Hii ni dawa safi sana,kwetu tunauita mkingili(ikingili) ukiacha magonjwa madogomadogo mengi ambayo mmea huu huweza kutibu kwa mafanikio makubwa nilipata jingine kwa rafiki yangu muhindi,yeye kwake ameyapanda kila sehemu kuzunguka ua wake.
Nikamuuliza kwa nini ameyaweka mengi kuliko maua mengine mazuri? Yeye akanijibu kuwa kwanza ni tiba ya magonjwa mbalimbali,lakini zaidi huwa anayatumia kiimani zaidi, anasema ukiwa na mimea hiyo nyumbani kwako basi watu wenye macho mabaya(ya husda) ambayo huleta madhara kwa watu na vitu hudhibitiwa barabara.
Anasema hata kama mchawi akija kwako kwa lengo baya basi mmea huu humfanya ashindwe kutimiza lengo lake,wachina pia wanauheshimu sana mmea huu kwa sababu kama hizo hizo, wao pia hudai kuwa mmea huu ukiupanda nyumbani huleta bahati njema, wahindi wa jamii ya ki hindu huchuma majani yake na kuyafunga pamoja na majani ya mwembe na kuyatundika mlangoni kama kinga dhidi ya wote wanaoingia ndani ya nyumba zao, hasa siku za sherehe au shughuli zinazokutanisha watu wengi,asante