Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

Umekanda unga mgumu!!
Ndani umeweka mafuta gani kabla ya kusukuma dada! Jitahidi utumie KIMBO my dear, halafu ziache ziumuke baada ya dk 20 mpaka 30.
Unga ulikuwa mlaini jamani, mafuta nimetumia ya alizeti hivi ya kimbo yapo miaka hii? Nayatumia kukandia tu au mambo yote
 
Kama kuna chakula napenda ni vyapati. Dah! Hata kavu nakula nalala. Ila iwe laini na nene. Sio hizi nyembamba utadhani wembe!! Hata ukiikata tu tiyari ishaharibu appetite.
Naomba jamani, ka kuna fundi karibu niweke order ya vyapati 30 yaani kila siku nile 1
 
Unga ulikuwa mlaini jamani, mafuta nimetumia ya alizeti hivi ya kimbo yapo miaka hii? Nayatumia kukandia tu au mambo yote
Mafuta yapo ya KIMBO dada,
Unatumia kusukumia baada ya kukata yale matonge, unasukuma unapaka halafu unasokota dada au wewe huwa unafanyaje
 
Watumia alizeti pia, KIMBO wapaka baada ya kusukuma tonge lako then wasokota.. Kama yako matonge 6 wapaka yotee, then unayaacha yanaumuka dada ndo usukume sasa chapati
Hizo hatua huwa nafanya ila sijui nakwama wapi walah
 
Back
Top Bottom