Jinsi ya kumfanya mwanamke akuheshimu na aheshimu muda wako

Jinsi ya kumfanya mwanamke akuheshimu na aheshimu muda wako

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Asili ya mwanamke ni kuharibu mambo.

Asili ya mwanaume ni kuweka vitu pamoja/ kuvifanya viwe vya sawa/kawaida.

Kwaiyo ukiona mwanamke anakufanyia vitu vya ajabu, anachafua mambo, anaharibu mambo, anavunja mipaka ujue ni kazi yako kuvifanya virudi kwenye mstari.

Sababu maamuzi yao yanatokana na hisia za muda huo.
Lakini wewe ndo umepewa tochi ya kuongoza mahusiano bila kujali hisia zenu za muda huo.
.
Kwenye kuongoza mahusiano lazima uwe na mipaka na misimamo.
Mipaka na misimamo ndo heshima yako mwanaume.
Ukishaheshimika utapendwa.
Na uisimamie bila huruma wala hisia. Hata huyo mwanamke anakutegemea uwe hivyo. Japo mara kwa mara atakushawishi kuvunja mipaka.

Ukivunja mara moja atataka ajue utavunja mara ngapi, atakujaribu zaidi.
Mpaka inafikia hatua hakuheshimu tena.
Sababu mipaka yako imeshavunjwa.
Na umemvumilia dharau zake ukiamini ipo siku atabadilika.
Lakini kila siku anakua jeuri kwako na anakudharau.
Ukishadharaulika unachukiwa.

Haijalishi umeishi na mwanamke kwa miaka mingapi. Akikudharau tu, huna chako tena.

Maana hutakua kipaumbele chake tena.
Hatojali muda mliopanga, hatotaka kupendeza kwako na hatokua anakuridhisha kimapenzi.
.
Cha kufanya.
- Pitia upya mipaka yako.
Jiangalie wewe kwanza, kabla kumlaumu mwanamke anakudharau.
Angalia ni kipi umekua kimuachia japo hupendi/ ulishamkataza.
Angalia ni wapi anavunja ratiba zako kwa mambo yasiyoeleweka.
Angalia ni wapi hakuridhishi japo ulishamwambia na ukapotezea.
Kisha ikazie misimamo na mipaka yako upya.
Mwanzoni hiki utapata shida. Sababu ulishamzoesha kuwa anaweza kukudharau. Lakini kazia, isisitize mpaka aelewe.
Rudisha heshima yako ndani.

- vaa ujasiri wako.
Mwanamke ana asili ya udhaifu.
Hudharau vidhaifu vingine. Ikiwemo wewe kama ukiwa dhaifu.
Lakini wanaheshimu na kupenda mtu jasiri. Kuwa wewe.
Haijalishi huyo mwanamke ni nani kwako, kuwa jasiri unapokua naye.
Usiogope atakukataa au la, usisite kuhimiza mipaka/ misimamo yako.
Akikuudhi usimnyamazie tu mwambie anapokukwaza.
Usikubali akuharibie ratiba/ bajeti, hata kama amekuahidi kulala nawe.

- Kuwa na maamuzi.
Pia utambue baadhi ya maamuzi utakayofanya hayatakua bora, au utokea lakini ni bora kuliko kumuachia mwanamke maamuzi.
Na uwe kiongozi kwenye mahusiano.
 
Kunguru afugiki akivunja mkataba nawe unavunja mkataba, kwann ubebe mzigo wa malezi mabovu ya mama yake.
Dharau ni matokeo ya malezi na ujinga, huwezi mbadilisha unaangalia jinsi ya kuponya roho yake. Kwann uhangaike kuosha nyanya chafu wakati nzima zipo tele?
 
Dawa ni kuachana nae tu.
Asili ya mwanamke ni kuharibu mambo.
Asili ya mwanaume ni kuweka vitu pamoja/ kuvifanya viwe vya sawa/kawaida.

Kwaiyo ukiona mwanamke anakufanyia vitu vya ajabu, anachafua mambo, anaharibu mambo, anavunja mipaka ujue ni

- Kuwa na maamuzi.
Pia utambue baadhi ya maamuzi utakayofanya hayatakua bora, au utokea lakini ni bora kuliko kumuachia mwanamke maamuzi.
Na uwe kiongozi kwenye mahusiano.
 
Mwanamke kama hana heshima na utii aachane na kitu kiitwacho ndoa
 
Mwanamke akishakudharau, kuja kukuheshimu tena ni uongo. wana mioyo ya ajabu sana hawa watu wakiamua lao likiwa negative umekwisha.

Akishakudharau hautakuwa comfortable kwake. uta loose tu. hautajiamini mbele yake na hapo otherwise uwe mtemi
 
Yaani gazeti lote hili ni kwa ajili ya kumfanya Mwanamke akuheshimu!!?

Bro, Pesa ndio heshima pekee Duniani, utaheshimiwa sio tu na Mwanamke hadi viongozi wa Dini na wa Serikali,

#TAFUTA PESA.
Pesa itakuletea heshima za kinafiki kuna mambo hata wasio na hela wanaheshimiwa na wake zao malaya ndio wanaheshimu pesa
 
Mwanamke kukuheshimu ni lazima. Kama hafanyi hivyo fukuza haraka sana
Nakubali mkali tatizo wanaume hawajiamini ile kauli ya hela mbele imeathiri wanaume wengi lakini mifano tunayo humu humu kwenye jamii zetu wapo watu vipato vya kawaida na hawaletewi dharau za ajabu ajabu. Pesa inaleta amani sana ukiwa nayo ila wapo watu kibao na pesa zao hawaheshimiwi kabisa
 
Nakubali mkali tatizo wanaume hawajiamini ile kauli ya hela mbele imeathiri wanaume wengi lakini mifano tunayo humu humu kwenye jamii zetu wapo watu vipato vya kawaida na hawaletewi dharau za ajabu ajabu. Pesa inaleta amani sana ukiwa nayo ila wapo watu kibao na pesa zao hawaheshimiwi kabisa
Hilo ukilielewa maisha yanakuwa mepesi. Kuna watu wanateseka na hela zao. Noma kweli yani.

Misimamo ndio kila kitu, kataa ujinga wa mwanamke asepe zake. Akijua unakaza hawezi kuleta utoto.
 
Yaani gazeti lote hili ni kwa ajili ya kumfanya Mwanamke akuheshimu!!?

Bro, Pesa ndio heshima pekee Duniani, utaheshimiwa sio tu na Mwanamke hadi viongozi wa Dini na wa Serikali,

#TAFUTA PESA.
Sishangai kwanini ulikomenti vile kwenye Uzi wa hakimi.
 
Back
Top Bottom