TANZIA GE2025 Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

TANZIA GE2025 Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Yaani nyinyi mbwa ikiwezekana mfutwe kabisa,mimi si pro-ndugai,lakini kwa nini ushangilie kifo cha mtu!?..sikua pro-magu,sikushangilia kifo chake
Umesahau cha Ally Kibao, tuliambiwa kifo ni kifo tu? Au kibao ni mnyama na ndugai ni binadamu
 
Yaani nyinyi mbwa ikiwezekana mfutwe kabisa,mimi si pro-ndugai,lakini kwa nini ushangilie kifo cha mtu!?..sikua pro-magu,sikushangilia kifo chake
Tukifutwa ndiyo atafufika,mjinga kweli wewe nyie mnavyofurahia kuuawa na kutekwa Kwa ndugu zetu mnaona sawa.
Yaani KIFO Cha ndugai kinauma kuliko kupotea na pengine kufa Kwa kina Ben,Soka,Mlay Mzee kibao na wengine.
KUFENI takataka nyie,tena mfe vibaya.
 
Somo kuu kwa wazee walio madarakani, tenda wema ili siku zako za kuishi ziwe nyingi.
 

Aliyewahi kuwa Spika na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia, leo Agosti 6, 2025, taarifa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson imeeleza kuwa msiba umetokea Dodoma

Dkt. Tulia amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

WASIFU MDOGO WA JOB NDUGAI
Alizaliwa Januari 21, 1963 na kupata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.

Amesoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).

Amesoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).

Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008)

Amekuwa Mbunge wa Kongwa kwa miaka 25 sasa (tangu mwaka 2000) na ameshika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.

Alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.

Katika uongozi wake wa bunge, mambo kadhaa yameibua mjadala mkubwa ikiwemo sakata la wabunge 19 wa CHADEMA wanaodaiwa kuvuliwa uanachama wao, na kuhojiwa kwa baadhi ya wabunge akiwemo Josephat Gwajima na Jerry Muro kwa madai ya kushusha hadhi na heshima ya bunge.

Suala jingine ni kumtaka mmoja wa wabunge aliyedai amevaa nguo zisizo za staha kutoka ndani ya ukumbi wa bunge. Uamuzi huo ulikosolewa vikali, wakosoaji wakieleza kwamba vazi la mbunge huyo halikuwa na tatizo. Karibuni, amezua mjadala tena kwa kusema Tanzania haitakiwi kukopa ili kufadhili miradi ya maendeleo.

Mbali na ubunge, amefanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Januari 6, 2022 amejiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.

Ndugai ni mume wa Fatuma Mganga.
Mungu adhihakiwi angalia kauli zao kabla na bado

Bado yule wa kifo ni kifo tu na yule wa wachawi walishakufa

Mwaka huu lazima mmalizane
 
Edmond alisema kwenye maono yake kuwa anaona mtu anatumwa kutoka Dodoma akiwa ameshika chupa nyeusi ikiwa na mfano wa poison kumdhuru mmoja kati ya watu watano wenye nguvu ya maamuzi
Yani nimeenda tena you tube kuichek clip yake mh trh alotaja ni mulemule.
 
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia leo August 06,2025 akiwa anaendelea kupatiwa matibabu Hospitalini baada ya kuugua ghafla. Ndugai amekuwa Spika wa Bunge tangu November 17, 2015 hadi Januari 06, 2022 alipojiuzulu na kuendelea kuwa Mbunge wa Kongwa nafasi ambayo ameendelea kuitetea kwa kuchukua fomu tena mwaka huu ambapo ameshinda kwenye kura za maoni. Ndugai ambaye amezaliwa January 22,1960 alishinda kura za maoni za Ubunge wa Jimbo la Kongwa kwa kupata kura 569
View attachment 3434043
Walijiba mafao wakidhani wataishi mille Asante mungu
 
Back
Top Bottom