SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Ziwa Natron linalopatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania mkapani na Kenya lina chemical materials ambazo ni muhimu viwandani. Ziwa Natron lina sodium carbonate na baking soda zenye matumizi mbalimbali.
Kama umeangalia kwa makini mwendelezo katika nyanja za sayansi, teknolojia na uvumbuzi duniani utaona na kugundua kuwa moja ya kitu kinachosukuma mabadiliko hayo ni ubunifu wa betri zinazoweza kukaa kwa muda mrefu.
Kuanzia kwa drones, magari ya umeme, baiskeli na pikipiki za umeme, umeme wa nishati mbadala kama jua, laptop computers, cellphones, machine zinazoongozwa na Artificial Intelligence, nk. hizi zote zinasukumwa na maboresho na ubunifu wa betri zinazoweza kukaa muda mrefu na ambazo ni "rechargeable". Ziwa Natron lina kemikali zinazoweza kutumika katika utengenezaji wa betri hizo.
Kuna mahitaji ya glass/vioo kwa matumizi mbalimbali. Duniani kote matumizi ya vioo ni makubwa sana. Kuanzia kwenye utengenezaji wa madirisha, milango na kuta za majengo ya kisasa, vioo vya magari, treni na ndege, vioo vya furniture, vyombo vya jikoni, electronics, nk. matumizi na mahitaji ya vioo ni makubwa sana. Ziwa Natron lina kemikali zinazohitajika sana katika utengenezaji wa vioo.
Embu niambieni nini nisichojua kinachokwamisha Ziwa Natron lisitumike ipasavyo kukuza uchumi wa nchi.