Joe Biden asinzia wakati Makamu wa Rais Dkt. Mpango akizungumza

Tatari alishaachana na urais baada ya kupigwa Knokout na Trump. Sasa anaandaa majabidhiano.
 
Lengo lilikuwa sio kukutana na Tanzania, Tz kajipendekeza tu Ndio maana kapuuzwa kusikilizwa
Acha utoto basi. Au kama hujui nyamaza! Tanzania ilijipeleka? Unajua Lobito railway inaanzia wapi hadi wapi na kwanin Tanzania imealikwa? Tumia hii simu kupata taarifa sahihi. 🙏🙏🙏
 
Tena hapo kajitahidi, angekuwa anazungumza MAMA angeletewa kitanda kabisa.
 
Inachosha kweli mtu unakwenda kuwekwa kwenye ma-cage ya chuma kama anavyoonekana hapo pichani lazima uchoke tu na kusubiria kurudi nyumbani mapema iwezekanavyo.
 
Sasa habari za "on behalf of her excellency..." zinamhusu nini huyo mzee?
Hata mimi ningeuchapa tuu..
 
Sass kama hakuna point ya kusikiliza baba wa watu si alale tuu
 
Huyo kachoka, katepeta tepetepe. Katumika sana Hadi kaexpire, hivyo anatamani hata Leo akapumzike.
 
Mkuu umeona mbali😂
 
Nilitegemea nawe kumpenda, kama maudhui ya majadilano haya yalipo tukutanishia. Lakini naona taratibu unajiweka pembeni, umebaki tu kuwa mtu wa kupenyeza viswali hapa na pale, huku mjadala ukibadilika!
Ni yeye alyeanzisha miradi ya kimkakati. SGR, Bwawa la umeme, maji,kupunguza rushwa, elimu bure,kujenga international airport, port mbalimbali,mfumo.mpya wa malipo serikalini, passport mpya,

Barabara, NIDA, hospitali, shule, vyuo, kujenga vivuko,vituo kama magufuri stand. Ni ubishi na chuku binafsi zinaweza kushindwa kuelewa mchango wake jambo alikuwa na mapungufu mengine hasa kuhusu demokrasia. Hakuamini kivile kwa hii aina ya demekrasia.

Nikiangalia SSH, Mbowe, Zitto sioni tofauti.

Naona Warioba ndiyo muwakilishi wa ukweli.
 
au alikua anaombwa hera...maana wenye hera bana wana visa
 
Lengo lilikuwa sio kukutana na Tanzania, Tz kajipendekeza tu Ndio maana kapuuzwa kusikilizwa
Negativity can be a way to blame your discomfort on someone or something else, it may make you feel better at first. But at the end it's the sign of stress.

Take it easy.......it is not possible Tz to invite itself in such event. Though I agree that, the meeting is not good for African countries future.
 
Wakiwa Angola, Joe Biden anaonekana akisinzia wakati makamu wetu wa Rais akizungumza.

Babu Biden kachoka. Arudi kwao huko Delaware akapumzike na wajukuu wake.

Hii ni aibu.
Inawezekana pia hotuba ya Makamu wetu wa Raisi ilikuwa inaboa. Labda alianza kuingiza uchawa akajisahau Biden sio kama Raisi wa Tanzania anaefurahia kusikia uchawa
 
Mkuu 'Lookmasin', basi nikadhani tumekwisha agana huko juu, kumbe bado kuna viporo huku chini vinahitaji kumaliziwa!

hayo uliyo eleza hapo juu kumhusu Magufuli, sina lolote ninalo weza kunyoosha uso wangu na kuyakataa hayo mema yaliyo lenga nchi yetu. Ukinisoma humu kumhusu Magufuli tokea mwanzo wake utatambua kuwa sijawahi hata siku moja kumnyima haki yake kuhusu hayo; isipo kuwa labda katika njia za utekelezaji wa baadhi ya mambo hayo. Uwanja wa kimataifa Chato lilikuwa ni kosa moja lililo onyesha udhaifu wake katika uongozi. Hilo sikukubaliana nalo hata mara moja, na jinsi alivyo shughulikia kwa upendeleo maalum kwa eneo lake. Huo ulikuwa ni udhaifu wa uongozi.

