Jitahidi sana mwanao asiwe na tabia hizi?

Jitahidi sana mwanao asiwe na tabia hizi?

mpe sifa za mtu anayetakiwa amtii,atagomea baba zake wadogo wamwone kimeo.

sio unamkataza tu hatakuelewa,mwambie awe anamfahamu anayemtuma,asimtume mbali asipopafahamu,asimtume jambo asiloliweza,na asisite kusema kwamba baba yake ulimkataza kabisa hayo hapo.

watoto hufata kwa usahihi waliyoelekezwa kwa utulivu na kuambiwa madhara yake wakikosea.
Noted
 
Isivyo bahati ni kwamba hizo ndizo tabia za watoto wengi... Mwanangu wa 2.5 anakosa namba 6 na 10 tu hapo
Umemaliza mkuu, bila unafki wala kuremba na huu ndio ukweli mchungu kwa baadhi ya wazazi
 
Watoto wa wapi hao?
Wanangu kulala mchana lazima
Wakitoka shule,wanakula,then wanalala lisaa limoja
Then wakiamka watacheza na wenzao lisaa limoja
Then watarudi ndani ya geti,kuoga na kufanya home work huku wakisubir msosi wa usiku,then wanapumzika nusu saa,saa 3 kamili usiku wako kwa bed wakiutafuta usingiz
Wikend ndo ratiba inabadilika
 
Kuna tabia flani mwanao akiwa nazo unayepata shida ni wewe mzazi

1. Mtoto kulilia kitu cha mgeni au chakula ulichowatengea wageni,

2. Akiwa anacheza na wenzake akiguswa tu kidogo kilio na machozi,

3. Kususa kitu kisa kimekatwa au kimepunguzwa mbele ya macho yake,

4. Mchana ukimwambia alale hataki,

5. Kukataa kuagizwa na mtu asiye mama au baba yake,

6. Kutukana watu,

7. Kusimama na kutazama watu wanaokula kitu na kuwataza akisubiria aitiwe

8. Ukimchapa na kumwambia anyamaze hanyamazi anaongeza kulia

9. Ukimtuma anaenda mazima,

10. Jitahidi mwanao asipende kushika vitu vya watu bila ya kupewa na mhusika hasa simu,

Haya ni baadhi tu yapo mengi ya kuzingatia katika malezi

Mtoto umleavyo ni mzigo wako na mateso yako mwenyewe ya baadae
Wangu hizo pigo zote hana ila kulala mchana labda awe anaunwa na ikitokea amelala basi usiku hapati usingizi
 
Kwa kweli ni mtihani Mkuu, naamini kila mzazi anatamani/kupenda watoto wenye tabia nzuri ila wengine kwa kweli ni wa kuwaombea mie mpaka nakuwa na fikra kuwa wanangu wananiogopa mie tu maana nikiwepo naona wanabehave vizuri tu, ila nisipokuwepo mpaka najiuliza hivi nakosea wapi?
 
Mambo yamebadilika .!!

Sisi enzi hata kama mgenj anakula ukawa unajipitisha utajuta mgeni akitoka.
1694636352278.jpg
 
Kuna tabia flani mwanao akiwa nazo unayepata shida ni wewe mzazi

1. Mtoto kulilia kitu cha mgeni au chakula ulichowatengea wageni,

2. Akiwa anacheza na wenzake akiguswa tu kidogo kilio na machozi,

3. Kususa kitu kisa kimekatwa au kimepunguzwa mbele ya macho yake,

4. Mchana ukimwambia alale hataki,

5. Kukataa kuagizwa na mtu asiye mama au baba yake,

6. Kutukana watu,

7. Kusimama na kutazama watu wanaokula kitu na kuwataza akisubiria aitiwe

8. Ukimchapa na kumwambia anyamaze hanyamazi anaongeza kulia

9. Ukimtuma anaenda mazima,

10. Jitahidi mwanao asipende kushika vitu vya watu bila ya kupewa na mhusika hasa simu,

Haya ni baadhi tu yapo mengi ya kuzingatia katika malezi

Mtoto umleavyo ni mzigo wako na mateso yako mwenyewe ya baadae
Hili ni picha la uswazi tupu.
 
Namba 8 ni dalili ya kiburi..

Mtoto ukimuadhibu anapaswa kuomba msamaha,akimaanisha kuwa anajutia alichofanya.

Kulia zaidi maana yake anaonesha kuwa alochofanya ni sahihi na kuadhibiwa ni kuwa anaonewa
 
Kuna tabia flani mwanao akiwa nazo unayepata shida ni wewe mzazi

1. Mtoto kulilia kitu cha mgeni au chakula ulichowatengea wageni,

2. Akiwa anacheza na wenzake akiguswa tu kidogo kilio na machozi,

3. Kususa kitu kisa kimekatwa au kimepunguzwa mbele ya macho yake,

4. Mchana ukimwambia alale hataki,

5. Kukataa kuagizwa na mtu asiye mama au baba yake,

6. Kutukana watu,

7. Kusimama na kutazama watu wanaokula kitu na kuwataza akisubiria aitiwe

8. Ukimchapa na kumwambia anyamaze hanyamazi anaongeza kulia

9. Ukimtuma anaenda mazima,

10. Jitahidi mwanao asipende kushika vitu vya watu bila ya kupewa na mhusika hasa simu,

Haya ni baadhi tu yapo mengi ya kuzingatia katika malezi

Mtoto umleavyo ni mzigo wako na mateso yako mwenyewe ya baadae
Nambw 5 sikubaliani na wewe mtoto wangu sio punda wa kutumwa hovyo kila mahali aende, pia kwa USALAMA wake ni hatari
 
Mtoto ukimchampa sio kazi yako kumapngia alie au asilie.

Utotoni mwangu sijawahi kupewa utaratibu wa kulala mchana lakini wenzangu walikuwa wanalala mchana hakuna kitu waliizd kwanzia ujanja mpaka akili shulen na hata wao walikuwa hawapendi kulala mchana.

Kwa kifupi kuna vitu umeandika ni nonsense.
Shida sio kulia,
Analia kwa style ipi?

Ukimwambia nyamaza ananyamaza?
 
Ni ngumu kukuta mtoto hana hizo tabia zote. Mfano huyu mwanangu mdogo ukimchapa hanyamzi haraka, akilia sana akiona huna time nae anakuomba kabisa umbembeleze("mama nibembeleze basi")
Kulala mchana hawapendi ila nawalazimisha. Mtu mzima ukila mbele ya mtoto bila kumpa ni lazima atakuangalia tu, akiona humpi atakuomba. (Hili halitokei stendi ni mazingira ya nyumbani.)Manake ikiwa mbali na nyumbani ndo ngumu mtoto kuomba.
 
Hapo kwenye kutumwa na Kila mtu hapana Kwa kweli. Sitaki mtu amtume mtoto wangu now a days Dunia imebadilika sana . Nimewahi kushuhudia mtoto akibebeshwa bhangi​
Nakazia.

Au mtu anamtuma mtoto wako sigara . Anamtuma usiku au barabarani
 
Back
Top Bottom