Mimi nilikuwa nashangaa sana, America yenye watu milioni 300 au zaidi inakuwaje waweke wazee ilihali watu wa makamo au vijana wanao, kwa nini kumg'ang'ania Joe Baden na Donald Trump
Nimekusoma na kufikiri kwa kina zaidi udadisi wako katika mistari yako hii miwili. Ni udadisi mzuri.
Mimi sina jibu ninaloweza kusema ni sahihi; lakini nitakurudisha nyuma kidogo, hasa kwa upande wa Trump alivyo fikia hapo wakati huu.
Kulikuwa na watia nia wengi kwenye nafasi hiyo, ambao mchujo uliwaondoa hadi kabaki Trump mwenyewe, pamoja na maswala yake mengi ya kesi yaliyokuwa yakimkabili
Hao watia nia wengi walikuwa ni vijana/wamakamo, siyo wazee kama Trump. Na Trump mwenyewe wala hakujihangaisha kupambana nao kwenye kinyang'anyiro huko kwenye ngazi za chini. Walihangaishana wao wenyewe kwa wenyewe kwa kuchuana na kudondoka mmoja mmoja hadi kabaki Trump pekee amesimama!
Ni kipi hasa kilichofanya Trump apendwe hivyo licha ya tabia zake? Sijui
Unajuwa, hawa wenzetu wenye vyama huko, kama hao Republicans, humo humo ndani ya chama kimoja kuna makundi yanayonyukana wao kwa wao. Hili kundi linalomsukuma Trump, ndilo lenye nguvu zaidi katika chama hicho. Hawa ni wahafidhina kwelikweli, na baadhi yao ni yale mapapa hasa ya ubaguzi. Wanaungana ndani ya chama hicho kumuunga mkono Trump kwa sababu ndiye anayeonyesha tabia na mambo yanayowakuna wao; mambo ambayo wangependa nchi hiyo iyawekee mkazo zaidi wakati huu katika siasa za nchi hiyo.
Ukienda upande wa Democrats, wao pia ndani ya chama chao kuna makundi hivyo hivyo, ambayo kila kundi linakuwa na watu/viongozi wanaopenda washike uongozi kuendeleza mambo wanayo yapenda wao. Biden, yeye hakushindana kwenye 'Primaries', kwa vile tayari alikuwa ni kiongozi. Kwa hiyo hapakutokea watu wa kutaka kumng'oa kwa vile alikuwa anategemewa kwenda kumaliza mhura wake wa miaka minne. Swala la uzee wake halikuwepo hadi hapo alipoonyesha dalili za wazi kabisa kwamba uzee unamchanganya.
Niseme tu kwa kumalizia, swala hapa siyo umri mkubwa/uzee, bali ni uwezo wa kuongoza na kujuwa maswala muhimu ya kuwa kiongozi.