Job Ndugai: Sijawahi kumjulia hali Tundu Lissu kwani ananiona kama shetani | Mbowe asikimbilie Urais kuficha aibu ya kushindwa Ubunge

Job Ndugai: Sijawahi kumjulia hali Tundu Lissu kwani ananiona kama shetani | Mbowe asikimbilie Urais kuficha aibu ya kushindwa Ubunge

Hii inadhihirishwa kuwa CCM mi Chama Cha Mashetani. Mwambie kuwa 40%ya waliochukua fomu urais wa ccm 2015waligombea ubunge.Inakuwaje spika hajui vitu vyepesi Kama hivi.Kweli ccm ni utopolo
 
Akiwa katika 360 ya Clouds Media, Job Ndugai amesema toka Tundu Lissu apate lile tukio la kupigwa risasi hakuwahi kumpigia simu yeye binafsi ya kumjulia hali kwani anajua Tundu Lissu anamuona Ndugai kama shetani. Hivyo Job Ndugai haoni sababu ya kumpigia simu mtu anayemuona yeye ni shetani.

Sambamba na hilo,pia Ndugai amemtaka Mbowe aache kukimbilia kwenye urais kama kichaka cha kukwepa aibu ya kushindwa vibaya kwenye ubunge. Ndugai anaamini kuwa Mbowe amekimbilia kwenye urais baada ya kuona ubunge hawezi kushinda.

This is nonsense 100%
Kwahiyo kwenye urais hakuna aibu ya kushindwa?
Dah shetani bwana.
 
Huyo ni kiongozi anaongoza Bunge la Tanzania. Poleni sana waTanzania; Job hajui kuwa mh Rais anamwona kama Shetani na bado anampigia na simu.
 
Aisee nimesikiliza mahojiano...anyway tumuombe mungu tupate kiongozi mwingine bunge lijalo!

Hongera yule mwanadada atleaset alikuwa na maswali mazuri!
 
Nadhani huyu mheshimiwa kabisa hakufaa kuwa spika wa bunge, upeo wake na busara zake zipo kidogo japo nasikia ni msomi, ndio pale tunasema unaweza kwenda shule lakini ukabaki na uzwazwa wako kama zamani tu.
 
Akiwa katika 360 ya Clouds Media, Job Ndugai amesema toka Tundu Lissu apate lile tukio la kupigwa risasi hakuwahi kumpigia simu yeye binafsi ya kumjulia hali kwani anajua Tundu Lissu anamuona Ndugai kama shetani. Hivyo Job Ndugai haoni sababu ya kumpigia simu mtu anayemuona yeye ni shetani.

Sambamba na hilo,pia Ndugai amemtaka Mbowe aache kukimbilia kwenye urais kama kichaka cha kukwepa aibu ya kushindwa vibaya kwenye ubunge. Ndugai anaamini kuwa Mbowe amekimbilia kwenye urais baada ya kuona ubunge hawezi kushinda.

This is nonsense 100%
Mbowe atuambie alimfanya nini Ndugai pale Kibaha sec?!
 
Ni kweli kabisa Mbowe akigombea ubunge ataaibika vbya Bora ajifiche huko huko kwenye urais
 
Back
Top Bottom