Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

Mahitaji:
Unga wa ngano kilo 1
Mayai 2
Chumvi
Maji
Siagi (butter) vijiko 3 vikubwa
Mafuta ya kula kwa ajili ya kuchomea
Iliki ya unga
Maziwa ya unga vijiko 3 vikubwa
Maelekezo:
Weka unga kwenye beseni au sufuria kavu kisha weka chumvi kiasi, maziwa vijiko 3 vya chakula na hiriki. Changanya mpaka uhakikishe vimechanganyikana vizuri.

Weka butter vijiko vitatu kwenye unga kisha changanya. Changanya hadi butter ishikane na unga vizuri na iwe na uwiano mzuri (isionekane kabisa).

Pasua mayai pembeni, yakoroge vizuri na kisha weka kwenye unga. Changanya zaidi hadi upate uwiano unaofaa.

Ukiona uwiano mzuri wa unga wako, weka maji ya uvuguvugu kwenye unga na anza kukanda. Kanda unga mpaka uwe laini na haushikani na chombo unachokandia wala haunati kwenye mikono. Hapo unga utakua tayari.

Kata mabonge ya unga kwa umbo la mviringo kisha weka kwenye chombo pembeni. Rudia hili zoezi hadi unga uishe.

Chukua donge mojamoja, paka unga weka kwenye kibao cha kusumia chapati. Sukuma chapati hadi iwe sawa. Paka mafuta kwenye chapati na anza kukunja.

Rudia hilo zoezi kwa madonge yote yaliyobaki. Ukimaliza, anza kusukuma chapati zako kwa ajili ya kupika.

Bandika kikaango jikoni. Acha kipate moto vizuri.

Weka chapati, acha iive hadi iwe rangi ya kahawia. Geuza upande wa pili, paka mafuta upande uliokua wa kahawia. Geuza, paka mafuta tena upande mwingine.

Hakikisha chapati inaiva vizuri na inachambuka,hapo utakua umemaliza kazi na tayari kula chapati zako.

6dad1ab84953baf6e47a820b921d16efc0eadaf4.jpeg
 
Thank you thank you, nitapika hii
Duh zako zilivo nene ukila moja tu unalala kitumbo juu
 
Tatizo kubwa la watengeneza chapati ni katika kuifanya iwe laini baada ya kuiva, nyingi huwa ngumu kama ngozi ya ngombe iliyokaushwa!

Je ni maandalizi ya aina gani yanayotakiwa ili kuhakikisha chapati unayoiandaa iwe laini baada ya kuipika/ ichoma n.k??
 
Hizi chapati kwa kuziangalia tu ni tamu. Ntazipika kwakweli maana nlikuwa natia maziwa kwenye pancake kumbe hata hizi za kusukuma. Asante sana
 
Asante sana tena ngoja niitupie bookmark kabisa ni moja kati ya useful uzi kwangu mie..
 
Back
Top Bottom