Jinsi ya kuepuka kupigwa na mawinga Kariakoo

Jinsi ya kuepuka kupigwa na mawinga Kariakoo

yeye hii hoja lawama anampa mteja. hali ya kua mteja kafika town kafika mpaka dukani lakini anaingizwa mkenge kwa sababu hana experience
Ndo utapeli huo. Hata wale wa tuma kwa namba hii mtumaji ni experience hana.
 
Kama serikali yenyewe unanunua gari labda Milioni nne ukifika bandarini Kodi Milioni nne tenà hivyo jumla 8m unategemea nini?

Wizi unatokana na usiri WA bei ya Bidhaa
Kama vile nauli serikali inavyotoa bei elekezi vivyohivyo n Bidhaa zingine inatakiwa Kutoa.

Hao Mawinga Kwao NI fursa na lengo la mfanyabiashara NI ku-make profit kadiri iwezekanavyo
Umehalalisha wizi na utapeli kwa jina la usiri na fursa.
 
Kinacho waharibia Mawinga NI TAMAA iliyopitiliza.
Imagine Mtu anakupiga Kwa zaidi ya elfu 50-laki Moja.
Na inauma unapokuta umepigwa parefu alafu mbaya zaidi ukute amekuimbisha receipt aandike pungufu. Yaani winga dawa yao kabla ya kulipa unamwambia anza ku-print receipt huku unahesabu hela, utaona anatoa macho na kuanza ooh unajua etc maana tajiri huwa anaandika receipt kwa bei ile aliyowatajia ila kile cha juu hakiwi documented kwenye receipt, hapa huwa tunaanza upya tena na kumshusha zaidi ikiwezekana kuondoka kabisa, hapa ndo tajiri wa kweli anajitokeza na kijifanya mpe tu kwa bei hiyo na kuwa siku mbaya kwa winga angalau atapozwa buku 5 ya kuleta mteja (maana ukizubaa umenunua mzigo wa laki 5 unakuta receipt imeandikwa laki 3 na nusu)
 
Wewe Mtu anauziwa Sabufa 150k Wakati bei Yake Mtaa WA pili NI 90k huoni Hapo kuna ulazima wa tahadhari
Mbona mpira wa simba na yanga ukichezwa Benjamini Mkapa unalipa kiingilio kibwa lkn kesho yake au baada ya wiki timu hiyohiyo ikicheza na nyingine kwenye uwanja huohuo kingilio ni tofauti kabsaa, vp hapo viti huwa vinabadilishwa au simba na yanga zikikutana uwanja unafungwa AC ndio maana viingilio huwa vikubwa? Na sijawahi kusikia mtu akisema amepigwa.
 
Hivi wakuu kwa mfano TV YA ALITOP INCH 32 KWA lindi kuna kipindi nilinunua 260000 je mnamaanisha kwamba kwa kariakoo assume bila winga unaweza kuipata kwa 200000?
BEI ZA TV KWA LEO
🔥 Offer offer 🔥
SAMSUNG
40(SMART)...........550000

