Kila mtu ana kiwango cha kuhimili matatizo na hizi ni changamoto tu za maisha hata mimi na wewe as long as tunapumua bado hatuna haki ya kusema hatuwezi kufikia hali ya jamaa muhimu tusali sana Mungu atuepushe.
Mimi namjua jamaa alikopa bank zaidi ya Tsh 200mill akaenda China kufunga mzigo akakutana na wahuni wakamnyoosha alipigwa cash yote akabaki mweupe akarudishwa bongo na ubalozi leo tupo nae mtaani hapa Kariakoo anapiga winga zake maisha yanaenda mwengine alikopa aendeleze biashara akaletewa mzigo mbovu akajinyonga,unaweza ukaona mmoja alikopa aanze biashara akapoteza akabaki normal huyu mwingine biashara alikuwa nayo tayari ila alipopoteza akajidhuru.
Ni vitu vya ajabu sana.
Kuwa karibu na Mungu kwa kufanya ibada(sio ile mi niko karibu na Mungu halafu hutendi yaliyo mema) ,humfanya mtu kuepukana na mawazo mengi maovu na mabaya.
Tukubali tukatae, mwanadamu unavyozidi kuwa mbali na Mungu ndivyo unavyozidi kuwa karibu na shetani na ndivyo mawazo mabaya zaidi kichwani huongezeka.
Shetani kazi yake ni kumpa mtu mawazo mabaya na ahadi za uongo, kwamba ukijiua ndio utapata ahueni dhidi ya matatizo yanayokukabili.
Amini, Amini nawaambieni ikiwa mtu utathubutu kutoka na kwenda kuona wagonjwa mahospitalini walau mara moja kwa wiki basi utajua nini umuhimu wa uhai . Toka ukae na watoto yatima, mafukara n.k halafu cheki jinsi gani wana furaha licha ya kuwa na hali duni, then utathamini kila ulicho nacho.
Amini, Hakuna kitu kinaua moyo kama kupendelea kukaa sana na watu wenye vipato vikubwa na wapenda starehe. Kuna mtu anapata stress tu kuona why hana uwezo wa kununua hennessy au kuwa na magari ya kisasa tu kama vijana wadogo wanaoenda kutamba pale kidimbwi.Stress zinampelekea hadi kukata tamaa ya maisha , anaona dunia ishakuwa ndogo,hastahili trna kuishi na hapo ndipo shetani hukuletea evil solution ,commit suicide!!! Jiue ili ukapumzike.
Amini ukijiua ,jua umejidhulumu nafsi yako na huko uendako hakuna mapumziko bali adhabu tu. Kwanza kujiua ni kukata tamaa na rehema za Mola wako.Huamini kuwaanaweza kukuvusha katika hali ngumu unayoipitia.
Hakuna akatae tamaa na rehema za mola wake isipokuwa dhalimu
Mungu atulinde sisi na vizazi vyetu dhidi ya kuzidhulumu nafsi zetu kwa kujiua ameen