Lakini pia tuelewe kuwa, ikiundwa tume na ikapewa hadidu za rejea makini za kufuata kufukunyua uozo huu, hata mkuu wa majeshi mwenyewe anahusika moja kwa moja kwenye kadhia hiyo.
Ipo hivii?
Amiri jeshi ambaye ndiyo rais anapotoa tamko, kwa mfano wa kutoa ajira kwa hao vijana kama motisha kwa kazi maridhawa za kujitolea walizofanya, basi hilo agizo hugeuka na kuwa ni amri ya utekelezaji wa moja kwa moja na inakuwa ni haki kwa walengwa.
Sasa tangu Marehemu Maguli atoe tamko hilo umepita muda mrefu bila ya utekelezaji, je ni nani aliyekwamisha mchakato huo?
Je hao vijana walielezwa kilichochelewesha ajira zao ama kama wao wavyosema 'kuandikishwa'?
Tena nimekuja kushangaa kusikia bado walikuwa hawajapewa haki yao hiyo ya ahadi kama ilivyotamkwa na Amiri jeshi!
Ninadhani hii kadhia inajirudia rudia.
Kama sikosei, kama si mwaka jana basi itakuwa ni mwaka juzi, kuna wengine waliahidiwa hivyo hivyo, nadhani waliojenga ukuta ama kazi zinazofanana na hizo, lakini walirejeshwa makwao na tukasikia kwenye vyombo vya habari mkuu wa majeshi akiwatangazia vijana hao warejee makambi ya Jwtz na kuandikishwa jeshi ili kutekeleza agizo la rais.
Sasa tujiulize, ni nani huyo kati kati anayekuwa ni kisiki cha utetekezaji wa amri za rais na amiri jeshi mkuu?
Tume makini ikiundwa, lazima mnyororo wa uozo utajulikana na kuwekwa wazi.
Wenye makosa ya kiuwajibikaji huenda wakawa ni wengi sana kuliko hao vijana zaidi ya 800 waliowatoa kafara na viongozi kubaki wamekalia viti vyao bila ya kuwajibishwa.