DOKEZO Jinsi ziwa Tanganyika lilivyo na maji mengi

DOKEZO Jinsi ziwa Tanganyika lilivyo na maji mengi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Lakini huko huko Korogwe huwaambii kitu kuhusu CCM. Nini nataka kusema hapa? Tumewarahisishia kazi viongozi wetu kutufanyia watakacho. Kwahivyo shida imeanzia kwetu
Ishia hapo hapo. Korogwe sio CCM kamwe. Walio kuwa Madarakani (marehemu mkurugenzi) walikataa kupokea fomu ya mgombea wetu bi Aminata Saguti, hata huyo chaguo la CCM hakuchukuliwa. Aliokotwa mtu jalalani ndio kasimikwa.
 
Kijiografia ziwa Tanganyika linakiwango kidogo cha chumvi, kwa sababu limepakana na maeneo yenye madini chumvi.... Mvua ikinyesha uvinza moja kwa moja maji yake uelekea ziwa Tanganyika, sasa chumvi inakosaje??????
Umewahi kufika Uvinza?.Nina maana yangu Kukuuliza hivyo.
 
Kwa nini mradi wa maji Tabora - Nzega walichukua ziwa Victoria badala ya ziwa Tanganyika, wakati ziwa Tanganyika lipo karibu na Tabora kuliko ziwa Victoria?

Na ninasikia mpango ni kufikisha maji ya Ziwa Victoria Dodoma.
Nadhani walitaka kunufaisha mikoa mingi zaidi,km Shinyanga,Simiyu,Tabora,n.k.
 
Ziwa Tanganyika ni la 2 duniani kwa kuwa na kina kirefu, kwa ukubwa Ziwa Victoria ni la 3 duniani na Tanganyika nazani ni la 5 au 6 kwa ukubwa
Tanganyika linamaji mengi kwasababu kwanza lina outlet moja tu kule Zambia inayopeleka maji mto Congo, pili lina kina kirefu. Disadvantage ya ziwa ni uwepo wa samaki wachache nazani inachangiwa na uwepo wa species chache za samaki
Outlet inaitwa mto lukuga ipo kongo katika mji wa kalemie..sio zambia.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu acha tununue ndege kwanza,, ujue ndege ni muhimu sana kuliko kitu chochote,, wapinzania mlitusema sana enzi za jk,, tunahitaji ndege nyingi[emoji847][emoji847]
Priority; priority; priority! Maendeleo ya vitu vs maendeleo ya watu.
 
Nikiwa Rais kipaumbele changu miundo mbinu, maji, barabara umeme hospital shule reli, meli.
Kisha kilimo lazima kiwe cha kumwagilia,, kuhusu umeme tuzalishe Dekawatt 1000.. sio mambo ya MW 3000
Duh mambo ya TW tutaweza kwa kutumia hydro na hata kama itawezekana uwekezaji wake ni mkubwa sana. Embu angalia kwenye hizi MW tu bado finance inasumbua!
Pamoja na weaknesses zake, mwendazake alikuwa anapiga hatua kubwa kwenye swala la miundo mbinu. Naona utataka kufuata legacy yake ukiwa rais
 
Kama Ziwa lingekuwa letu pekeyetu ingekuwa poa, lakini Burundi,Drc,Zambia nao wamo.
Ziwa Victoria sio letu peke yetu, Ila mbona maji yake ndio yanatumika mikoa ya Kanda ya ziwa?
 
Alafu kuna yule punda milia analeta kauzi kake eti oooh tuombe mungu mvua zinyeshe ili mgao wa maji na umeme uishe

Popote ulipo nakupa middle funger
 
Mkuu nachanganyikiwa hapo kwenye height na length ya ziwa. Nilihisi ni kitu kimoja ila naona vipo tofauti. Msaada kwa hili.

Red Giant

dudus
Sawa. Length ni umbali (urefu) toka kaskazini Burundi linakoanzia ziwa hadi kusini nchini Zambia, ni mbali sana! Angalia kwenye ramani.

Height ni kina au kimo (toka juu hadi chini kilindini au chini hadi juu), ambapo Width (upana) ni kutoka upande mmoja wa ziwa kwenda mwingine kwa kukatisha, si kufuata urefu wa ziwa.
 
Duniani ziwa Tanganyika ni la pili kwa ukubwa baada ya ziwa Baikal. Ziwa Baikal lina ujazo wa kilomita za ujazo 23,000 huku Tanganyika likiwa na 18,900. Nyasa lina 8,500 na Victoria lina 2,500. Ziwa Victoria linaingia kwenye ziwa Tanganyika karibu mara nane.

Ziwa Tanganyika lina asilimia 18.9 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia. Tanzania sisi tunamiliki 46% ya ziwa Tanganyika. Kwa maana hiyo, hilo linatufanya tumiliki asilimia kama 8.5 ya maji safi yote yaliyopo kwenye uso wa dunia. Ukijumlisha na sehwmu za ziwa Nyasa na Victoria utaweza kuta karibia asilimia 11 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia yapo Tanzania.

Ukitoa maji yote kwenye ziwa Tanganyika halafu ukasema mito yote duniani itiririke kulijaza, itatumia karibia miezi saba kulijaza. Mto mkubwa wa Amazon utatumia karibu miaka mitatu. Mto Congo utatumia miaka 13.

Ukisema mto Rufiji utiririke kujaza Ziwa Tanganyika utatumia karibu miaka 1,400.

Hili ziwa peke yake linaweza kunywesha kila jiji Tanzania nzima. Na kila mtanzania. Ukipiga hesabu ya watanzania wote milioni 60 na ukipiga hesabu ya kuwa kila mtu, mtu mzima hadi mtoto mchanga anatumia lita mia moja kwa siku utaona kuwa tunahitaji kilomita za ujazo 2.2 kwa mwaka. Kinadharia, kwa idadi hiyo tunaweza kutumia maji ya ziwa hilo kwa miaka 8,500.

Asitokee mtu wa kutuambia tuna upungufu wa maji.
Kama wenzetu wameweza jenga pipe la mafuta toka urusi mpaka germany, tunashindwa kujenga pipe la maji kupeleka mikoa ya pwani? Sometimes hatuhitaji misaada ya hela( hazitumiki ipasavyo, tungeomba msaada wa kujenga pipe
 
Back
Top Bottom