Jirani anaweza kukufanya uchukie nyumba yako

Mungu atakubariki kwa ku share rizki na malaika hao.
 
Kuna sehemu moja mtaa wa pili jamaa mmoja anafuga nguruwe harufu iliyopo pale hata ukiwa nyumba ya 5 kutoka kwake harufu inafika sasa sijui yule jirani wa karibu anaishije harufu mbaya kinoma mimi mpita njia tu sikuhizi nimebadili njia
Ila nyama yake unakula husikii hiyo harufu mshehe??
 
Dar Es Salaam inapoteza sifa ya mji unaofaa kuishi binadamu. Huu uholela sijui population ikifikia 10M itakuwaje . Tatizo la Dar wamejaa washamba, . Wanafanya mambo ya kishamba yanayofaa yafanyike huko vijijini kwa kisingizio cha kutafuta pesa. Huwezi kuyaona haya kama tangu uzaliwe hujawahi kuishi nchi zilizoendelea
 
Ndio hasara ya kuishi uswahilini
 
Mkuu nadhani kutoelezana ukweli na kukumbatia unafiki yaweza kuwa ndiyo utamaduni halisi wa Mtz.

Unonaje teka teka inayoendelea, chanzo chake si ni kuambizana tu ukweli.

Kwa hiyo kumbe mtu kumweleza ukweli ili aweze kurekebisha, yeye kichwani mwake anafasiri tofauti, yaweza kuwa ni elimu ama chuki.

Na kununa huko yaweza kuwa kapata sababu, donge lilikuwepo rohoni mwake siku nyingi kutokana na life style yako, huwezi jua.

Umefanya vizuri kuhangaika naye mapema, vinginevyo ungeishi maisha ya kero kwa faida zisizokuhusu.

Kila mtu aishi maisha yake bhana asikutishe na ndita zake.
 
Kwa vile tu mkuu hujaishi nchi nyengine lkn sisi ni wastaarabu mara 6 zaidi
Nikitaja mfano mmoja kati ya mingi niliyo nayo, nimekaa sehemu kadhaa Rwanda ustaarabu ni zaidi ya maelezo
 
Kesi kama hizo ni kupelekwa kwa mwenyekiti wa serikali za mtaa kutoa lalamiko....Kuna sehemu ilikuwa "KOTA" walitengewa sehemu ya kufuga na si kwenye makazi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…