Job Ndugai: Sijawahi kumjulia hali Tundu Lissu kwani ananiona kama shetani | Mbowe asikimbilie Urais kuficha aibu ya kushindwa Ubunge

Yani anafanya kumuattack tu mbowe kila swali analoulizwa, mara hakupigwa alianguka ni story nilizosikia yani anaongea naye hana uhakika. Mara alilewa chakali
Sasa mkuu ulitegemea majibu ya aina gani kwa mtu aliyekua anasimamia mhimili wa bunge ambae nae alimpiga gongo la kichwa mgombea mwenzake mpk akazimia then suala la Mbowe kushambuliwa yeye atashangaa nini sasa mkuu?Maana kama ni suala la kutoa kichapo yeye ndio master.
 
Mbowe hakushambuliwa ila alilewa akaanguka na kuteguka mguu
 
Hapa wanapoenda kwenye matangazo mambo yanaweza kubadilika maana wamejitahidi kumswalika kwelikweli mpk unaona aliyekuwa spika anawayawaya
 
Spika kwa jinsi anavyoongea hawezi kuwa mwamuzi wa haki. Ana chuki binafsi na iliyokuwa kambi rasmi ya upinzani . Anawabeza na kuwadhalilisha tu.

Haongei kama msomi bali kada mkereketwa.
 
Akiwa katika 360 ya Clouds Media, Job Ndugai amesema toka Tundu Lissu apate lile tukio la kupigwa risasi hakuwahi kumpigia simu yeye binafsi ya kumjulia hali kwani anajua Tundu Lissu anamuona Ndugai kama shetani. Hivyo Job Ndugai haoni sababu ya kumpigia simu mtu anayemuona yeye ni shetani.

Sambamba na hilo,pia Ndugai amemtaka Mbowe aache kukimbilia kwenye urais kama kichaka cha kukwepa aibu ya kushindwa vibaya kwenye ubunge. Ndugai anaamini kuwa Mbowe amekimbilia kwenye urais baada ya kuona ubunge hawezi kushinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…