Jirani anaweza kukufanya uchukie nyumba yako

Kuna Kiwanja kipo Masaki uza huko njoo ununue huku.
 
Kuna sehemu moja mtaa wa pili jamaa mmoja anafuga nguruwe harufu iliyopo pale hata ukiwa nyumba ya 5 kutoka kwake harufu inafika sasa sijui yule jirani wa karibu anaishije harufu mbaya kinoma mimi mpita njia tu sikuhizi nimebadili njia
hao majirani wameshazoea hata wewe ungeendelea kupita hapo pua yako ingekuwa ishazoea harufu za kishezi
 
Makanisa yanapiga kelele, kipindi nanunua kiwanja nilikuwa nakwepa makanisa, kuna kanisa likajengwa mbali na nnapo kaa ila wana mspika huo yaani kama vile wanafanyia ibada zao ndani kwangu.
 
Pole tatizo ni wewe, unajengaje kwenye kiwanja 20 kwa 20, huna maono ?! Hapo hata ukipata pesa ya kununua gari utapaki wapi au tajenga tena sehemu nyingine.


Binadamu ukishajenga nyumba ya kuishi Jenga kimoja then kula maisha na mishe mishe.


Ukitaka hewa safi tafuta viwanja vya gharama walau mikoani milion 3 unapata 30 times kiwanja unajenga na unaweka ukuta harufu ya mavi ya ng'ombe uipati kwa watu wa aina hii labda ukiingia jf.
 
Tatizo mikoani ukipata heart attack hata cardiologist hakuna. Tutabanana hapa hapa town.
 
ba
bado wauza supu ya Panya
 
Ndio maana mi nilinunua pori saa hivi nina aman.
 
Ulishawahi skia mtu anachimba shimo la taka tena kinyesi Cha nguruwe mpakani ambapo nyumba yako imetizamana na mpaka huo,na nyuma ya nyumba hakuna nafasi ni hapo mbele tu .
 
Yangenikuta hayo lakini uzuri kijijini ukishakuwa kwenye system basi wewe unaweza kuwa hakimu ,Askari ,mtendaji mda wowote basi jirani yeyote akileta ujinga namuhudumia perpendicular bila kucheka nao .

Sasa wananiogopa
Umekuwa kauzu🤣🤣
 
Mimi jirani yangu mlokole muda wa kulala wanangurumisha sala kwa sauti ya juu nimelalamika hadi kwa Mkuu wa Wilaya wapi imenibidi na mimi niokoke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…