Mwanzi1
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 6,000
- 4,589
Huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu. Naona unazungumza inavyotakiwa kuwa na sio ilivyo. Hiyo kupata nguvu ya kuongea kutoka kwa wananchi ni iwapo uchaguzi unaheshimiwa, na sio yale maagizo aliyotoa Magufuli kwenye uchaguzi. Huko nyuma unapozungumza ccm walikuwa wanapita zaidi ya 30% bila kupingwa? Huko nyuma ulikuwa unakuta Karatasi la kura rais aliye madarakani jina lake linakuwa juu bila kufuata alphabet za chama? Huyo mama hana hisani yoyote anatoa maana anajua fika hakukuwa na uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Kwa mawazo haya sidhani kama mtafika 2024. Mnahitaji muujiza wa hali ya juu kutoka kwenye fikra tofauti ikimaanisha uongozi mpya na sio wa kiharakati). Huwezi kusema jina la rais liko juu na huku umeweka sahini ya kukubali kanuni zote za uchaguzi halafu unapindukia pale tuu ukishindwa uchaguzi. Karatasi za kura zinaangalia vigezo vingi pamoja na kupuguza makosa ambayo mpiga kura anaweza kukosea kama majina ya wagombea wawili wenye mvuto wakiwa karibu-karibu. Nashukuru Mama mmarekani wamewapa somo na mpaka sasa akili zinaanza kuingia, hakuna njia ya mkato na kutegemea nguvu ya nje kwenye kupambania haki.