Ishia hapo hapo. Korogwe sio CCM kamwe. Walio kuwa Madarakani (marehemu mkurugenzi) walikataa kupokea fomu ya mgombea wetu bi Aminata Saguti, hata huyo chaguo la CCM hakuchukuliwa. Aliokotwa mtu jalalani ndio kasimikwa.Lakini huko huko Korogwe huwaambii kitu kuhusu CCM. Nini nataka kusema hapa? Tumewarahisishia kazi viongozi wetu kutufanyia watakacho. Kwahivyo shida imeanzia kwetu
Sawa, nimekupata MkuuKumbuka GDP per capita inavyopatikana.
Sio Bahari ya Hindi kweli?.hivi chanzo cha mto ruvu ni wapi?
Umewahi kufika Uvinza?.Nina maana yangu Kukuuliza hivyo.Kijiografia ziwa Tanganyika linakiwango kidogo cha chumvi, kwa sababu limepakana na maeneo yenye madini chumvi.... Mvua ikinyesha uvinza moja kwa moja maji yake uelekea ziwa Tanganyika, sasa chumvi inakosaje??????
Nadhani walitaka kunufaisha mikoa mingi zaidi,km Shinyanga,Simiyu,Tabora,n.k.Kwa nini mradi wa maji Tabora - Nzega walichukua ziwa Victoria badala ya ziwa Tanganyika, wakati ziwa Tanganyika lipo karibu na Tabora kuliko ziwa Victoria?
Na ninasikia mpango ni kufikisha maji ya Ziwa Victoria Dodoma.
Outlet inaitwa mto lukuga ipo kongo katika mji wa kalemie..sio zambia.Ziwa Tanganyika ni la 2 duniani kwa kuwa na kina kirefu, kwa ukubwa Ziwa Victoria ni la 3 duniani na Tanganyika nazani ni la 5 au 6 kwa ukubwa
Tanganyika linamaji mengi kwasababu kwanza lina outlet moja tu kule Zambia inayopeleka maji mto Congo, pili lina kina kirefu. Disadvantage ya ziwa ni uwepo wa samaki wachache nazani inachangiwa na uwepo wa species chache za samaki
Priority; priority; priority! Maendeleo ya vitu vs maendeleo ya watu.Mkuu acha tununue ndege kwanza,, ujue ndege ni muhimu sana kuliko kitu chochote,, wapinzania mlitusema sana enzi za jk,, tunahitaji ndege nyingi[emoji847][emoji847]
Duh mambo ya TW tutaweza kwa kutumia hydro na hata kama itawezekana uwekezaji wake ni mkubwa sana. Embu angalia kwenye hizi MW tu bado finance inasumbua!Nikiwa Rais kipaumbele changu miundo mbinu, maji, barabara umeme hospital shule reli, meli.
Kisha kilimo lazima kiwe cha kumwagilia,, kuhusu umeme tuzalishe Dekawatt 1000.. sio mambo ya MW 3000
Milima ya uluguru..morogoro.hivi chanzo cha mto ruvu ni wapi?
Kama hujawahi ishi kigoma huwezi elewa..ziwa Tanganyika halina maji chumvi, lina maji baridi
Ziwa Victoria sio letu peke yetu, Ila mbona maji yake ndio yanatumika mikoa ya Kanda ya ziwa?Kama Ziwa lingekuwa letu pekeyetu ingekuwa poa, lakini Burundi,Drc,Zambia nao wamo.
Kwahiyo wataka kusema lina maji chumvi mkuu?
Maji tunayotumia ni kidogo tu.Ziwa Victoria sio letu peke yetu, Ila mbona maji yake ndio yanatumika mikoa ya Kanda ya ziwa?
Sawa. Length ni umbali (urefu) toka kaskazini Burundi linakoanzia ziwa hadi kusini nchini Zambia, ni mbali sana! Angalia kwenye ramani.
Acha uvivu mkuu, tafuta taarifa kwa kusoma. Siku hizi kila kitu kinapatikana mtandaoni.Hizi takwimu umezitoa wapi?
Kwamba Maji ya mto ruvu yanatoka baharini kwenye lower level yanarudi nchi Kavu kwenye higher level?Sio Bahari ya Hindi kweli?.
Nilipata D ya Hisabati CSE.Vipi kuhusu mita za ujazo?
Cubic metres
Cubic feets
Centimeter cubic
Bila shaka hesabu zilikupiga chenga
Nilipata D ya Hisabati mtihani wa NECTA Kidato cha Nne. Baada ya hapo nikawa "Ngwini" 95%Kama cubic meter ipo basi cubic kilomita ipo pia.
Usikaze sana shingo kijana.
M^3 au Km^3.
Kama wenzetu wameweza jenga pipe la mafuta toka urusi mpaka germany, tunashindwa kujenga pipe la maji kupeleka mikoa ya pwani? Sometimes hatuhitaji misaada ya hela( hazitumiki ipasavyo, tungeomba msaada wa kujenga pipeDuniani ziwa Tanganyika ni la pili kwa ukubwa baada ya ziwa Baikal. Ziwa Baikal lina ujazo wa kilomita za ujazo 23,000 huku Tanganyika likiwa na 18,900. Nyasa lina 8,500 na Victoria lina 2,500. Ziwa Victoria linaingia kwenye ziwa Tanganyika karibu mara nane.
Ziwa Tanganyika lina asilimia 18.9 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia. Tanzania sisi tunamiliki 46% ya ziwa Tanganyika. Kwa maana hiyo, hilo linatufanya tumiliki asilimia kama 8.5 ya maji safi yote yaliyopo kwenye uso wa dunia. Ukijumlisha na sehwmu za ziwa Nyasa na Victoria utaweza kuta karibia asilimia 11 ya maji yote safi yaliyopo kwenye uso wa dunia yapo Tanzania.
Ukitoa maji yote kwenye ziwa Tanganyika halafu ukasema mito yote duniani itiririke kulijaza, itatumia karibia miezi saba kulijaza. Mto mkubwa wa Amazon utatumia karibu miaka mitatu. Mto Congo utatumia miaka 13.
Ukisema mto Rufiji utiririke kujaza Ziwa Tanganyika utatumia karibu miaka 1,400.
Hili ziwa peke yake linaweza kunywesha kila jiji Tanzania nzima. Na kila mtanzania. Ukipiga hesabu ya watanzania wote milioni 60 na ukipiga hesabu ya kuwa kila mtu, mtu mzima hadi mtoto mchanga anatumia lita mia moja kwa siku utaona kuwa tunahitaji kilomita za ujazo 2.2 kwa mwaka. Kinadharia, kwa idadi hiyo tunaweza kutumia maji ya ziwa hilo kwa miaka 8,500.
Asitokee mtu wa kutuambia tuna upungufu wa maji.