Jitizame kama umerogwa ukiwa nyumbani kwako

Jitizame kama umerogwa ukiwa nyumbani kwako

Kuna siku niliota mbwa wawili wakubwa Sana ambao kupitia ndoto hao waliokuwa na cheo Cha kikomandooo na walikuwa wakinilinda wote wawili na ilipofika muda mbwa mweusi aliitwa kwenda kwenye kikao Chao Basi akaniongoza nikamsindikiza Hadi kwenye chumba Chao Cha kikao ambacho kulikuwa na Wakubwa wao ambao Ni makomandoo wa kibinadamu lakini Yule Mweupe alibaki nje akinisubiria nilipotoka ndani huyu aliyekuwa nje akanisindikiza Hadi alipoona nimefika mahala ambapo siwezi kupotea akarudi.. na nilipita eneo ambako kulikuwa na soko na butcher za nyama za Ng'ombe..

Nini Maana yake

Niletee hizi ndoto inbox hapa tunachafua
 
Ya jamaa aliesema ukichukua mkaa..majani ya mbaazi na kipande Cha mti wake ukafunga pamoja unaona wachawi...hi nimejaribu na haijafanya kazi...yako next week ntakuja na majibu
Mi' napenda sana mambo ya mauzauza, lakini siyaoni. Nimejaribu kutembea usiku wa manane peke yangu sioni kitu, nimeenda mpaka makaburini usiku wa manane nayo bilabila.
Hiyo ya majani na matawi ya mbaazi kama wewe mpemba imebuma kwako, generally, labda inabuma.
Wanaojua kiuhakika jinsi ya kuona wachawi, majini na viumbe vya ajabu watuwekee hapa, na sisi tuuone ulimwengu wa pili
 
Ni upumbavu tuu sayansi iwakomboe waafrika na huu utopolo wa nguvu za kichawi
 
Yaani unayaita live kwenye river wa kulalia 😂😂😂
Nalog off
 
Kwangu hiyo kusaga mkaa, kuuchanganya na ubani kisha niulalie Alhamis ndio kitu cha ajabu.

Mkaa unawasha moto gani? Kwanini iwe siku ya Alhamis na sio siku yeyote? Majini wazuri??? Siwataki kuanzia wazuri hadi wabaya.

Kama hadi hapa nilipo sijawahi fanya hizo mambo na naendelea vizuri, siwezi kabisa hata kujaribu, achilia mbali kuwaza.

Naamini nilizaliwa siku moja, ntakufa siku moja pia, mlinzi wangu ni Mungu Muumba mbingu na vyote viijazavyo dunia.
Wewe ndio maana halisi ya jamii......
wote hatuwezi kuwa na akili moja
 
Kwangu hiyo kusaga mkaa, kuuchanganya na ubani kisha niulalie Alhamis ndio kitu cha ajabu.

Mkaa unawasha moto gani? Kwanini iwe siku ya Alhamis na sio siku yeyote? Majini wazuri??? Siwataki kuanzia wazuri hadi wabaya.

Kama hadi hapa nilipo sijawahi fanya hizo mambo na naendelea vizuri, siwezi kabisa hata kujaribu, achilia mbali kuwaza.

Naamini nilizaliwa siku moja, ntakufa siku moja pia, mlinzi wangu ni Mungu Muumba mbingu na vyote viijazavyo dunia.
Na nasikia mkaa uwekwa kunako mbumbusu ya maiti demu wa kikatoriki kama kakata moto bila ya kupata mtoto!.
 
Sijakataa ila uchawi upo na watu hasa watu wa karibu wanatumia uchawi kuwaharibia wenzao na nimeandika tu kama umerogwa utaona kama hujarogwa huobi kitu its simple
True mwafrika utumia uchawi kama burudani wenzetu utumia uchawi kutatua changamoto za maendeleo
 
Habari wanajamii,

Napenda kuchukua fursa hii kuwapa darasa huru jinsi ya kujiangalia mwenyewe kama umerogwa.

1. Chukua mkaa usagesage uwe kama unga changanya na ubani wowote uusage vizuri kisha ufunge kwenye karatasi na uuweke kwenye mto wako unaolalia.

2. Usiku wa kuamkia alkhamis weka dawa yako na uulalie utakutana na ndoto zako zote zinazohusiano na uchawi kama aliekuroga umerogwaje wapi vitajionesha.

Asanteni sana
Kwetu mkaa utumika pia kwa mtoto mchanga (mdogo)kumuwekea chini ya mchago kama anakuwa anastukastuka usiku na kulia na hali huwa shwari.
 
Nakubaliana na wewe ila mimi natumia uchawi kuzuia wanaodhuriwa na uchawi na natumia uchawi kuwarahisishia waliokua na magumu bila ya kumuasi mungu uchawi ni zawadi ndugu ha ha ha
Mungu na shirki ni wapi na wapi
 
Mimi nimeweka nimeota mambo ya chakula chakula tu.....yani tupo sehemu tunakula ila mimi napewa kipaumbele kwenye hiko chakula...mkuu kwamba ndo narogwa kupitia chakula ama???? [emoji15][emoji15][emoji15][emoji134][emoji134][emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
 
Na nasikia mkaa uwekwa kunako mbumbusu ya maiti demu wa kikatoriki kama kakata moto bila ya kupata mtoto!.

Mh! Kwamba asizae hata huko anakoenda kwenye maisha mapya au walaaniwe walioingiza chululu hapo hazikuzaa matunda
 
Pia nimeota tupo sehemu kuna muziki dj anapiga muziki na waliomzunguka ni wadada wengiiiiiiiii wanachezacheza hapo.. nakwendakwenda pale kwa dj...mimi nimekaa pembeni sichezi badae dj alivomaliza na kufunga muziki akaandika ki note na kuniachia mkononi yeye akaondoka ndani yake kukiwa na note ya tsh elfu 10 wale wadada walikua wanashangaa sana ???? Nini maana yake??
 
Mimi nimeweka nimeota mambo ya chakula chakula tu.....yani tupo sehemu tunakula ila mimi napewa kipaumbele kwenye hiko chakula...mkuu kwamba ndo narogwa kupitia chakula ama???? [emoji15][emoji15][emoji15][emoji134][emoji134][emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]

Huna anaekuroga ndugu, kwa ndoto ulioota kuna mambo mazuri yanakuja siku zijazo zidisha maombi
 
Pia nimeota tupo sehemu kuna muziki dj anapiga muziki na waliomzunguka ni wadada wengiiiiiiiii wanachezacheza hapo.. nakwendakwenda pale kwa dj...mimi nimekaa pembeni sichezi badae dj alivomaliza na kufunga muziki akaandika ki note na kuniachia mkononi yeye akaondoka ndani yake kukiwa na note ya tsh elfu 10 wale wadada walikua wanashangaa sana ???? Nini maana yake??

Zote zinaashiria mambo mazuri yanakuja, sio mambo madogo ila mambo ya pesa
 
Back
Top Bottom