65(UHD 4K).........1800000

LG
65(UHD 4K).........1800000

70(UHD 4K).........2100000

TCL
43(smart frameless android)....575000

50(smart Android 4k).....880000

55(smart Android 4k...985000

65(smart frameless android UHD)...........1480000

BOSS
32(frameless)...........225000

43(smart frameless).....460000

55(smart Android double)....800000

55(smart WebOS).......930000

ZUNNE
43(smart frameless)...430000

LITTLE MORE
43(frameless smart)....430000

SOLAR MAX
21(double)............110000

22(single)............115000

24(single)...........130000

24(double)..........140000

42(frameless kawaida)....360000

43(smart frameless haijatimia vizuri)....................380000

43(double normal).......395000

43(double smart).....420000

Star x

50 (smart)...800000

58(smart android)...1020000

ALYONS
17(double).............100000

19(double)..............110000

22(double)..............125000

32 ( fremless) .....215000

32(double)...........220000

EVVOL
N32 ( sio smart ) .....220000

ARBODER
19(DOUBLE)...........110000

MAISHA
24( double).....135000

ZAC
32(frameless).....210000

MO ELECTRO
43 (frameless)..... 490000

SKYWORTH
65(SMART UHD ANDROID)....1400000


HIGH Q
43(normal frameless).....390000

43(smart frameless).......415000

_


NB:ambazo hatujaweka kwenye orodha zimeisha kwa sasa mpka hapo baadaye tena
 
Ila mkuu, hawa mawinga tukiwaendekeza ni suala la muda tu hawatadhibitika kama vishoka.
Mfumo utawaondoa, leo china au nchi nyingine zilizoendelea ukitaka kufika dukani kwake hataki, anataka kila kitu tumalizane online na anauzia dunia nzima kuliko wewe unayedisplay, ukija kwa hawa waswahili wetu ukimwambia nitumie picha ya bidhaa unayouza tayari biashara imekufa au yaweza kuchukua masaa kadhaa kupata hiyo picha na usije ukarogwa ukamwambia picha haionekani vizuri atakuwa hakusikilizi tena.
 
Kwema Wakuu!

Nimemsikia ndugu yangu ngara23 akilalamika mwezi mzima wa Tisa, na sasa tumeingia mwezi wa Kumi bado anaendelea kulia.

Kariakoo mawinga kabla mteja hajafika tayari wanakuwa na bei wameshakubaliana karibu mtaa mzima.

Mfano, umeenda kununua fridge aina ya Hisense lita 160, watakubaliana labda laki sita na tisini.

Ukifika, atakayekupokea atakuambia laki saba na nusu, kisha atajifanya anakupunguzia mpaka 690k. Hapo atasisitiza kuwa hapunguzi kwani amepunguza vya kutosha.

Wakati huo fridge bei yake ni 570k hadi 620k. Hivyo, ukijichanganya si ajabu ukapigwa zaidi ya laki moja.

Sasa ili usipigwe zingatia mambo yafuatayo:

  1. Kusanya taarifa za kitu unachotaka kununua kabla ya kwenda Kariakoo. Ikiwa tayari una pesa au unatarajia kuwa nazo wiki moja ijayo, fanya utafiti mtandaoni na tembelea maduka Kariakoo ukiwa huna pesa ili ufanye upelelezi vizuri. Kisha weka wastani wa bei baada ya kufanya upelelezi. Mfano wastani wa Hisense ni 670k.
  2. Usiingie kwenye maduka yenye mtaji mdogo. Kadiri mtaji unavyokuwa mkubwa, ndivyo uwezekano wa kupata bidhaa za bei nafuu unavyokuwa mkubwa.
  3. Epuka maduka yaliyopo mbele ya barabara. Ikiwa mbele ya barabara, basi loweka kwenye ghorofa. Mtaji mdogo + mbele ya barabara = bei za juu. Zunguka upande wa nyuma, kisha angalia duka lenye mtaji mkubwa, hapo kuna nafasi ya kupata bei nzuri.
  4. Usiingie dukani na kununua kwenye maduka yenye wauzaji wengi, hasa wale watakaokurukia. Duka lenye vijana wengi kupigwa ni rahisi zaidi. Hautakuwa na uhuru wa kufikiri vizuri kwani watakuzonga sana.
  5. Hakikisha unamtambua mwenye biashara au msimamizi wa duka. Hawa mara nyingi hawatakupokea na huwa ndani wakishughulikia shughuli za duka kama hesabu. Ukiona mtu anajifanya yupo busy, mfuate huyo na uliza bei.
  6. Usiwe mwepesi kuuliza bei. Zunguka dukani kama unashangaa bidhaa kabla hawajajua unataka kununua nini. Baada ya muda utajua mazingira ya duka na kiongozi wa duka ni nani, kisha uliza bei ya bidhaa unayotaka.
  7. Tekni za kupunguza bei (bargain price techniques). Ikiwa amekutajia bei ya kuanzia laki tatu hadi laki tano unusu, punguza laki moja na hamsini. Mfano, fridge bei yake laki 7, mwambie una laki tano hamsini hadi sabini. Ukimfuata mwenye duka, punguza kidogo kidogo hadi mfikie bei unayoitaka.
Nenda ukiwa umevaa kawaida, na usiongee sana ili wasicheze na akili yako. Kumbuka kuwa mawinga, sarange, madalali, na wafanyabiashara wana uwezo wa kusoma saikolojia za wateja wao.

Acha nipumzike sasa.
Kariakoo ni sehemu ya masikini kwenda kufana shoping
 
Back
Top Bottom