Jinsi tunavyoishi wakristo hapa Zanzibar kipindi hiki cha mfungo

Nijuavyo tanzania haina dini ila watu wake wana dini. Na katiba imesema wazi kwamba watu wanaweza kuabudu au kua na dini ila wasivunje sheria za nchi.

sasa sijui zanzibari ina katiba yake na bara inakatiba yake? Maana kama tuna katiba 1 huko zanzibari uo mkanganyiko wa nini?

yaani kisa wewe unafunga ndio uwafungishe na wengine?

hii sio sawa kabisa tuko kwenye nchi huru kila mtu anatakiwa aishi bila kuvunja sheria za nchi yetu. Hizi dini zisiondoe utu wetu.

kama muslam unafunga basi usi muhukumu hasiyefunga wala kumtesa kwa afate kile unachotaka wewe. Vivo hivyo kwa wakristo. Kama tutafanya hivyo basi tutaishi kwa upendo na sio ubinafsi.
 
Sheria si moja kwenye nchi zilizoungana? Iweje wasio waislamu wasipewe haki wanazopata na kustahili Bara hasa wanaokuwa safarini Zenj mwezi wa Ramadhan?
ndio maajabu ya muungano wetu wa serikali mbili ulivyo, zipo sheria zinazotumika upande wa bara zikijivika koti la muungano zikikosa nguvu za kutekelezwa visiwani zanzibar.

kwenye ishu ya ramadhani kama nilivyosema hapo juu serikali ya zanzibar ambayo inajitapa haifungamani na dini yoyote nayo inafanya makosa kwa kuweka sheria zisizowafurahisha wananchi wa imani nyengine kwa kutumia mwamvuli wa kulinda tamaduni za kizanzibari.

mimi siamini kama asilimia ndogo ya wasiokuwa waislamu italeta athari kubwa sana kwa asilimia kubwa ya wafungaji wa mwezi wa ramadhani, mbona wakati wa funga za sunna ya sita wapo baadhi ya waislamu wanaofunga na wasiofunga na hakuna athari yoyote kubwa inayotokezea.
 
Katika sheria moja ya zanzibar huruhusiwi kula mchana mwezi wa ramadhan na migahawa yote ifungwe, fata sheria huwezi nenda tanganyika ukale mchana
 
wewe mtoa mada msukule kweli.. Sasa wewe ulitakaje?
 
Mie ninachopinga Mkuu ukiangalia kwenye kitovu cha uislamu kule Saudi Arabia upuuzi huu wa kufunga hotels mwezi wa Ramadhan haupo na nchi zote za Kiarabu UAE, Kuwait, Misri, Jordan, Qatar etc. Sasa iweje huko uislamu ulikoanzia hakuna huu upuuzi uliojaa dhambi wa kufunga mahoteli mchana wakati wanajua fika kwamba Zenj ina wageni wengi ambao si waislamu? Kwanini wakomolewe wakati wakiwa ugenini?

 
Umeandika porojo tu kuonesha ujinga wa hii dini yenu,

mzee kufunga ni zaidi ya kuacha kula mchana na kula usiku kama mnavyofanya.
 
Hivi ww umewahi kwenda nchi za kiarabu mwezi wa ramadhan, hivi ww umewahi kuona upuuzi wa vbanga vya migahawa vya ajabu ajabu huko nchi za kiarabu au unakulupuka tu
 
Ni kwann Nile kwa kujificha? Kwan mie mwizi? Kwan wewe kufunga kwako kunanihusu Nini mm? Mbna wakristo wakifunga hawazuii wengine?
Nyie Ni washamba/mbumbumbu hamna elimu ndio maana
Kwanini uvae na kuvua nguo kwa kujificha?
Acha chuki izo, zitakuunguza mwenyewe
 
mkuu hayo ndio maamuzi ya serikali ya zanzibar kwa kutumia mwamvuli wa kulinda tamaduni za kizanzibari ifikapo mwezi wa ramadhani, niliwahi kumsikia naibu waziri fulani akimjibu mwakilishi wa jimbo fulani akisema ya kwamba utamaduni huo upo zanzibar tokea mwaka 1964.

ukiangalia kwa kiasi kikubwa hoja hii iliwalenga zaidi wale vijana wa kiislamu wasiokuwa na utamaduni wa kufunga ramadhani haliyakuwa wana afya imara, ndio maana serikali inachukua maamuzi ya kuzifunga hoteli na migahawa ili kuwabana wasiofunga ramadhani wasipate chakula.

wanachosahau serikali ni kwamba zanzibar hawaishi waislamu peke yao na kadri siku zinavyosogea muingiliano wa imani visiwani zanzibar unazidi kuongezeka.
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…