Lakini tukitazama upande wa pili wa Magufuli; upande ambao kwangu na wengi wengine ulimwondolea sifa stahiki kwa hayo mazuri yake, ni tabia zake kama binaadam, ambazo zilikuwa hazilingani kabisa na heshima ya uongozi wa nchi.
Alipenda sana kusifiwa, nadhani hata hii dhana ya "uchawa" kwa mama imeanzia huko kwa Magufuli.
Sijui kama kweli alikuwa na dhamira ya kweli juu ya "wanyonge" alio kuwa akiwaimba mara kwa mara kila alipoona anastahiri sifa. nahoji hili, kwa sababu halikuendana sana na matendo yake ya kutaka kuwainua wanyonge hao. Nilichoona ni kama alikuwa akitafuta wanyonge wawe upande wake zaidi kwa nadharia tu, sikuona vitendo thabiti toka kwake.
Tabia za kiongozi kukiuka au kutofata taratibu na sheria zilizopo; hili lilionekana wazi zaidi toka kwake, na Samia sasa hivi anatembelea humo humo, hastuki. Chukulia mfano wa chaguzi za 2019/2020 zilivyo kuwa; na sasa 2024 tayari tumejionea wenyewe, na tunasubiri tu kumaliza kwa kishindo hapo 2025. Huu ni mfano mmoja tu wa ukiukwaji wa taratibu na sheria ulio kuwa ni sehemu ya ungozi wa Magufuli; uongozi usio kuwa na heshima hata kidogo.
Mambo ya uonevu kwa watu wengine ambao walionekana kuwa na maoni yanayo pingana na ya kwake. Angalau ange jitahidi kuonyesha njia mbadala za kuwa zuia, kama kuwapeleka mahakamani, hata kwa uigizaji, kidogo ingempunguzia mwonekano mbaya alio uonyesha kama kiongozi.

Kama ulivyo sema, yapo mengi ya kumpendea Magufuli, kama hayo uliyo orodhesha hapo juu, na hata pengine kwa baadhi ya mabaya yake kama nilivyo jaribu kuyaeleza hapo juu.
Ndiyo maana sasa, hata mimi ukiniuliza sasa hivi ni kiongozi gani Tanzania inamhitaji kutokana na wananchi wa nchi hii walivyo sasa; nitakwambia bila kuficha kwamba tunamhitaji MAGULI mwingine asiye kuwa na baadhi ya mabovu zaidi aliyo kuwa nayo Magufuli...., kama uonevu, na ukiukwaji wa sheria.
Tukimpata kiongozi wa aina hiyo, hata hizi nyimbo za Demokrasia mimi hazinisumbui sana. Kiongozi awe ni mtu anaye ipenda Tanzania na wananchi wake wote kwa moyo thabiti. Huyo ndiye tunge bahatika kumpata; nchi yetu ingetulia kabisa..
 
Wewe tukupe uongozi leo utakuwa na kasoro zako, blind spots zako labda utaangalia waliokuunga mkono ukawapa vipaumbele.

Lakini kwa ujumla ukiwa fair unaweza kusema kweli Magufuli hakusaidia Watanzania, hakuwa Mzalendo? Samia hajaanzisha hata mradi mmoja, hana sera hata moja ya ukombozi, ubunifu anatembea kwa sera za Magufuli na kuwalipa wapinzani. Hakuna original idea, seriousness, nia thabiti kusaidia nchi.
 
Lakini kwa ujumla ukiwa fair unaweza kusema kweli Magufuli hakusaidia Watanzania, hakuwa Mzalendo?
Nadhani kwa kumpenda zaidi Magufuli, inawezekana ukawa unakosa uwazi wa akili unao takiwa kuwa nao. Mimi sijasema kuwa Magufuli hakuwa na mazuri. Nisome vizuri unielewe; labda lugha niliyo tumia kidogo inafanya nisieleweke kirahisi.

Swala la "Uzalendo" wa Magufuli siwezi kumhukumu juu ya hilo. Niliona maneno mengi na baadhi ya vitendo vilivyo ashilia kuwa ni Mzalendo. Lakini pia niliona vitendo vilivyo onyesha mapungufu ya uzalendo huo. Ninapenda kuamini kwamba alikuwa ni mzalendo ambaye baadhi ya matendo yake yalimwondolea sifa hiyo.

Ni vigumu sana mtu yeyote kutafsiri 'uzalendo' wa mtu mwingine kwa nchi yake. Siyo rahisi sana kufanya hivyo. Ndiyo maana, katika viongozi wote tulio wahi kuwa nao nchi hii, ukiniuliza nikutajie moja kwa moja ninaweza kumwona kuwa alikuwa ni mzalendo wa kweli bila ya kusita kabisa, nitakutajia wawili tu..., hii haina maana hao wengine hawakuwa na uzalendo, la hasha.
Mwalimu Nyerer na Edward Sokione hawa walikuwa ni wazalendo wa kweli kweli wa nchi hii. Lakini hapo hapo, siwezi kamwe kusema Kikwete siyo mzalendo moja kwa moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…