DOKEZO Jinsi ziwa Tanganyika lilivyo na maji mengi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Duniani ziwa Tanganyika ni la pili kwa ukubwa baada ya ziwa Baikal. Ziwa Baikal lina ujazo wa kilomita za ujazo 23,000 huku Tanganyika likiwa na 18,900. Nyasa lina 8,500 na Victoria lina 2,500. Ziwa Victoria linaingia kwenye ziwa Tanganyika karibu mara nane.

Ziwa Tanganyika lina asilimia 18.9 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia. Tanzania sisi tunamiliki 46% ya ziwa Tanganyika. Kwa maana hiyo, hilo linatufanya tumiliki asilimia kama 8.5 ya maji safi yote yaliyopo kwenye uso wa dunia. Ukijumlisha na sehwmu za ziwa Nyasa na Victoria utaweza kuta karibia asilimia 11 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia yapo Tanzania.

Ukitoa maji yote kwenye ziwa Tanganyika halafu ukasema mito yote duniani itiririke kulijaza, itatumia karibia miezi saba kulijaza. Mto mkubwa wa Amazon utatumia karibu miaka mitatu. Mto Congo utatumia miaka 13.

Ukisema mto Rufiji utiririke kujaza Ziwa Tanganyika utatumia karibu miaka 1,400.

Hili ziwa peke yake linaweza kunywesha kila jiji Tanzania nzima. Na kila mtanzania. Ukipiga hesabu ya watanzania wote milioni 60 na ukipiga hesabu ya kuwa kila mtu, mtu mzima hadi mtoto mchanga anatumia lita mia moja kwa siku utaona kuwa tunahitaji kilomita za ujazo 2.2 kwa mwaka. Kinadharia, kwa idadi hiyo tunaweza kutumia maji ya ziwa hilo kwa miaka 8,500.

Asitokee mtu wa kutuambia tuna upungufu wa maji.
Sijawahi kusikia kipimo kinaitwa kilometa za ujazo!
 
Hapo umenena kweli, kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu ni sisi wenyewe. Ina maana siri ya kuendelea au kukwama iko kwetu wenyewe, hususan kwa wenye dhamana ya kutuongoza!

Viongozi ndiyo wabinafsi ,wanajiangalia wao tu na si wananchi,miradi wanayoifanya ya kuzima moto ni kwasababu wanapiga 20%.

Hawana plan.
 
Katika maziwa yote nchini, Victoria linaongoza kwa kunyonywa, mpaka limelala aisee
emoji3.png
emoji3.png
emoji3.png
emoji3.png
Maji ya ziwa Victoria yakifika mpaka Dodoma si ndo maji yatapungua
 
Duniani ziwa Tanganyika ni la pili kwa ukubwa baada ya ziwa Baikal. Ziwa Baikal lina ujazo wa kilomita za ujazo 23,000 huku Tanganyika likiwa na 18,900. Nyasa lina 8,500 na Victoria lina 2,500. Ziwa Victoria linaingia kwenye ziwa Tanganyika karibu mara nane.

Ziwa Tanganyika lina asilimia 18.9 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia. Tanzania sisi tunamiliki 46% ya ziwa Tanganyika. Kwa maana hiyo, hilo linatufanya tumiliki asilimia kama 8.5 ya maji safi yote yaliyopo kwenye uso wa dunia. Ukijumlisha na sehwmu za ziwa Nyasa na Victoria utaweza kuta karibia asilimia 11 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia yapo Tanzania.

Ukitoa maji yote kwenye ziwa Tanganyika halafu ukasema mito yote duniani itiririke kulijaza, itatumia karibia miezi saba kulijaza. Mto mkubwa wa Amazon utatumia karibu miaka mitatu. Mto Congo utatumia miaka 13.

Ukisema mto Rufiji utiririke kujaza Ziwa Tanganyika utatumia karibu miaka 1,400.

Hili ziwa peke yake linaweza kunywesha kila jiji Tanzania nzima. Na kila mtanzania. Ukipiga hesabu ya watanzania wote milioni 60 na ukipiga hesabu ya kuwa kila mtu, mtu mzima hadi mtoto mchanga anatumia lita mia moja kwa siku utaona kuwa tunahitaji kilomita za ujazo 2.2 kwa mwaka. Kinadharia, kwa idadi hiyo tunaweza kutumia maji ya ziwa hilo kwa miaka 8,500.

Asitokee mtu wa kutuambia tuna upungufu wa maji.
Sasa kwa ufafanuzi huu, si bora tungekukabidhi tu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ili utufanyie maajabu!

Uchambuzi umekwenda shule mpaka basi. Ningekuwa mimi ndiyo Rais wa Nchi hii, watu kama nyinyi mngepata shida sana! Maana ningezitumia akili zenu kwa manufaa ya Taifa, mpaka basi.
 
Hii imekaa kitaalamu,hatuna akili,hatuna ubunifu,hatuna nia ya kutoka tulipokwama kila siku tuko palepale

hatuwezi kabisa kutumia rasilimali tulizobarikiwa....hili ziwa lingekuwa uswiss huko lingekuwa na manufaa makubwa sana kwa waswiss.

Ziwa Tanganyika unaambiwa tangu kuumbwa kwake walishavua asilimia 2 tu ya samaki wote waliohai ingekuwa huko mbele hili ziwa lingekuwa na faida kubwa sana kwa nchi,cha ajabu hata waishio jirani na ziwa hili hukosa maji mabombani,tumuombe Mungu atupe akili ya kuziona fursa na kuzitumia Amiin.
usimsumbue Mungu ...unamuomba akupe akili zipi?
 
