Job Ndugai: Sijawahi kumjulia hali Tundu Lissu kwani ananiona kama shetani | Mbowe asikimbilie Urais kuficha aibu ya kushindwa Ubunge

Job Ndugai: Sijawahi kumjulia hali Tundu Lissu kwani ananiona kama shetani | Mbowe asikimbilie Urais kuficha aibu ya kushindwa Ubunge

Natazama 360 Clouds naona Hassan Ngoma anambana Spika maswali mpaka anajichanganya kuhusu suala la Mbowe.

Kuhusu sheria ya habari analalamika lalamika tu kuwa wapinzani wanapendelewa na mitandao ya kijamii na waandishi wa habari...
Uyu mzee ana elimu gani?
 
Hata ukimchukia haisaidii chochote sana Sana itakuzeesha na kukusabsbishia makunyanzi usoni. Raha jipe mwenyewe
 
Nadhani huyu mheshimiwa kabisa hakufaa kuwa spika wa bunge, upeo wake na busara zake zipo kidogo japo nasikia ni msomi, ndio pale tunasema unaweza kwenda shule lakini ukabaki na uzwazwa wako kama zamani tu.

Inanikumbusha Headmaster wa shuleni. Alikua akisema : There’s a difference between going “to” school and going “through” school!
 
Hii Interview ya Leo 360 wamejua kuitendea haki. Ndugai anaulizwa maswali anajibu ambacho hakuulizwa.. Anakazana na Mbowe.. Mbowe na Kundi lake.

Hassana Ngoma mwishoni anamuuliza Bunge lake limekuwa kama linakandamizwa na Serikali na Bunge ni Mhimili unaojitegemea.. Anajibu eti kipindi chake cha Bunge wamefanikiwa kutengeneza kumbi za mikutano hapo hapo Bungeni na siyo kwenda UDOM au CBE Kama miaka ya nyuma.. Pia wameweka na lifti kwenda Ghorofa ya Nne..Swali analoulizwa na Majibu ni tofauti.. Hadi Aibu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye bado ni spika hadi hapo atakapochaguliwa spika mwingine, bunge limevunjwa lakini nafasi ya spika inabaki hivyo.

Ni kweli kabisa. Aidha Spika anaweza kuitisha kikao cha Bunge la dharula kama kutakuwa na jambo linalohitaji maamuzi ya Bunge. Yeye bado ni Spika mpaka atakapopatikana Spika mwingine wa Bunge lijalo.
 
Hii Interview ya Leo 360 wamejua kuitendea haki..
Ndugai anaulizwa maswali anajibu ambacho hakuulizwa.. Anakazana na Mbowe.. Mbowe na Kundi lake.

Hassana Ngoma mwishoni anamuuliza Bunge lake limekuwa kama linakandamizwa na Serikali na Bunge ni Mhimili unaojitegemea.. Anajibu eti kipindi chake cha Bunge wamefanikiwa kutengeneza kumbi za mikutano hapo hapo Bungeni na siyo kwenda UDOM au CBE Kama miaka ya nyuma.. Pia wameweka na lifti kwenda Ghorofa ya Nne..Swali analoulizwa na Majibu ni tofauti.. Hadi Aibu...

Sent using Jamii Forums mobile app

Alikuwa anafanya kusudi tu. Hilo swali hawezi lijibu.
 
Ndugai punguza uswahili, ktk nchi nyingine Spika ni mtu mkubwa sana! ila ktk miaka yako spika imekuwa tofauti kabisa na enzi za Sitta na makinda. hadi bunge limeonekana la mipasho, uswahili na mambo ambayo hata std 6 hayapo!
 
Natazama 360 Clouds naona Hassan Ngoma anambana Spika maswali mpaka anajichanganya kuhusu suala la Mbowe.

Kuhusu sheria ya habari analalamika lalamika tu kuwa wapinzani wanapendelewa na mitandao ya kijamii na waandishi wa habari...
Mmm! kumbe mwezi wa 10 siyo mabali
 
Ni kweli kabisa. Aidha Spika anaweza kuitisha kikao cha Bunge la dharula kama kutakuwa na jambo linalohitaji maamuzi ya Bunge. Yeye bado ni Spika mpaka atakapopatikana Spika mwingine wa Bunge lijalo.
Akiitisha hicho kikao cha dharula wanahudhuria akina nani kwa mujibu wa katiba?
 
Back
Top Bottom