Kwema Wakuu!
Nimemsikia ndugu yàngu
ngara23 akilalamika Mwezi mzima wa Tisa na Sasa ñàona tumeingia Mwezi wa Kumi bado anaendelea kulia.
Kariakoo mawinga Kabla mteja hajafika tayari wanakuwa na bei wameshakubaliana Karibu Mtaa mzima.
Mfano, umeenda Kununua Fridge aina ya hicense lita 160 wàtakubaliana labda Laki Sita na tisini.
Ukifika, wewe atakayekupokea atakuambia Laki Saba na nusu.
Kisha atajifanya anakupunguzia mpka 690k. Hapo atazinda kuwa hapunguzi kwani amepunguza vya kutosha.
Wakati Hilo Fridge bei yake 570-620k. Hivyo ukijichanganya siô ajabu ukapigwa zaidi ya Laki moja.
Sasa ili usipigwe zingatia Mambo yafuatayo;
1. Kusanya tàarifa za kitu ambacho unaenda kununua Kabla hujaenda Kariakoo.
Tayari unahela au unatarajia kuwa na Pesa wiki Moja ijayo.
Fanya survey huku na Huko, Mitandaoni, tembelea maduka Huko Kariakoo ukiwa huna pesa ili uwe comfortable kufanya upelelezi wako.
Kisha weka wastani WA bei ya Bidhaa baàda ya kufanya upelelezi.
Wastani Umepata Hisence NI 670k.
2. Usiende kwèñye Maduka yenye Mtaji Mdogo.
Ingawaje Maduka mengi huwa ni display tuu na mzigo mwingi upo stoo lakini hutoshindwa kujua Duka lenye mtaji Mkubwa.
Kadiri mtaji unavyokuwa Mkubwa ndivyo possibility ya kupata Vitu vya bei rahisi NI Mkubwa.
3. usiende Maduka yaliyopo Mbele ya Barabara, Chini.
Likiwa mbele y Barabara baasi lowe ghorofani.
Mtaji Mdogo+ mbele ya Barabara automatically tunatarajia Vitu vitakuwa bei ya juu.
Zunguka upande wa Nyuma au Mtaa WA nyuma, Kisha angalia Duka lenye mtaji Mkubwa Hapo kûna possibilities ya kupata Vitu Kwa bei ràfiki.
4. Usiingie na kununua Duka lenye Wauzaji wengi hasa wale watakaokurukia na kudandia.
Duka lenye Vijana wengi kupigwa NI dakika Mbili. Zaidi hautakuwa na Uhuru wa Kufikiri Sawasawa kwani watakuwa wanahakikisha wanakuzonga. Kama wewe siô Mtu unayejimini na mwepesi kushawishiwa Basi Maduka yenye mawinga wengi haiwezi kuwa option nzuri kwako.
5. Hakikisha unamtambua mwenye biashara au aliyeachiwa biashara.
Hawa mara nyingi hawatakupokea na huwa ndàni Kabisa wakiendelea na aidha Kúpiga hesabu, kuandika hesabu, kukata risiti, na Kutoa maelekezo.
Utawatambua Kwa Saikolojia Yao jinsi ilivyo. Kwanza hawatakuwa na kiwewe cha kukukaribisha, facial expressions zào NI kama hazipo Moja Kwa Moja na wéwe Bali zitakuwa zinawasaliana na mawinga, au ukiingia hata kama alikuwa Hana Kazi atajifanya anapanda juu kuchukua mzigo au kushusha Bidhaa, au kuandika andika ilimradi Kutoa Nafasi kwa Winga mmoja kûja kukuhudumia
Wewe ukiona hivyo mfuate huyohuyo àmbaye anajifanya yupo busy Kisha uliza bei.
6. Usiwe mwepesi kuuliza Bei.
Fika dukani, zunguka kama unashangaa Bidhaa Kabla hawajajua unàtaka kununua nini. Waô watakuwa wanakuuliza unàtaka nini. Wewe usiwajibu endelea kushangaa Bidhaa Moja baada ya ñyiñgine.
Baàda ya dakika utakuwa sehemu ya mazîngira ya Duka lile Akili na Hisia zako zitakuwa comfortable na tayari utaanza kuelewa lugha na mahusiano ya mule dukani na waliopo.
Ulizia Vitu àmbavyo haunashida navyo Siku hiyo.
Yaani wewe umeenda Kununua Washing machine, lakini unaulizia Pressure cooker. Wakati wanakuelekeza, endelea kufuatilia wateja wenzako wakitaka Nani anakuwa incharge kama Kiongozi wa Hilo Duka.
Ukishajua, unamfuata na kuulizia bei ya Washing Machine NI ngapi.
Kikawaida ukimfuata mwenye Duka au Msimamizi WA Duka utaona body language ya mawinga na mwenye Duka zikiwasiliana ingawaje siô Kwa Mdogo.
Mwenye Duka atakuwa Hana jinsi Ikiwa utamdhibiti machoni na hakikisha maneno ya mawinga yasikutoe kwèñye shabaha.
7. Tekniki ya kupunguza bei ya Bidhaa (bargain price Technics)
Kama amekutajia bei kuanzia Laki tatu Mpaka Laki tano unusu punguza Laki na ishirini Mpaka Laki na hamsini
Mfano, anakuambia Fridge bei yake Laki 7.
Mwambie Una Laki tano hamsini mpaka sabini.
Muda huo úwe nahakika unayeongea naye NI mwenye Duka au Msimamizi WA Duka Hilo. Atakuambia bei ya mwisho 680k wewe panda Mpaka 590. Atashuka mpka 670. Wewe mwambie 600k.
Atashuka mpka 665k huku akikazana amekusaidia Sana.
Mwambie mfuko wako umeishia Hapo. Huku unajifanya unàtaka kuondoka. Atakuambia Basi lete 660k.
Mwambie 610k ukiwa Sasa upo MLANGOni unaondoka huku kwamba utarudi.,
Bei kuanzia 150k Mpaka 300k
Punguza 50-70.
Mfano amekuambia Pressure Cooker lita 6 NI Tsh 200k.
Guna Kisha akikuuliza unangapi mwambie parefu Sana. Wewe Una 120. Atacheka. Muulize bei ya kuuzia. Atakuambia lete 190k mwambie 130k. Atakuambia upo chini Sana.
Mwambie kûna Mtu alikudanganya kuwa Yake alichukua 135k. Atakuambia huo NI wongo Kisha atakuambia, wewe mwisho unangapi. Mwambie 140k huku ukiondoka, atakuambia leta 180k huku akijifanya anakufungia. Wewe toa 150k pekee kuwa ndîo upo nazo. Kama haiwezeniki mwambie ndîo Pesa uliyonayo.
Kwa bei 50k to 100k punguza 15- 25
Kwa bei ya 10k - 50k punguza 7k to 10
Kwa bei ya 5k to 10k punguza 2k to 4k
Nenda ukiwa umevaa Kawaida siô uende kama unasafiri.
Usiwe mjuaji na muongeaji ongeaji hii itawapa Nafasi ya kucheza na Akili yako. Kumbuka mawinga, Sarange, madalali, na wafanyabiashara wanaujuzi WA kusoma Saikolojia za wateja waô.
Acha nipumzike sasa