Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Nakujibu kama shabiki wa CCM. Mimi sijibishani na CCM au Serikali bali apologists wao ambao hawataki wakosolewe.Mkuu, Katiba Mpya haitapatikana kwa azimio la CC ya CHADEMA. Process ya kufanya mabadiliko ya Katiba inasimamiwa na Bunge la JMT kupitia sheria ya Bunge inayotungwa kwa ajili hiyo.
CHADEMA wamepata wapi kura Bungeni za kuwawezesha kutunga sheria itakayosimamia mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwa namna wanayotakata wao? Ndiyo maana nakuambia CHADEMA watapiga pesa kisha wasepe bila Katiba Mpya kupatikana, kama walivyofanya 2015!
BTW, kweli sikubaliani na CHADEMA katika maeneo mengi, lakini mimi sio CCM wala Serikali ya CCM. Naona unanijibu kama vile unaijibu CCM au Serikali ya CCM.
Ingekuwa Chadema inaamini kuwa Katiba Mpya itatokana na maazimio yao wala wasingejisumbua kuzunguka nchi nzima kuomba wananchi wasimame nao katika juhudi zao za kudai Katiba mpya.
Chadema wanajua bunge lililopo haliwezi kuwaunga mkono kwenye hili. Lakini kwa vile bunge linapata uhalali kutoka kwa wananchi, wananchi wakiamua kuwa wanataka Katibu hawatazuiwa na bunge.
Hizo pesa unazodai Chadema watapiga zinatoka wapi? Mwaka 2015 walijitoa baada ya kuona bunge la wakati ule linataka kubadilisha matakwa ya wananchi kwa faida ya chama chao. Na waliamini naively kuwa Rais yeyote atakaekuja ataendelea na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya. Na mpaka sasa hamna Rais aliyesema hataki Katiba Mpya. Wanachosema ni kuwa Katiba Mpya sio priority kwao. Waaminiwe kuwa wakati muafaka ukifika itajadiliwa. Lakini hawatoi timeline ya huo wakati muafaka utafikiwa lini na nani ataamua kuwa ndio wakati muafaka.
Ni kweli kuwa Katiba Mpya haiwezi kupatikana bila CCM kuunga juhudi. Na kwa vile iliyopo inakipa privilege kubwa, njia pekee ya kukifanya chama hicho kukubali mabadiliko ya maana ni ile itakayotokana na presha kutoka kwa wananchi na sio chama chochote cha siasa. Ubaya kwa CCM ni kuwa siku hiyo ikifika, kitatoka madarakani na hakitarudi tena na historia yake itakuwa tainted for ever. Inawezekana wengi wetu hatutaiona hiyo siku lakini itakuja tu na Chadema na wengine watakumbukwa katika historia kuwa walisimamia haki ya wananchi kupata Katiba inayo reflect mahitaji yao.
Amandla...