JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

Mtaji wa CCM ni wajinga. Hao vijana walikua wajinga ndio CCM wakawatumia
 
Mimi nilidhani aanze kuwajibishwa aliyekuwa anawafanyia 'mentorship' vijana hawa. Pia uchunguzi yakinifu ufanyike ni kwa namna gani vijana hawa waliweza kufanikiwa kufanya kitendo hiki ambacho akikubaliki kwa vipimo vya aina yoyote! Matokeo ya uchunguzi si lazima watupatie sisi raia, lakini hatua zichukuliwe kitendo hiki kisijirudie tena.
 
Watu wengine hamna huruma kabisa.Ila siku yakiwakuta ndio ,mtaombwa muhurumiwe.
Mwanajeshi haandamani Boss hata iweje kuna chain of command anatakiwa aifate kama hajatendewa haki sio maandamano HAIPO HIYO DUNIA NZIMA
 
1 mpaka 800 ni wachache? Jipeni matumaini ila muda huo ni lazima tuwe makini
Kwani wanaenda kukaa sehemu moja? Hao wanaenda vijijini kwao. I have been in it Tanzania ina control sana silaha so ukishatemwa kwenye system jiandae kuwa mtu wa kawaida.
 
Yaani wameshindwa kabisa kukaa nao chini wakamalizana hadi wawafukuze? Kwahio tuna jeshi bado linalotumia nguvu zaidi kuliko akili zaidi. Kwa babahti mbaya sana hata wakiwahoji hawataweza kuandika chochote, hatuna waandishi wenye uthubutu huo
Mtu anaweza kugoma jeshini hafai mwanajeshi hagomi
JKT wanapewa sehemu ndogo sana ya mafunzo ya kijeshi ndiomaana hata wale wanaopata bahati ya kuajiliwa jeshini lazima waende mafunzo tena

Kumbuka wale vijana waliokufa wakati wa mafunzo pale pwani mwaka Jana tukaambiwa walikula vyakula vyenye sumu mtaani....wale ni miongoni mwa wale vijana wa JKT waliojenga ukuta wa mererani
Walikula chakula chenye sumu au walifia kwenye kozi wajenzi wanavumbi sana kifuani ndio mana wanawakwepa... wanawatumia kwenye ujenzi wanawaharibu baadae wanawaita UNFIT
 
Shida kubwa wengine wanaongea bila kuangalia uhalisia wa mambo na hawajui kinachoendelea kisa uongo uongo adi jeshini. Makosa ya namna ya kuajiri vijana toka jkt ilianza baada ya uongozi wa awamu ya tano kuingia.
Vijana wanapmaliza mafunzo ya miezi sita ya awali walikua wanatawanyishwa kwenye makambi mbalimbali yaliyopo chini ya jwtz kwa ajili ya uzalishaji mali na ulinzi kama sehemu ya malezi.

Wakiwa kwenye makambi ya malezi ndipo jeshi..magereza..usalama..bot..takukuru n.k wanakwenda kufanya recruitment wa vijana hawa kulingana na sifa wanazohitaji pindi wakiwa na uhitaji na kwa kwenda kwenye makambi yote ya malezi.

Shida ikaanzia kipindi cha magufuli; yeye alitoa amri wa kuajiriwa waliojenga Ukuta Marerani lakini waliokua wanalima mpunga Chita..wanaolinda mipaka huko Kigoma na Uganda na Rwanda hakuona kama wanasifa ya kuajiriwa..waliokua wanalima mahindi huko Mgambo Tanga hakuona kama wanastahili kuajiriwa sijui alifikiri wote waje Mererani kujenga ukuta bila kuwepo mgawanyo wa ki majukumu.
CDF na mkuu wa jkt wakajikalia kimya bila kuona kuna upendeleo kwenye ajira.

Watu wenye uwezo wakawapanyika vijana wao humo humo na ikawa rushwa ndani ya jeshi.
Ujenzi ulipoanza tena Chamwino stori ikawa ile ile waajiriwe wanaojenga ukuta..hao CDF na mkuu wa jkt wakawa kimya tu; vijana waliopo makambi ya mbali wakawa na vilio mbona wanaajiriwa wa Dodoma tu? then wenye michongo wakafanya wanavyojua vijana wao wakaja nao Dodoma kwenye ujenzi.

Uchaguzi ulipowadia pia wanachukuliwa vijana kwenda kuaribu uchaguzi kwa upendeleo huohuo kua wataajiriwa.

Sasa leo wanawaona kama wanaketa uasi. Swali ni je kwanini hawakushauri Magufuli kipindi hicho kuhusu ajira? wamwambie kua wao wanataratibu zao za kuwapatia vijana wa jkt ajira?
Mambo ni mengi ngoja niishie hapa.
Asante sana mkuu
 
Vijana wa JKT wapo wengi tu street na kijana aliyeiva ataheshimu kiapo chake kwa nchi.
 
Sawa kwanini waandamane kwan waliambiwa wanardishwa makwao ???
Kama Kurudishwa wangerudishwa wote 2400 mmechagua watoto wa maskin hao 800 mnawaita waasi hao watoto wa wakubwa ndio mmeona wanafaa haya bwana mtaji wa maskin
 
Buku hamsini kwa mwezi malipo yao...
Haha na ndiyo vijana wa mataga hao walitumika pia kwenye hujuma za uchaguzi wa october.

Tutarajie roba za mbao zitachachamaa huko mitaani watu 800 wenye mafunzo ya kutumia silaha wametupwa mtaani.
 
Haha na ndiyo vijana wa mataga hao walitumika pia kwenye hujuma za uchaguzi wa october.

Tutarajie roba za mbao zitachachamaa huko mitaani watu 800 wametupwa mtaani.
Enzi hizo nimeenda kwa mujibu nikashangaa kuona malipo yao 50K dadekiii[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Yani daah hapana aisee mimi ile 50K walikuwa wakitupa kama posho ilikuwa inaisha ndani ya siku 2 kwa kula biskut na chapati..Ngurutu mdudu njaa muda wote
 
Kuna wakati gharama haiangaliwi, hasa linapokuja swala la majeshi au tuseme ulinzi na usalama. Hao vijana hawatoshi kuwa askari kwa gharama yoyote ile.

Tanzania si mara ya kwanza, Nyerere aliivunja TAR na kuwaamuru maafsa na askari wao wote kuvaa nguo za kiraia na kwenda nyumbani. Hapo hapo akaunda jeshi jipya la TPDF ya Sasa. Askari unamgomea afande Brigadier General? Kweli? Waache wavune walicho panda.
 
Akipiga Pini hizo bidhaa za China, wewe utatazizalisha na kukidhi mahitaji sokoni? Sukari tu ya Kilombero na Mtibwa imetushinda kushusha Bei, alizeti tu mafuta yake hayashikiki fikiria tena
Hizo ni hujuma, wakulima wakipeleka miwa kiwandani wanaambiwa mibovu haifai, kumbe miwa imewazidia na hawataki kuongeza mashine ilihali mahitaji yapo, sasa kama sio hujuma hiyo ni nini? Tukomeshe hizi hujuma
 
Back
Top Bottom