Jinsi Rais Samia anavyotoa mamilioni ya sadaka kwa Makanisa

Acha uongo 500 milioni Jimbo la Arusha ilikuwa dhulma zilizofanywa na watendaji wasio waadilifu ya kupora eneo la kanisa na tukaambiwa tulipe Kwa kulinunua tena
 
Rushwa tu hiyo,zaidi ya bilioni moja hapo,kodi zetu zinapanywa sana.
 
Mama mjane alibarikiwa kwa kuwa alitoa sehemu ya chote ya alichonacho lakini hawa watoza ushuru walitoa tu ziada.
 
Afadhali zingetumika kujenga barabara ya kipande cha Dar Hadi Chalinze kwa njia mbili walau kama njia 3 alizoanzisha JPM inashindikana.
Barabara hiyo itanufaisha Watu bila kujali dini zao na hata wasio na dini maana binadamu wote wote ni Sawa mbele ya sheria.

Kuliko kupeleka zikapigwe na kamati za ujenzi na Viongozi wa dini kuwa machawa wa kusifu na kuabudu .
 
Barabara kipande cha DSM hadi Chalinze Kwanini hakijengwi kwa njia 3 ?
Huyu Waziri wa ujenzi Mbona kama mzito fulani hivi au ?
Hata kule bungeni sijuwahi kumsikia akiwasilisha hoja kwa kuonesha kuwiwa ?!

Magari kila siku yanakwama masaa 5 na kuendelea mfululizo .
Barabara inayounganisha mikoa na nchi za jirani wapakani zote,
Tangu Uhuru iko single ? 🙆‍♂️🤦‍♀️😭
 
Bakwata wao wanapewa mgao wao kupitia CCM kama Jumuia ndani ya CCM, ila Sheikh wa Mkoa wa Arusha ya kwake imepitia kwa RC Makonda
 

Tuwekee jumla pale chini
 
Mama anapanda mbegu, anasubiri mavuno tu basi!

Hawa walio pewa hizi pesa, kweli watapiga kampeni, au ananunua kimya chao; wasiseme chochote juu yake?

Hii pesa ni uwekezaji, ili izae mara dufu na zaidi.
Hawa viongozi wa dini wote kwa hakika wanazo akili za kutosha kuwaelewesha maana ya michango hii waliyo pewa.
Sasa kama kweli mungu wao wanaye mtumikia wao haya ndiyo yanayo mpendeza, sina shaka yoyote na walakini wa mungu huyo.

'Curiously', mkuu 'Quinine', hao wengine kwenye dini nyingine wao wamepewa ngapi? Hatuwezi kusema hapa kwamba matoleo haya yana lengo (ajenda) maalum?

Kiongozi wa nchi, kweli anadiriki kufanya haya bila ya kuhojiwa chochote juu ya hatma ya taifa analo liongoza?
 

ni rushwa kama zilivyo rushwa nyengine
 
Hivi hizi hela anatoa wapi?
EEEeeeenHEEEee!
Hivi kweli bado unauliza swali la namna hii hapa?
Huoni tuna nunuliwa kama bidhaa, tena enzi hizi, jameni!

Acha atuuze; lakini kati yetu watumwa hapatakosekana watakao kataa; kama ilivyo kataliwa enzi zile za giza.

Mi nilidhani Magufuli ni shetani katika kiwili wili cha binaadam, lakini huyu mwanamke,; hata sijui nimwelezee vipi?
 
Tuwekee na Misikitini mkuu maana huko hazitangazwi ni kimya kimya. Anza na ile Range Rover ya Mufti wa Jamhuri ya Arusha
 

Bila kuwasahau Kuna sheikh was Arusha, gari 100m/-.

Yawezekana Kuna biashara nzuri ya wapiga kura makanisani na misikitini huko.

Lucas Mwashambwa, Tlaatlaah au nasema uongo ndugu zangu?
 
kiasi chote bila kujumlisha "X" ni Shilingi 1,485,000,000.
Sasa baada ya hapo, ongeza na zile za pikipiki 4 kila kata (Tanganyika)!

Na bado sana. Watu bado hawajanunuliwa. Subiri wakati wa Kampeni na kupiga kura.

Mkuu 'lzy', usisahau kuwa na kinoti buku chako karibu; kwani safari hii tutashuhudia ambacho hatujawahi kukishuhudia, na pengine haitatokea tena katika historia ya nchi hii.
 
Mkuu, walisema Lowassa alikuwa na uchu wa madaraka lakini huyu mama ni namba nyingine. Naona ni fedha za waarabu hizi. Wanaogopa asije kutolewa 2025 wakati wanataka kuendelea kuchuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…