Joh Makini, sitokusamehe kwa kutuharibia mziki wetu Nako 2 Nako Soldiers

Joh Makini, sitokusamehe kwa kutuharibia mziki wetu Nako 2 Nako Soldiers

"Look, if you had, one shot, or one opportunity
To seize everything you ever wanted. In one moment
Would you capture it, or just let it slip?"

Huwezi choshwa na lyrics kama hizi za Eminem kamwe

Sawa, sauti yake kali mno.... mtazamo wangu.
 
Watanzania tunapenda sana lawama. Kiufupi Joh kawasaidia sana N2N kuendelea kuwa kwenye ramani, maana baada ya kina Lord Eyes kuwa mateja walikuwa washapoteana, so alipoanza kushirikiana nao kwenye kazi tukaendelea kumsikia GNako akiendelea kuliwakilisha kundi. Joh anaanzaje kuwahofia N2N wakati yeye tu kama Solo ana hits nyingi na kubwa kuliko hilo kundi?
 
Umemkosea sana heshima Eminem kumfananisha na huyu mpuuzi 69 au na ww upo upande Diddy hamkubali eminem.
[emoji16][emoji16][emoji16]yaani yule mpumbavu sijui ndio freemason ama ndio wakati umefika!!!
Hip hop nayo imewekwa sukari siku hizi,wengine wanaongeza na rangi ndio hawa kina tekashi 69.
 
Nimesoma Uzi wako mpaka hapo uliposema Humpendi Eminen nimejua wewe hujui lolote kuhusu hii tasnia..

Endelea kupenda singeli.

Ni sawa mkuu, siijui tasnia kivile ila nina machaguo yangu.... sipendi kufokewa!

Michano iliyotulia, ndo maana nimemkubali LordEyez na Jombii sio JCB... vivyo hivyo kwa Eminem.

Sina tatizo na legacy yake!
 
Ni sawa mkuu, siijui tasnia kivile ila nina machaguo yangu.... sipendi kufokewa!

Michano iliyotulia, ndo maana nimemkubali LordEyez na Jombii sio JCB... vivyo hivyo kwa Eminem.

Sina tatizo na legacy yake!
Acha linganisha Slim Shady na takataka
 
[emoji16][emoji16][emoji16]yaani yule mpumbavu sijui ndio freemason ama ndio wakati umefika!!!
Hip hop nayo imewekwa sukari siku hizi,wengine wanaongeza na rangi ndio hawa kina tekashi 69.

[emoji1][emoji1][emoji1] Ngoja tuone anafika wapi uwezo wake tutajua mpaka atakapo toa album ndio tutajua ukubwa wake.
 
Ktk Dunia hii, Nawapenda wanaume 3 tyuuh.
> G Nako
> Geofrey lea
> Chris Brown

Nawapenda hawa viumbe hadi nahisi uchizi kabisaaah.
Ukinipata au ukiniona utajuta kwa nini hukunijua mapema. Hao wanachonizidi ni jina tu.

Pamoja na hilo I do appreciate the fact that G Nako is a piece of machinery on choruses.
 
Hapa unamuonea Joh

N2N walianza kujifia kabla hata Weusi haijazaliwa

Enzi N2N inatamba weusi haikuwepo, kulikua na Joh aka Rapture akiwa solo na akina Nikki chini River camp soldiers..... halikia kundi la mziki bali kijiwe tu cha wana wanachana

Ibra akalianzisha N2N akajitoa na Lod izy akazama kwenye mihadarati kundi likafa

Weusi ilianza kama collabo na baada ya kuendana wakaunda kundi rasmi Joh nikki na gnako na baadae loyd izy

Hakujawahi kuwa na ushindani kati ya kundi la weusi vs liver camp
 
Salamu zikufikie,

Unajiita Mwamba, ni kwa ujanja wa nje uliofanikisha kumzima mpinzani baada ya kuangushwa vibaya ulingoni.

Wadau na walio timamu watakumbuka hili, Joh Makini na timu yake River Camp Soldiers. Si ajabu usikumbuke ngoma yoyote kali kutoka kwenye kundi hili, kama ipo tusaidiane.

River Camp Soldiers ikiongozwa na Joh Makini, na mdogo wake Nikki, Bonta na wengine kama wapo (wasiojulikana), haikuwa na maajabu kama kundi.

Sana sana ilitumika kumbeba Joh kwa kiasi kikubwa, huku akiibatiza majina mbalimbali kwa vipindi tofauti (Mfano Good Music Family ‘GMF’ hadi Ngumu Nyeusi ‘WEUSI’) lakini yote haikufua dafu.

Wakati huo akichezea ‘vitasa’ vikali kutoka kundi hasimu Nako 2 Nako Soldiers, likiongozwa na Lord Eyez, G Nako, Bou Nako na Ibra da Hustler.

Kama kundi walikuwa wakitamba kwa kila ngoma waliyoachia, walitamba na hakika walikosa upinzani, labda kwa mbaaali Kikosi Cha Mizinga ya Kalapina.

Kwa uchache tu nikukumbushe ngoma kali kama Ndo Zetu, Mchizi Wangu, Hawatuwezi, Bang! Hapo sijasahau Mchizi Wangu Remix, ni kwa vile nimeahidi kutaja mawe kwa uchache.

Joh Makini aliona kabisa mazishi haya hapa, ikabidi atumie ujanja na akili kubwa ili kujipatia ushindi wa mezani, nje ya uwanja.

If you can’t beat them, join them. Ndiyo turufu aliyotumia Joh Makini.

Akavizia kipindi Lord Eyez yupo ‘high’ kwa mihadarati, akamsajili kiungo wake mchezeshaji G Nako. Na kwa fitina nyingi kuhakikisha timu zinaungana ili awe kiongozi.

Hebu fikiria, Nako 2 Nako imesambaratika kipindi ambacho imepata ‘lebo’ Bongo Records kwa Godfather Majani, hii inawezekenaje!

Na hapo tayari wamesharekodi album nzima, wimbo pekee uliosikika kutoka album hiyo ni HAWATUWEZI, fikiria ngoma kali kiasi gani zimefia studio kwa Majani!

Sasa we jamaa Joh Makini, Mwamba, umeua ushindani kisha ufurahie tu kuwa kiongozi wa kundi lisilo na maana!

Hizi nyimbo zenu uchwara Wapoloo sijui Gere sijui Arosto kabisa unaona ni hadhi ya Lord Eyez au unamkomesha kijanja!

Nako 2 Nako tunawadai ngoma kali, lawama zote ni kwako Mwamba, binafsi sitokusamehe!

Bring back our NAKO SOLDIERS!
Fido vato bana acha utoto
 
Joh makini haez wafikia waturutumbi,watengwa, na katuulia nako to nako yetu. Yani kwa kifupi kina stoper, Davi, jcb,chindo, spacdawg. Na hapo kwenye hiyo weusi ndo anamlalia Isaa( Lord eyes), Isaa sijui kwann haskii anakomeshwa tu pale. Ye ni mkuubwaa kuliko huyo mwamba
Wangekuwa wakubwa tungewasikia Tanzania nzima. Hao kina spacdawg wanajulikana baadhi ya mitaa tu ya Arusha mjini.
 
Back
Top Bottom