Jinsi ya kupika maharage kwa njia rahisi bila kutumia gharama kubwa

Jinsi ya kupika maharage kwa njia rahisi bila kutumia gharama kubwa

Kiafya inakubalika?
Yes, kitu kinachofanyika hapo in kisayansi zaidi, kwa kuwa maji yakichemka hayazidi nyuzi jota mia, zaidi ya hapo yanakuwa mvuke na unapotea angani, kinachofanyika ni kuzuia evaporation na kumaintain water temperature, then tunakata moto. That's all
 
Habari za mapumziko ya mwisho wa wiki,

Leo nimeona bora niwashirikishe jambo moja hasa wale wanaoishi single a.k.a bachelor.

Mara nyingi nimeona watu wa kada hii husumbuka sana katika maandalizi ya chakula na kupelakea kuwa na mahusiano mazuri na wauza chips au Mama lishe ili angalau kuitendea haki miili yao, na mara nyingine wanabuni mboga rahisi kama mayai, dagaa wa kukaanga na mtindi ili kukamilisha zoezi. Lakini napenda kuwajulisha sasa unaweza kupika maharage kwa dk 10 na ukafurahia maisha, fuata maelekezo haya;

1. Andaa maharage yako tayari kwa kupikwa,

2. Washa jiko lako kisha tenga maharage yako, subiri mpaka yachemke kabisa (boiling point)

3. Mimina maharage na maji yake kwenye Thermos (chupa ya chai) hakikisa chupa yako haipozi, na pia hakikisha maji yanajaa mpaka juu.

4. Funika chupa yako vizuri kisha ondoka nenda kazini.

5. Ukirudi toka kazini njoo na nyanya,vitunguu,karoti nk tayari kuunga maharage yako tayari kwa kuliwa.

Nawatakia Siku njema, nasubiri mrejesho.

Stay blessed

Umesema dk 10 kisha unasema”Ukirudi toka kazini”.......!!!!Kazi gani ya kutoka na kurudi ndani ya dk 10.
 
Mkuu umechapia kidogo sio dk kumi unatakiwa unayaache usiku mzima au kama unaweka asbh jioni ukitoka kazini ndondo tayari
 
Napenda maharage na wali au na ugali au na chapati kuliko hata navyopenda nyama au samaki, ila issue ni kuyapika huku mjini ni gharama sana mpaka uwe na mkaa.

Hivi kwa mtu aliye bachelor ni bora kununua maharage yaliyopikwa mgahawani au bora kununua maharage na mkaa na kupika? Kipi nafuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nunua pressure cooker kama hauna. Kisha nunua maharage loweka nenda kazini (Kama ni magumu), ila pia sio lazima kuloweka. Tia kwenye pressure cooker maharage yako, washa jiko lako nusu saa yameiva.
 
Nunua pressure cooker kama hauna. Kisha nunua maharage loweka nenda kazini (Kama ni magumu), ila pia sio lazima kuloweka. Tia kwenye pressure cooker maharage yako, washa jiko lako nusu saa yameiva.
Asante sana mkuu presha cooker kwa jiko la mkaa unaweza kutumia mkaa wa pesa ngap?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nichemsha maharage kiko mbili mara moja kwa mwezi. Yakiiva ninaacha yapoe ninatia kwenye mabakuli ya plastic ya 1/2 kilo ni awe is kwenye freezer.
 
Back
Top Bottom