Sasa kwa ufafanuzi huu, si bora tungekukabidhi tu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ili utufanyie maajabu!

Uchambuzi umekwenda shule mpaka basi. Ningekuwa mimi ndiyo Rais wa Nchi hii, watu kama nyinyi mngepata shida sana! Maana ningezitumia akili zenu kwa manufaa ya Taifa, mpaka basi.
Ukimpa Wizara mtu kama huyu hawezi fanya lolote atabakiwa kuchanganyikiwa tu
 
"Nyasa lina lita 8,500" ?
Hili ni ziwa au tank la maji lililo nyumbani kwa mtu?

Lakini pia wanaposema upungufu wa maji wanamaanisha kwenye vyanzo ambavyo wao ndio wameweka miundombinu.

Ikitokea mvua isinyeshe kwa muda mrefu watalazmika kujenga miundimbinu mipya kwenye vyanzo vingine
[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Ukitaka kujua tofauti ya maji Ziwa Victoria na Tanganyika, Chukua product hizo mbili uonje utapata majibu. Japo yote mnaita maji baridiiiiiiii
maxresdefault.jpg

Kilimanjaro-drinking-water-1024x233-middle.png
 
"Nyasa lina lita 8,500" ?
Hili ni ziwa au tank la maji lililo nyumbani kwa mtu?

Lakini pia wanaposema upungufu wa maji wanamaanisha kwenye vyanzo ambavyo wao ndio wameweka miundombinu.

Ikitokea mvua isinyeshe kwa muda mrefu watalazmika kujenga miundimbinu mipya kwenye vyanzo vingine
Amesema Kilomita za ujazo! Na sio Lita, soma vyema andiko lake.
 
Hapo kwenye kilomita za ujazo naona kama hapako sawa. Ninavyofahamu mimi kilomita ni kipimo cha urefu na siyo ujazo.
Hujawahi pokea Ankara ya maji kwa "meter cubic"? Uwingi unaongezeka kutokana na ukubwa wa kitu kinachopimwa na hasa ujazo. Ingekiwa maji ya kwenye ndoo ungetumia vipimo vidogo.
 
Hujawahi pokea Ankara ya maji kwa "meter cubic"? Uwingi unaongezeka kutokana na ukubwa wa kitu kinachopimwa na hasa ujazo. Ingekiwa maji ya kwenye ndoo ungetumia
Hesabu zilikuwa zinanipiga chenga. Kidato cha nne nusura nipate F. Lakini nikaambulia D.
 
Kwa nini mradi wa maji Tabora - Nzega walichukua ziwa Victoria badala ya ziwa Tanganyika, wakati ziwa Tanganyika lipo karibu na Tabora kuliko ziwa Victoria?

Na ninasikia mpango ni kufikisha maji ya Ziwa Victoria Dodoma.
We ni muongo watu tumezaliwa kigoma maji ya ziwa TANGANYIKA sio ya chumvi acha ujuaji wako ng'ombe wewe.
 
Ni ajabu nchi kama hii Ina maziwa makubwa Tanganyika, Nyasa, Victoria, Rukwa...na mito mikubwa kama Ruvu, Rufiji,Ruvuma, ugalla nk...eti ni Masikini na raia zake hawapati maji safi na salama! Yaani mtu anaweza kuona hii nchi ni ya mataahira!
 
Duniani ziwa Tanganyika ni la pili kwa ukubwa baada ya ziwa Baikal. Ziwa Baikal lina ujazo wa kilomita za ujazo 23,000 huku Tanganyika likiwa na 18,900. Nyasa lina 8,500 na Victoria lina 2,500. Ziwa Victoria linaingia kwenye ziwa Tanganyika karibu mara nane.

Ziwa Tanganyika lina asilimia 18.9 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia. Tanzania sisi tunamiliki 46% ya ziwa Tanganyika. Kwa maana hiyo, hilo linatufanya tumiliki asilimia kama 8.5 ya maji safi yote yaliyopo kwenye uso wa dunia. Ukijumlisha na sehwmu za ziwa Nyasa na Victoria utaweza kuta karibia asilimia 11 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia yapo Tanzania.

Ukitoa maji yote kwenye ziwa Tanganyika halafu ukasema mito yote duniani itiririke kulijaza, itatumia karibia miezi saba kulijaza. Mto mkubwa wa Amazon utatumia karibu miaka mitatu. Mto Congo utatumia miaka 13.

Ukisema mto Rufiji utiririke kujaza Ziwa Tanganyika utatumia karibu miaka 1,400.

Hili ziwa peke yake linaweza kunywesha kila jiji Tanzania nzima. Na kila mtanzania. Ukipiga hesabu ya watanzania wote milioni 60 na ukipiga hesabu ya kuwa kila mtu, mtu mzima hadi mtoto mchanga anatumia lita mia moja kwa siku utaona kuwa tunahitaji kilomita za ujazo 2.2 kwa mwaka. Kinadharia, kwa idadi hiyo tunaweza kutumia maji ya ziwa hilo kwa miaka 8,500.

Asitokee mtu wa kutuambia tuna upungufu wa maji.
Ziwa Victoria ni kubwa kuliko Ziwa tanganyika. Hizi data umezitoa wapi? Na hizo units ulizozitaja hapa ziko kwenye vipimo gani, vya nini?
Angalia hapa:

Back
Top Bottom