Habari za mapumziko ya mwisho wa wiki,
Leo nimeona bora niwashirikishe jambo moja hasa wale wanaoishi single a.k.a bachelor.
Mara nyingi nimeona watu wa kada hii husumbuka sana katika maandalizi ya chakula na kupelakea kuwa na mahusiano mazuri na wauza chips au Mama lishe ili angalau kuitendea haki miili yao, na mara nyingine wanabuni mboga rahisi kama mayai, dagaa wa kukaanga na mtindi ili kukamilisha zoezi. Lakini napenda kuwajulisha sasa unaweza kupika maharage kwa dk 10 na ukafurahia maisha, fuata maelekezo haya;
1. Andaa maharage yako tayari kwa kupikwa,
2. Washa jiko lako kisha tenga maharage yako, subiri mpaka yachemke kabisa (boiling point)
3. Mimina maharage na maji yake kwenye Thermos (chupa ya chai) hakikisa chupa yako haipozi, na pia hakikisha maji yanajaa mpaka juu.
4. Funika chupa yako vizuri kisha ondoka nenda kazini.
5. Ukirudi toka kazini njoo na nyanya,vitunguu,karoti nk tayari kuunga maharage yako tayari kwa kuliwa.
Nawatakia Siku njema, nasubiri mrejesho.
Stay blessed