Tulisema utawala wa mwendazake (revered) hayati (late) Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli ulikuwa wa kidiktekta na kuburuza mihimili yote ya dola Tanzania kufanya maamuzi yasiyo sawa na pia kuwaumiza waTanzania wengi.
Watu majumba yao yalivunjwa kupisha miradi bila fidia, wafanyabiashara kutishwa, raia kubambikiwa kesi, uhuru wa kujieleza kubinywa, mbinyo mkubwa ulitumika kuwatisha watendaji serikalini wasitoe haki, uchaguzi ulikuwa ni wa hadaa, listi ni ndefu ya mapungufu na ukatili haya yote yanabidi kunakiliwa na kuandikiwa kitabu yasijitokeze tena ktk Tanzania yetu.