Akiwa katika 360 ya Clouds Media, Job Ndugai amesema toka Tundu Lissu apate lile tukio la kupigwa risasi hakuwahi kumpigia simu yeye binafsi ya kumjulia hali kwani anajua Tundu Lissu anamuona Ndugai kama shetani. Hivyo Job Ndugai haoni sababu ya kumpigia simu mtu anayemuona yeye ni shetani.
Sambamba na hilo,pia Ndugai amemtaka Mbowe aache kukimbilia kwenye urais kama kichaka cha kukwepa aibu ya kushindwa vibaya kwenye ubunge. Ndugai anaamini kuwa Mbowe amekimbilia kwenye urais baada ya kuona ubunge hawezi kushinda.