JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

Jeshini sikutaka kwenda japo nilipata nafasi kwasababu ya kusema ndiyo kila kitu hata kama unaonewa.....ndiyo afande, ndiyo afande.........hawa madogo nadhani hawakujua kuwa Utii Jeshini ndiyo jambo la kwanza
 
Kweli mkuu jeshini utii Ndo swala la kwanza
 
.nakumbuka kipindi namaliza kidato cha nne nilikosa post za kwenda advance kwasababu combination nilizoandika kwenye ile karatasi sikubalance
.nikakaa home nikiwa nasubiria hatma yangu kama ni kwenda chuo ama advance private, ila home kukawa hakuna helaa hivo nikawa mpole tuu..
.sasa katika harakati za hapa na pale nikahamia mkoa mwingine kwa ndugu yangu nilikuwa napiga graphics design hatar..nikakutana na mbunge wa eneo hilo akanipa kazi nimtengenezee majarida yakionrmesha miradi aliyokamilisha
Nilifanya kazi kwa ufanisi mkubw akatokea kuwa rafiki yangu sana...siku nikamwambia hali yangu ya maisha yalivyo akaniambia dogo ondoa shaka nitakuingiza jeshini...tukaendelea na mishe mishe mwezi wa 6 nakumbuka akanipigia simu nimtumie matokeo yangu nikamtumia akasema unachet cha kuzaliwa nkamwambia ninacho akasema jiandae utapigiwa simu muda wowote kuripot kambi fulani...
.ila muda huo kazi za jeshini zilinitoka moyoni nilikuwa nazichukia sana...nilikuwa nataka maisha ya uhuru nifanye mitikasi yangu ya biashara..huwezi amini nilireject iyo ishu...
.kuna jamaa nilikuwa nakaa nae huo mkoa nilioenda nayeye pia alifanyiwa huo mpango ilibidi tuwe wawili..baada ya mwaka mmoja nilisikia amehamishiwa kambi ya ruvu akitokea kambi nyingine sijui alikuwa kishaajiriwa...
 
🙏🙏🙏 Huenda alibahatika kupata nafasi sehemu
 
Sitoshangaa siku nikisikia hao vijana wote waliondamana hawajarudishwa kwao ila wapo jela ya siri au wameshapotezwa kabisa. Hakuna nchi yoyote inayojifahamu iwaache tuu watu ambao wanasema wamefanya uasi warudi nyumbani. Uasi au mutiny ni kosa kubwa sana popote pale duniani.
 
Kifupi hao sio watanzania ni raia wa nje waliojipenyeza JKT

Watanzania huogopa jeshi sana wasingefanya huo ujeuri asante CDF message sent.Waelewe Tanzania ni ya watanzania.Wote wakamatwe na wahojojiwe uraia wao barabara
Kwa hiyo JKT ina train watu wasio Watanzania na kuwaahidi ajira? Asee hebu acha kulidhalilisha Jeshi ukifikiri kwamba unalitetea
 
Mkuu hapo chini nimeona umelitaja jeshi letu pendwa la TanPol,tujuze linahusikaje hapo kwenye mada.
 
Kuna kitabu cha amri ukimaliza phase one unapewa. Kile ndicho hukupa kujua amri halali na zisizo halali. Sio kila jambo ni kutii tu, huo utakuwa undezi.

Vijana wakae JKT miaka 5 wafanye kazi kama punda kazi imeisha unashindwa kuwaajiri kama alivyosema Magufuli unawapa kazi nyingine.
 
Mimi nimeshangaa sana vijana hao kujipanga kufanya maandamano bila intelijensia ya jeshi kuwabaini mapema na kuwadhibiti.Hivi jeshi letu siku hizo likoje?
Lakini pia tuelewe kuwa, ikiundwa tume na ikapewa hadidu za rejea makini za kufuata kufukunyua uozo huu, hata mkuu wa majeshi mwenyewe anahusika moja kwa moja kwenye kadhia hiyo.

Ipo hivii?

Amiri jeshi ambaye ndiyo rais anapotoa tamko, kwa mfano wa kutoa ajira kwa hao vijana kama motisha kwa kazi maridhawa za kujitolea walizofanya, basi hilo agizo hugeuka na kuwa ni amri ya utekelezaji wa moja kwa moja na inakuwa ni haki kwa walengwa.

Sasa tangu Marehemu Maguli atoe tamko hilo umepita muda mrefu bila ya utekelezaji, je ni nani aliyekwamisha mchakato huo?

Je hao vijana walielezwa kilichochelewesha ajira zao ama kama wao wavyosema 'kuandikishwa'?

Tena nimekuja kushangaa kusikia bado walikuwa hawajapewa haki yao hiyo ya ahadi kama ilivyotamkwa na Amiri jeshi!

Ninadhani hii kadhia inajirudia rudia.

Kama sikosei, kama si mwaka jana basi itakuwa ni mwaka juzi, kuna wengine waliahidiwa hivyo hivyo, nadhani waliojenga ukuta ama kazi zinazofanana na hizo, lakini walirejeshwa makwao na tukasikia kwenye vyombo vya habari mkuu wa majeshi akiwatangazia vijana hao warejee makambi ya Jwtz na kuandikishwa jeshi ili kutekeleza agizo la rais.

Sasa tujiulize, ni nani huyo kati kati anayekuwa ni kisiki cha utetekezaji wa amri za rais na amiri jeshi mkuu?

Tume makini ikiundwa, lazima mnyororo wa uozo utajulikana na kuwekwa wazi.

Wenye makosa ya kiuwajibikaji huenda wakawa ni wengi sana kuliko hao vijana zaidi ya 800 waliowatoa kafara na viongozi kubaki wamekalia viti vyao bila ya kuwajibishwa.
 
Narudi tena kwenye uzi huu.

Kuhusu hao vijana 854 waliositishiwa mikataba na JKT, nakubaliana na uamuzi ulichukuliwa. Kwa sababu, kitendo kilichofanywa na vijana hao hakikidhi matakwa ya JKT na dhana nzima ya ulinzi na usalama wa Taifa letu Tanzania.

Hata hivyo, hao vijana ni watanzania, na walikuwa hawajaingia sawasawa kwenye utumishi wa kijeshi ndiyo maana sheria za kijeshi hazikutumika kuwaadhibu. Kwa hiyo, wameonywa/adhibiwa 'kiraia'. Kwa kuwa wanahadhi ya kiraia basi tutumie utaratibu wa kiraia kuwaasa na sasa warudi kuwa raia wema kiasi cha kuaminiwa tena kulitumikia Taifa la Tanzania kwa ujuzi walionao. Katika kuaminiwa huku, nashauri wasiaminiwe kurudi kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa sasa na hata baadaye kidogo.

Binafsi, ili vijana hawa waweze kuaminiwa tena kwa sisi raia wenzao na viongozi wa taifa hili wa sasa na wajao, nawashauri waombe radhi rasmi tena hadharani kwa kitendo chao kisichokubalika kutokana na sehemu walipokuwa wana'fundwa'/mentored. Pia waahidi kwa maadishi mbele ya wanasheria wa viapo kuwa hawatarudia kitendo hicho cha kufedhehesha vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na Tanzania kwa ujumla.

Wakifanya hivyo, viongozi wa taifa hili wapokee maombi yao ya kuomba radhi na wawasamehe huku wakiwapa angalizo kuwa kuanzia sasa watakuwa wanafuatiliwa nyendo zao. Na haya yote mawili yatekelezwe kwa vitendo.

Yangu ni hayo.
 
Back
Top Bottom