Jitahidi sana mwanao asiwe na tabia hizi?

Noted
 
Isivyo bahati ni kwamba hizo ndizo tabia za watoto wengi... Mwanangu wa 2.5 anakosa namba 6 na 10 tu hapo
Umemaliza mkuu, bila unafki wala kuremba na huu ndio ukweli mchungu kwa baadhi ya wazazi
 
Watoto wa wapi hao?
Wanangu kulala mchana lazima
Wakitoka shule,wanakula,then wanalala lisaa limoja
Then wakiamka watacheza na wenzao lisaa limoja
Then watarudi ndani ya geti,kuoga na kufanya home work huku wakisubir msosi wa usiku,then wanapumzika nusu saa,saa 3 kamili usiku wako kwa bed wakiutafuta usingiz
Wikend ndo ratiba inabadilika
 
Wangu hizo pigo zote hana ila kulala mchana labda awe anaunwa na ikitokea amelala basi usiku hapati usingizi
 
Kwa kweli ni mtihani Mkuu, naamini kila mzazi anatamani/kupenda watoto wenye tabia nzuri ila wengine kwa kweli ni wa kuwaombea mie mpaka nakuwa na fikra kuwa wanangu wananiogopa mie tu maana nikiwepo naona wanabehave vizuri tu, ila nisipokuwepo mpaka najiuliza hivi nakosea wapi?
 
Hili ni picha la uswazi tupu.
 
Namba 8 ni dalili ya kiburi..

Mtoto ukimuadhibu anapaswa kuomba msamaha,akimaanisha kuwa anajutia alichofanya.

Kulia zaidi maana yake anaonesha kuwa alochofanya ni sahihi na kuadhibiwa ni kuwa anaonewa
 
Nambw 5 sikubaliani na wewe mtoto wangu sio punda wa kutumwa hovyo kila mahali aende, pia kwa USALAMA wake ni hatari
 
Shida sio kulia,
Analia kwa style ipi?

Ukimwambia nyamaza ananyamaza?
 
Ni ngumu kukuta mtoto hana hizo tabia zote. Mfano huyu mwanangu mdogo ukimchapa hanyamzi haraka, akilia sana akiona huna time nae anakuomba kabisa umbembeleze("mama nibembeleze basi")
Kulala mchana hawapendi ila nawalazimisha. Mtu mzima ukila mbele ya mtoto bila kumpa ni lazima atakuangalia tu, akiona humpi atakuomba. (Hili halitokei stendi ni mazingira ya nyumbani.)Manake ikiwa mbali na nyumbani ndo ngumu mtoto kuomba.
 
Hapo kwenye kutumwa na Kila mtu hapana Kwa kweli. Sitaki mtu amtume mtoto wangu now a days Dunia imebadilika sana . Nimewahi kushuhudia mtoto akibebeshwa bhangi​
Nakazia.

Au mtu anamtuma mtoto wako sigara . Anamtuma usiku au barabarani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…