Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Pale Mwanga Tower, Makumbusho limetokea tukio la mtu asiyefamika kujirusha kutoka gorofani, ambapo inasemekana tukio hilo limetokea mapema leo majira ya saa kumi na moja asubuhi.
Mpaka majira ya saa mbili asubuhi bado mwili wa mtu huyo ulikuwa eneo hilo. Taarifa zaidi zitakujia kadri zitakavyopatikana.
Joel Misesemo enzi za uhai wake
=====
Kijana asiyefahamika aliyekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35 amefariki baada ya kujirusha kutoka gorofa ya 15 katika jengo la Derm lililopo Makumbusho, Dar es Salaam.
UPDATE: Polisi yathibitisha aliyejiua, kufanya uchunguzi
POLISI: KAMERA ZIMEONESHA JOEL MISESEMO AKIJIRUSHA MAKUSUDI KUTOKA GHOROFA YA 7
Kufuatia tukio la kifo cha Joel Misesemo Chizi mwenye umri kati ya miaka 35 hadi 40, Mkazi wa Mwananyamala, Jeshi la Polisi limesema chanzo cha awali ni mhusika kujirusha kutoka ghorofani kwenye jengo la Derm Plaza lililopo Makumbusho Kijitonyama.
Imeelezwa kuwa Joel alifika eneo hilo akiwa na gari aina ya Suzuki rangi ya silver (T142 DRM) na kuonekana katika jengo hilo Saa 11 Alfajiri ya Mei 23, 2023, akamwambia Mlinzi wa zamu kuwa anaenda kufanya ibada kwenye Msikiti uliopo ghorofa ya 15 ndani ya jengo hilo, muda mfupi baadaye alijirusha.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema kamera za jengo hilo zimemuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya 7 kupitia dirishani na mwili wake umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa uchunguzi Zaidi