Jinsi ya kupika chapati za maji ambazo hazina viungo vingi

Aaliyyah

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2022
Posts
19,041
Reaction score
46,239
Natumaini mkopoa

Tujifunze namna ya kupika chapati za maji Kwa njia rahisi na haraka pia ni moja ya vitafunwa ambavyo havina mambo mengi

Mahitaji
Ngano robo au kias unachopenda Kulingana na familia Yako
Iriki au vanilla
Sukari /chumvi ni vile upendavyo
Yai moja au mawili
Maji ya baridi

Hatua
Chukua bakuli safi na kavu weka ngano na sukari Changanya kidogo Kisha Anza kuweka Maji ya baridi kidogo kidogo huku unakoroga had utapoona ngano Yako imekuwa uji mzito hakikisha hauna mabonge

Ongezea mayai pamoja na iriki au vannila endelea kukoroga kama itakuwa Bado nzito ongezea maji kidogo Ili upate uji ambao sio mzito Wala mwepesi Sana

JINSI YA KUPIKA
Weka pan Yako jikoni subir ipate moto hakikisha moto sio mkali. Kama pan sio non stick ipake mafuta kidogo ikipata joto

Weka uji wako wa ngano katika pan acha Kwa dakika 1 au 2 had uone Inakuwa kavu kidogo geuza upande wa pili nao acha kidogo Kisha weka mafuta nusu kijiko Chakula upande mmojaKisha geuza upande mwingine nao hivo had uone imebadilika rangi

Toa chapat zako jikoni zitakuwa tayari. Sio mjuzi sana wa mapishi karibuni pia kuongezea maoni

Unaweza kunywa na chai ya rangi hata maziwa

 
Shangaziii mbona hukunifundsha nimpikie ankolii wakoo,
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Shangazi yangu wewe nimekuandalia notes za kutosha pamoja na kiboko πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…