Joel Peter kawauliza waislamu na wakristu swali gumu

Joel Peter kawauliza waislamu na wakristu swali gumu

Mbona nyie mnasomewa mistari ileile kila leo,mjinga nani?
Kwani unasumbua vip na kitu hukiamini 😅😅You're doubting yourself. Yaani hapo una wasiwasi,unataka maisha yawe hivi ..
Jiulize kwa utashi wako wewe tu mbona unashindwa kuwa kama mtu fulani ?
 
Dunia imepitia uongo, utapeli, na propaganda nyingi Sana,
ila Uongo mkubwa zaidi ni huu,

Hebu fikiria, unaambiwa kuna mungu muweza WA yote, yupo sahihi na hajawahi kukosea,

Ameumba dunia kwaajili yetu, na ataiangamiza tena kwaajili yetu,
Alijua ataiangamiza dunia kabla hata hajaiumba, 🥱.

Lakini aliimba hivyo hivyo,😅 ili aje kuiangamiza

Ameumba Moto WA jehannamu kwakua ametuumba tukosee ili atuchome, 🤔

japo alikua na uwezo wa kutuumba tusiwe wakosefu, ili atuumbie Pepo Tu, watoto wake pendwa

Anajua tunachohitaji lakini mpaka tumuombe, 🐐
hapa yaani kazidiwa mpaka na mbuzi, anaye hudumia watoto wake,

Hebu fikiria hii, kawaumba Adam na hawa, wakiwa bado wageni duniani akawatupia joka, ili liwajaribu,
na Kwa ugeni wao wakarubunika. lakini aliwapa Adhabu ya shuruba watu wote hata ambao walikua hawajazaliwa wakajumuishwa, 🤯

Any ways
Usiwape mbwa ?
Credit : Joel Peter FacebookView attachment 3634865

Kuna vitabu vingi sana vimeeleza juu ya masuala ya dini. Vitabu hivyo vyote vimeandikwa na watu. Hata Biblia na Quaran vimeandikwa na kutafsiriwa na watu. Lakini hayo mawazo yaliyoelezewa humo yalitoka wapi?

Binafsi naamini neno kuu limetoka kwa muumba. Ni neno sio vitabu. Watu walioandika vitabu hawakuzuiliwa kuweka pia tafsiri zao.

Inawezekana kuna mambo yaliongezwa, na pengine kuna mambo hayakuwasilishwa. Hilo ni swala jingine.

Suala la Dunia ilivyo leo; ni matokeo ya mwanadamu kuasi kusudi la Mungu. Sitaki kuamini kuwa Mungu aliumba dunia ili aje kuiangamiza. Ila Mungu alisikitishwa na uasi wa mwanadamu, akadhamiria kuiagamiza Dunia.

Biblia na Quaran ni miongoni mwa kitabu kilichoweza kupenya kwa nguvu kubwa sana. Ila pia vipo vitabu ambavyo havikupata hiyo nafasi. Yapo mawaidha ambayo hayakupata nafasi. Uasi wa mwanadamu tangu enzi ndio maana tumeishi dunia yenye misukosuko.
 
Unataka kusema Mungu hakujua kuhusu uasi utakao kuja kutokea duniani kabla hajaiumba hadi asikitishwe
 
Yes inawezekana kabisa tena katika uislam siyo tu kukusamehe bali pia kama wewe uliyeomba masamaha upo serious kweli basi yale mabaya yanageuzwa kuwa mema...Huwa al ghafur al Rahim.
Mkuu yanageuzwaje mabaya kuwa mema?! Kwamba kama ulipata 100% ya mabaya inageuka kuwa 100% ya mema au. Embu nisaidie mkuu
 
Katika viumbe Mungu alivyo Umba Binadamu ndiye aliyepewa uwezo wa kufanya mambo kwa uamuzi wake/ free will na ndio sababu atahukumiwa kwa jinsi aalivyotumia huo uhuru.
hata hivyo Mungu ameweka dirisha la kuomba msamaha ambalo lipo wakati wote pale tunapo mkosea na tukajirekebisha na Kuomba msamaha...
tofauti na wanyama wengine...
Wewe umeyajuaje yote hayo mkuu?
 
Mbona wanyama wanateseka, wameumbwa ili wateseke? Wengine wanawindwa na kuliwa na wanyama wenzao, wengine wanawindwa na binadamu kwa mahitaji mbalimbali sasa nao kosa lao ni nini mpaka wapitie kashkash zote hizo?
 
Mungu yupo ila biblia na qur an zinatupeleka chaka tena amazon kabisa.. kwaiyo mungu amefanya wazungu watengeneze gari halafu sisi tutengeneze vikombe na maplastiki
 
Mungu yupo ila biblia na qur an zinatupeleka chaka tena amazon kabisa.. kwaiyo mungu amefanya wazungu watengeneze gari halafu sisi tutengeneze vikombe na maplastiki
Biblia na Quaran vimezuia mwafrika hasitengeneze gari? 😂
 
Mbona wanyama wabateseka, wameumbwa ili wateseke? Wengine wanawindwa na kuliwa na wanyama wenzao, wengine wanawindwa na binadamu kwa mahitaji mbalimbali sasa nao kosa lao ni nini mpaka wapitie kashkash zote hizo?
Hawana consciousness kama ya binadamu
 
Biblia na Quaran vimezuia mwafrika hasitengeneze gari? 😂
Walipotuwin wazungu waliwai kupata taarifa kuhusu habari za Mungu. Na kuna maarifa walituficha.

Mzungu yeye amepambana kuna mambo muafrika hasiyatambue. Na ametufundisha namna ya kukataa vya kwetu vya asili tulivyopewa na Mungu, tusadiki vya Mzungu.
 
Back
Top Bottom