Wanaodai Serikali inaficha au inachakachua takwimu ni upinzani. Najiuliza, iwapo kila Chama cha Siasa kina mashina, iweje wasiwe na takwimu sahihi? Au wanasubiri matokeo ya kura za uchaguzi wadai kuwa wameibiwa ati wao wanazo zilizo sahihi. Kwa kura inawezekana kuficha lakini kifo cha binadamu hakifichwi.
Hivyo basi natoa changamoto kwa kila member wa JF, ataje vifo vya nyumbani kwake, mtaani na ukoo, tutapata takwimu sahihi. Nyumbani kwangu, jirani, mtaani na ukoo hakuna aliyeathirika au vifo hadi sasa. Maisha yanaendelea kama jana na juzi hata kesho, kwa ulinzi wake Mungu.
Tanzania bila COVID-19 yawezekana, kama inavyojihirisha hadi sasa.
JIKINGE UMKINGE JIRANI
JILINDE UWALINDE WAPENDWA WAKO