Joel Peter kawauliza waislamu na wakristu swali gumu

Mbona nyie mnasomewa mistari ileile kila leo,mjinga nani?
Kwani unasumbua vip na kitu hukiamini 😅😅You're doubting yourself. Yaani hapo una wasiwasi,unataka maisha yawe hivi ..
Jiulize kwa utashi wako wewe tu mbona unashindwa kuwa kama mtu fulani ?
 

Kuna vitabu vingi sana vimeeleza juu ya masuala ya dini. Vitabu hivyo vyote vimeandikwa na watu. Hata Biblia na Quaran vimeandikwa na kutafsiriwa na watu. Lakini hayo mawazo yaliyoelezewa humo yalitoka wapi?

Binafsi naamini neno kuu limetoka kwa muumba. Ni neno sio vitabu. Watu walioandika vitabu hawakuzuiliwa kuweka pia tafsiri zao.

Inawezekana kuna mambo yaliongezwa, na pengine kuna mambo hayakuwasilishwa. Hilo ni swala jingine.

Suala la Dunia ilivyo leo; ni matokeo ya mwanadamu kuasi kusudi la Mungu. Sitaki kuamini kuwa Mungu aliumba dunia ili aje kuiangamiza. Ila Mungu alisikitishwa na uasi wa mwanadamu, akadhamiria kuiagamiza Dunia.

Biblia na Quaran ni miongoni mwa kitabu kilichoweza kupenya kwa nguvu kubwa sana. Ila pia vipo vitabu ambavyo havikupata hiyo nafasi. Yapo mawaidha ambayo hayakupata nafasi. Uasi wa mwanadamu tangu enzi ndio maana tumeishi dunia yenye misukosuko.
 
Unataka kusema Mungu hakujua kuhusu uasi utakao kuja kutokea duniani kabla hajaiumba hadi asikitishwe
 
Yes inawezekana kabisa tena katika uislam siyo tu kukusamehe bali pia kama wewe uliyeomba masamaha upo serious kweli basi yale mabaya yanageuzwa kuwa mema...Huwa al ghafur al Rahim.
Mkuu yanageuzwaje mabaya kuwa mema?! Kwamba kama ulipata 100% ya mabaya inageuka kuwa 100% ya mema au. Embu nisaidie mkuu
 
Wewe umeyajuaje yote hayo mkuu?
 
Mbona wanyama wanateseka, wameumbwa ili wateseke? Wengine wanawindwa na kuliwa na wanyama wenzao, wengine wanawindwa na binadamu kwa mahitaji mbalimbali sasa nao kosa lao ni nini mpaka wapitie kashkash zote hizo?
 
Mungu yupo ila biblia na qur an zinatupeleka chaka tena amazon kabisa.. kwaiyo mungu amefanya wazungu watengeneze gari halafu sisi tutengeneze vikombe na maplastiki
 
Mungu yupo ila biblia na qur an zinatupeleka chaka tena amazon kabisa.. kwaiyo mungu amefanya wazungu watengeneze gari halafu sisi tutengeneze vikombe na maplastiki
Biblia na Quaran vimezuia mwafrika hasitengeneze gari? 😂
 
Mbona wanyama wabateseka, wameumbwa ili wateseke? Wengine wanawindwa na kuliwa na wanyama wenzao, wengine wanawindwa na binadamu kwa mahitaji mbalimbali sasa nao kosa lao ni nini mpaka wapitie kashkash zote hizo?
Hawana consciousness kama ya binadamu
 
Biblia na Quaran vimezuia mwafrika hasitengeneze gari? 😂
Walipotuwin wazungu waliwai kupata taarifa kuhusu habari za Mungu. Na kuna maarifa walituficha.

Mzungu yeye amepambana kuna mambo muafrika hasiyatambue. Na ametufundisha namna ya kukataa vya kwetu vya asili tulivyopewa na Mungu, tusadiki vya Mzungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…