BAK brother hii ishu tunakosea sana tunapoamua kuwasukumizia mzigo wa lawama waumini wa dini ya kiislamu wote kwa ujumla, kwa sababu hayo maamuzi ya kupiga marufuku kuuzwa kwa chakula nyakati za asubuhi hadi jioni ya saa 10 naamini ni maamuzi yanayotolewa na serikali tu bila ya kuwashirikisha waislamu japo kwa njia ya sampling.
ikiwa ofisi ya
mufti mkuu nayo inahusika kwenye kadhia hii basi na wao watakuwa kwenye makosa kwa sababu mtume rehma na amani ziwe juu yake nyakati za uhai wake kwa nyakati tofauti aliweza kuishi na waumini wa imani tofauti (wakristo,mayahudi, wasioamini uwepo wa mungu a.k.a makafiri) lakini haijawahi kutokezea akaingilia uhuru wa imani zao hususani wakati wa ramadhani.
kwa serikali (zanzibar) inayojitapa kila siku haifungamani na imani yoyote ya kidini kwenye kuendeshwa kwake binafsi naamini inafanya makosa makubwa sana kujivisha joho la mamlaka ya kidini (uislamu) kwa kutumia muamvuli wa kulinda tamaduni za kizanzibari zinazopaswa kufuatwa na wote, kufanya hivi ni kuleta upendeleo kwa imani fulani.
serikali ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa mjini magharibi ilipaswa kuendelea kuonyesha msimamo wa kuwa neutrals kwenye ishu zozote za kidini huku ikihakikisha inazuia uvunjaji wa sheria kwenye matukio muhimu ya kidini yanaendeshwa na imani tofauti.
mimi ninapofunga na
Khantwe asipofunga kula kwake hadharani hakuniathiri na chochote kwa sababu hata wakati wa funga muhimu ya ARAFA wapo wanaofunga na wasiofunga na hakuna tatizo linalotokezea.
lakini mkuu ukiangalia upande wa pili wa shilingi asilimia kubwa (95%) ya wanaoishi visiwa vya zanzibar ni waislamu, ni tofauti na mazingira ya huko Bara ambako kuna jamii kubwa yenye mchanganyiko wa kiimani tofauti, hivyo basi hata kama ingelitokezea serikali isingejivika muamvuli wa kidini wakati wa mwezi wa ramadhani basi hao raia wenyewe wangelijivika muamvuli huo wa uislamu wa ramadhani.
kwa mfano ukiangalia asilimia kubwa ya wafanya biashara za chakula visiwani zanzibar ni waislamu, vivyo hivyo asilimia kubwa ya wanunuaji wa chakula kwenye migahawa na madukani ni waislamu.
ikiwa wanunuaji wakubwa wapo kwenye mfungo je kuna mfanya biashara wa imani yoyote atakayekuwa tayari kula hasara ya biashara yake kwa mwezi mzima hususani kwa biashara za asubuhi (chai) na mchana(lunch)?
ndio maana kwa kuliona hilo wafanyabiashara wa chakula wakaamua kubadilisha mfumo wa biashara zao kwa kuepuka hasara yenye kuepukika, wafanya biashara wengi wa chakula kwa sasa wameelekeza biashara zao nyakati za jioni kwa sababu ndio muda ambao wanakutana na wateja wao wa kila siku wanaokutana nao kwenye miezi ya kula mchana hususani wale wasiokuwa na familia za kuwaandalia chakula kama muanzilishi wa hii thread au wale wanaocherewa kurudi majumbani mwao/kwao kwa sababu ya majukumu ya kikazi.
nitatoa mfano mwengine mdogo kwa yanayotokezea nyakati za sikukuu za iddi.
ukija zanzibar siku ya iddi mosi ni ngumu sana kuwakuta wafanya biashara wa chakula wakifanya biashara zao nyakati za asubuhi na hata mchana, na hii ni kwa sababu wanunuaji wakubwa wa chakula hujumuika na familia zao kwa ajili ya kupata chai asubuhi na chakula cha mchana kwa watakachobarikiwa (most inakuwa pilau na biriani).
utamuuzia nani chapati, maandazi, keki, sambusa na vyenginevyo sikukuu ya kwanza haliyakuwa mteja wako atavipata nyumbani kwake/ kwao?
utamuuzia nani pilau au biriani nyakati za mchana sikukuu ya kwanza haliyakuwa wanunuzi wakubwa wanakula majumbani kwao/ mwao?
hivyo basi unakuta tabaka la wanunuzi linabaki lile lile lisilokuwa na familia za uhakika zitakazowawezesha kupata vyakula muda wowote wanaojisikia (tabaka hili ni chache), na bahati mbaya sana visiwani zanzibari majorities ya raia wanaishi majumbani mwao/ kwao pamoja na familia zao ambazo huwawezesha kupata chakula muda wowote wanaojisikia.
nimpe pole sana mleta mada kwa kadhia iliomkuta, namshauri kama ana uwezo atafute msichana muelewa atakayemlipa kwa huduma ya kupikiwa chakula au aishi pamoja na familia yake inapofika mwezi wa ramadhani ili kuepuka usumbufu wa kukumbwa na njaa, kama yote hayo hayawezekani basi ajiandalie chakula chake mwenyewe anapoishi.
sijafurahishwa na haya matusi yanayoelekezwa kwa waislamu wote kwa tatizo ambalo halijasababishwa na waislamu wote, hapa ninapoishi kwa takribani miaka 20 tumezungukwa na nyumba tatu za wakristo ambao tumewakuta mtaani na wazazi wao wapo tokea mapinduzi, tunaheshimiana, kusaidiana, tunapena mialiko ya sherehe mfano harusi kwa kila hali na haijawahi kutokezea kudhihakiwa kwao kwa sababu ya kula au kupika mchana,na ikifika krismasi/ pasaka wanasherehekea kwa uhuru bila ya vitisho vyovyote kutoka kwa majirani.
mara nyingi mgogoro mkubwa zanzibar uliopo dhidi ya watu wanaotoka bara ni ishu za siasa hususani mjadala wa muungano pamoja na uingiaji kiholela wa watu kutoka bara wanaokuja kuafuta ajira na si utofauti wa dini.
Religion is never the problem; it’s the people who use it to gain power. – Julian Casablancas