TANZIA GE2025 Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Am paining, my heart is bleeding, crying for my people.

Sleep calmnly Mkuu ulikuwa na idea ya nchi kujitegemea nakumbuka kikao chako cha mwisho kilichokuletea mitikisiko ya nywele hadi nyayo za Miguu.
 
Pole kwa wafiwa na wote walioguswa na msiba

Rest well Job
 
Aliyewahi kuwa Spika na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia, leo Agosti 6, 2025, taarifa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson imeeleza kuwa msiba umetokea Dodoma

Dkt. Tulia amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

WASIFU MDOGO WA JOB NDUGAI
Alizaliwa Januari 21, 1963 na kupata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.

Amesoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).

Amesoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).

Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008)

Amekuwa Mbunge wa Kongwa kwa miaka 25 sasa (tangu mwaka 2000) na ameshika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.

Alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.

Katika uongozi wake wa bunge, mambo kadhaa yameibua mjadala mkubwa ikiwemo sakata la wabunge 19 wa CHADEMA wanaodaiwa kuvuliwa uanachama wao, na kuhojiwa kwa baadhi ya wabunge akiwemo Josephat Gwajima na Jerry Muro kwa madai ya kushusha hadhi na heshima ya bunge.

Suala jingine ni kumtaka mmoja wa wabunge aliyedai amevaa nguo zisizo za staha kutoka ndani ya ukumbi wa bunge. Uamuzi huo ulikosolewa vikali, wakosoaji wakieleza kwamba vazi la mbunge huyo halikuwa na tatizo. Karibuni, amezua mjadala tena kwa kusema Tanzania haitakiwi kukopa ili kufadhili miradi ya maendeleo.

Mbali na ubunge, amefanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Januari 6, 2022 amejiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.

Ndugai ni mume wa Fatuma Mganga.
Tusihuzunike "Kifo ni kifo".
 
Kuna uwezekano mkubwa Lissu akatolewa wiki ijayo maana kifo hiki kitakuwa kimewapa wengi funzo na somo.
Nao watakuwa waoga Kwa kuogopa yajayo na hivyo kuona umuhimu wa kumuachia huru
 
No hakuna inawezekana yeye Samia ndiyo kamuua msela. Ingekuwa onyo basi mkwe wake mtoto wake wangetuma ujumbe
Kwanini "walimruhusu" ashinde kura za wajumbe ikiwa wana mkakati wa kummaliza?

Ilikuwa ni mojawapo ya mbinu? kummaliza katika mchakato?

Kuna muunganiko gani kati ya mchakato wa kampeni na mauaji yake?

Na kwanini alikubali "kushindishwa" kura? Hakutambua hatari ya kushindishwa na wabaya wake?

Au "waliomshindisha" ni watu tofauti na mahasimu wake? inawezekana?

Au alikuwa na malengo gani? Au alikosea kusoma drafti?

Au ni kifo cha kawaida? au ni ujumbe? Au? Au? Au aliridhia? Au? Au? Au?

Au wauaji wana malengo ya kupindisha maoni ya watu kuhusu chanzo cha kifo chake? Kwa kuuonesha umma kwamba ameuwawa na wabaya wake? Kumbe sivyo?
 
Aliyewahi kuwa Spika na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia, leo Agosti 6, 2025, taarifa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson imeeleza kuwa msiba umetokea Dodoma

Dkt. Tulia amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

WASIFU MDOGO WA JOB NDUGAI
Alizaliwa Januari 21, 1963 na kupata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.

Amesoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).

Amesoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).

Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008)

Amekuwa Mbunge wa Kongwa kwa miaka 25 sasa (tangu mwaka 2000) na ameshika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.

Alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.

Katika uongozi wake wa bunge, mambo kadhaa yameibua mjadala mkubwa ikiwemo sakata la wabunge 19 wa CHADEMA wanaodaiwa kuvuliwa uanachama wao, na kuhojiwa kwa baadhi ya wabunge akiwemo Josephat Gwajima na Jerry Muro kwa madai ya kushusha hadhi na heshima ya bunge.

Suala jingine ni kumtaka mmoja wa wabunge aliyedai amevaa nguo zisizo za staha kutoka ndani ya ukumbi wa bunge. Uamuzi huo ulikosolewa vikali, wakosoaji wakieleza kwamba vazi la mbunge huyo halikuwa na tatizo. Karibuni, amezua mjadala tena kwa kusema Tanzania haitakiwi kukopa ili kufadhili miradi ya maendeleo.

Mbali na ubunge, amefanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Januari 6, 2022 amejiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.

Ndugai ni mume wa Fatuma Mganga.
Baba NDUGAI msalimie JPM mwambie Wana mtandao wanafanya Yao.
 
Kwa wale waliongalia movie ya apocalypto ndo kama haya yanayoendelea Sasa Kati ya chadema na CCM
 
Msipokuwa waelewa na kuendana na upepo unavyovuma mtakuwa wajinga na wapumbavu na hii nchi CDM kuikamata haitotokea kwa akili hizi...

Ukitaka kufanya siasa kwenye kila kitu huwezi kufika popote, kuna muda tumia akili, na hapo CCM ndipo inawazidi kila siku...

Ok uzi wa tanzia huu, RIP JOB NDUGAI
CCM inazidi kila siku kwasababu Wana dola na polisi ndo maana siyo lingine. Wepesi sana kuliko pamba.

Erythrocyte
 
Back
Top Bottom