Basi jana nimerudi kwenye mood ya mapishi, nikajiandaa nikapika chapati.
Mmh, walau nime improve kutoka mifuniko ya masefuria to something very new. Chapati hazikuwa ngumu wala laini, zilikuwa slippery kama ulimi wa Mlugo. Ukitafuta hivi, meno yanakuwa kama yanafanya 'ice skating', ukiweka mchuzi ndio inakuwa poa.
But zombie alinielekeza wapi nilikosea, nilitumia maji moto badala ya baridi. So leo narudia homework.
cc King'asti na snowhite, mwenzenu naumbuka jamani. Ingekuwa si kuogopa haya ma ID tungekuwa tunakutana once in a while kupika tu, tuna rotate kwa nyumba tofauti tofauti, tunakuja na vifaa vya tunavyotaka kupika, na ma hot pot ya take away.
Tukirudi home ni kuchemsha tu watu wanakula.
Jaribu tena unga jaribu kuukanda vizuri na si kuutia maji mengi......
Wakati unasukuma unahisi hasa hii chapati ya ukweli
Last edited by a moderator: