwa risasi pia bila mafanikio wala kumjeruhi (nahisi zilikuwa beef zao) hivyo sisi wote tulivyoona jamaa anaelekea upande wetu tukawahi kufunga mlango wa salon na kukimbilia uwani, lengo ni kutaka jamaa asiingie mle salon maana pengine jamaa wangemfata na kusababisha vifo na kwetu pia.

Sasa yule jamaa akapitiliza hadi Spar, maana salon ilikuwa karibu na Spar ambapo kuwalikuwa na askari wamekuja kununua vitu Spar, alaf muda wote huo walikuwa hawajui hili wala lile. Jamaa akakimbilia ndani ya Spar na kuwataarifu askari, wale jamaa walipoona yule mtu kaingia za Spar wakageuza kurudi kwenye gari yao. Jamaa nae akawataarifu askari kuwa kuna watu wanamkimbiza. Hivyo wazee walichofanya wakampakia jamaa kwenye gari lao na kutoka nae kwa kasi sana lengo la kuwawahi na kuwa tight jamaa eneo la tukio. Kwa bahati mbaya walipotoka wakakuta ile gari ya wale majamaa imeshaondoka tayari. Hivyo ikabidi waende na jamaa kituoni wakaandike maelezo ya kilichotokea.

Hiki kilikuwa ni kile kipindi cha mabeef ya madereva texi (mabasi) wenyewe kwa wenyewe.

Hivyo muda mungine raia anaweza kusaidia kuwapata wale wanaomtafuta wamuue kama anawafahamu vizuri wauaji.
 
Pole mzee, SAUZI ni nchi ya hatari sana kuishi.
Ongeza umakini kuanzia unapoamka mpaka unaingia kulala.
Ikiwezekana fuatilia tu upate kibali uwe na cha moto.
Nimeona umesema kupata kibali ni changamoto, pambana upate mzee.
Asante sana mkuu. Itabidi nipambane kwa namna yoyote ili nipate kitu cha kunilinda.
 
Pole mzee, SAUZI ni nchi ya hatari sana kuishi.
Ongeza umakini kuanzia unapoamka mpaka unaingia kulala.
Ikiwezekana fuatilia tu upate kibali uwe na cha moto.
Nimeona umesema kupata kibali ni changamoto, pambana upate mzee.
Asante sana mkuu. Itabidi nipambane kwa namna yoyote ili nipate kitu cha kunilinda.
 
Huu ni ukweli ambao haupingiki mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…